Via vya uzazi

Inashauriwa kuweka safi mavuzi na via vya uzazi. Faida za kuweka safi via vya uzazi ni:

  • Kuzuia kusambaza magonjwa
  • Kuzuia wadudu kukua hapo
  • Mahusiano mazuri na mwenzi wako
  • Kuzuia harufu mbaya

Kunyoa mavuzi ni moja ya njia ya kuweka safi via vya uzazi. Inazuia uwezekano wa kutunza wadudu na kufanya iwe rahisi kusafisha. Usafi wa via vya uzazi unaweza kufanyika wakati unapooga au unapoosha sehemu nyingine za mwili. Lakini kuna wakati ambapo utahitajika kusafisha sehemu za siri pekee. Kama vile:

  • Kabla na baada ya kushiriki ngono: Hii itaweka safi sehemu za siri safi ili kuzuia harufu mbaya
  • Baada ya kufika mshindo: Wakati mwingine wanaume wanaweza kufika mshindo wakiwa usingizini. Kwa hali kama hii unapswa kujisafisha.
  • Wakati wa kupata damu ya hedhi: Wanawake wanapswa kusafisha sehemu za siri mara kwa mara katika kipindi hiki.
  • Kabla na baada ya kujifungua: Kusafisha mara kwa mara sehemu za siri kabla a kujifungua, kutaweka mazingira mazuri na kuzuia karaha kwa mtu anayekusaidia wakati wa kujifungua. Baada ya kujifungua, ni muhimu kujisafisha mara kwa mara ili kuzuia harufu mbaya.

Kujihudumia wakati wa hedhivia vya uzazi

Ni hali ya kawaida kwa wanawake kupata damu ya hedhi kila mwezi baada ya umri wa balehe. Ili kuweka safi mazingira ya via vya uzazi, ni muhimu kutumia vitambaa safi na laini. Matumizi ya vipande vya nguo yanashauriwa hasa kama pad zilizotengenezwa kwa pamba ni adimu. Vitambaa vinapswa kubadilishwa na kuoshwa mara kwa mara. Vitambaa vilivyokwisha kutumiwa vinapswa kulowekwa kwenye maji kwa muda na kisha kufuliwa kwa sabuni na kuanikwa nje ili kukauka. Kama unaweza kununua, tumia sanitary towel au lady pads. Vitambaa na pads zilizotumika zinapaswa kuchomwa au kuzikwa ili wanyama na watu wasikutane nazo.

Jifunze zaidi hapa kuhusu kusafisha;

Vyanzo

https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/conditionsandtreatments/personal-hygiene

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *