Maelezo ya jumla

Ukianza kupata vidonda mdomoni unaanza kuwa na maumivu kama umeungua moto, kisha unapata kishimo kidogo cha rangi ya hudhurungi au nyeupe, ambacho baadae hubadilika rangi na kuwa chekundu. Vidonda vya mdomoni huwa vinajirudia rudia lakini haviambukizi. Vidonda vya mdomoni ni rahisi sana kuwapata watu ambao wana msongo mkubwa wa mawazo au waliochoka sana kwa shughuli wanazofanya. Baadhi ya wanawake wanapata vidonda vya mdomoni kabla ya hedhi. Kama una meno ya bandia au vifaa vya kutegemeza meno ambayo havikai vizuri au kama unapiga mswaki vibaya na kwa nguvu, unaweza pia kusababisha vidonda mdomoni. Kwa mara chache, vidonda mdomoni vinaweza kusababishwa na kansa.

Mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama

  • Unajihisi kuugua au/na una homa
  • Unapatwa na vidonda vingi kwa wakati mmoja
  • Umekuwa na kidonda mdomoni kwa zaidi ya wiki 2 au/na kama kinaongezeka ukubwa

Unachoweza kufanya mwenyewe ukiwa na vidonda mdomoni

Kidonda cha kawaida cha mdomoni huwa kinapona baada ya wiki moja au mbili baada ya matibabu, lakini kwa wakati huu wote, kidonda kinaweza kuleta karaha sana. Unaweza kujaribu njia zifuatazo ili kupunguza maumivu na kusababisha kidonda kipone haraka iwezekanavyovidonda mdomoni

  • Kula vyakula laini, vyakula vinavyotuliza kama vile yorgut na ice cream. Kunywa maji au vinywaji vingine kutumia mrija.
  • Epuka kula vyakula ambavyo vitachachawisha mdomo na kuumiza vidonda, vyakula vyenye chumvi nyingi na pilipili, vyakula vigumu kama vile karanga, viazi vibichi au vigumu na vyakula au vinywaji vya moto sana , matunda kama vile machungwa na limao na vinywaji kama vile kahawa.
  • Safisha meno kwa kutumi mswaki laini
  • Unaweza kutumia dawa ya kuskutua meno ‘’antiseptic mouth wash’’- unaweza kusukutua mdomo kwa kutumia dawa ya kuskutua ili kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi kwenye kidonda, hii itasaidia kidonda kupona haraka
    • Kama mbadala unaweza kutengeneza mchanganyiko maalumu ili kusukutua, unaweza kuchanganya maji na chumvi ili kutengeneza dawa ya kusukutua.
    • Weka nusu kijiko (kijiko cha wali) cha chumvi kwenye maji yaliyojaa kwenye kikombe (kikombe kiwe cha ujazo wa 250ml).
    • Maji yawe ya uvuguvugu na unaweza kusukutua mara kadhaa. Sukutua kwa angalau sekunde 30 na kisha tema.
  • Unaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu ya mdomoni kwa kutumia madawa maalumu yenye kutia ganzi vidonda mdomoni
    • ‘’Local anesthetic benzocaine’’ inasaidia kupunguza maumivu kwenye vidonda vya mdomoni. Mchanganyiko huu unapatikana madukani kama dawa ya maji au gel.
    • Usitumie mara kwa mara dawa hizi, zinaweza kuongeza harara, kuwa makini unapozitumia
    • Usitumie dawa hizi kwa zaidi ya siku 7, isipokuwa kama umeelekezwa na daktari

Mwone daktari kama una vidonda mdomoni na

Panga kumwona daktari kama

  • Una maumivu makali ambayo hayaishi hata baada ya kufanya njia zilizoelekezwa hapo juu
  • Unapata shida kumeza
  • Kidonda hakijapona baada ya wiki 2 au kama unaona kinaongezeka ukubwa
  • Unapatwa na vidonda mara kwa mara

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001448.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *