Maelezo ya jumla kuhusu ugonjwa wa klamidia

Ugonjwa wa klamidia ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na bakteria. Mara nyingi hauna dalili. Unaweza kusababisha maumivu wakati wa kukojoa, usaa utoka kwenye uume ama uke, au maumivu kwenyi pande ya chini ya tumbo ya mama. Unaweza kuwa hatari kwa maana unaweza kusababisha maumivu ya kiuno kwa wakinamama na unaweza kusababisha ugumba kwa wakinababa na wakinamama ikiwa hawakutibiwa. Unatibiwa na antibiotiki.

Ugonjwa wa klamidia unaenezwaje?

  • Ngono ya ukeni, mdomoni (na mara chache), kupitia njia ya haja kubwa
  • Kushika macho kwa mikono yenye maji maji yenye uambukizo.
  • Kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto- wakati wa kujifungua.

Dalili za ugonjwa wa klamidia

Uvimbe kwenye via vya uzazi. Muda haujulikani. Dalili zingine kuanzia siku 7-14.

  • Wanawake: hakuna dalili kwa wanawake 4 kati ya 5.
  • Kama mlango wa kizazi umeathirika, uchafu hutoka ukeni, kuhisi maumivu wakati wa kukojoa, kutokwa damu ukeni kusiko kawaida, kutokwa na damu baada ya kufanya ngono.
  • Kama ni uvimbe wa fupanyonga (PID): kutokwa damu na maumivu chini ya tumbo. Mlango wa kizazi huonekana kuvimba. Uvimbe kwenye njia ya haja kubwa (proctitis)
  • Wanaume: uume kuwaka moto, kutokwa na uchafu kwenye uume. Kunaweza kusababisha uvimbe kwenye njia ya mkojo. (urethritis).

Vipimo/Tiba ya klamidi

  • Vipimo
  • Wanawake: uchunguzi wa sampuli ya fupanyonga; kipimo cha mkojo.
  • Wanaume: sampuli ya njia ya mkojo, kipimo cha mkojo.
  • Vinaweza vikawatatanisha na kisonono. Fanyiwa vipimo vya haya magonjwa yote – kisonono na klamidia.
  • Tiba:

Madhara ya ugonjwa wa klamidia

  • Wanawake: Uvimbe wa via vya uzazi unaweza kusababisha maumivu sugu ya nyonga, utasa, matatizo ya ujauzito (utungaji wa mimba nje ya kizazi).
  • Wanaume: Uvimbe kwenye mirija ya mbegu za uzazi, Korodani na tezi kibofu.
  • Watoto wachanga: Hupata uambukizo wakati wa kuzaliwa, kupata uambukizo kwenye macho na nyumonia.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/chlamydiainfections.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *