Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa amiba (Amoebiasis) ni ugonjwa wa matumbo unaosababishwa na vimelea vya Entamoeba histolytica.

Je! Ni nini dalili za ugonjwa wa amiba?

Kwa kawaida, ugonjwa huu hudumu kwa wiki mbili, lakini unaweza kurudi ikiwa hautatibiwa vyema.
Dalili zisizo kali ni:

Dalili kali:

Kumbuka: 90% ya watu wote wenye ugonjwa wa amiba hawana dalili yoyote.

Ni nini kinachosababisha Ugonjwa wa amiba?

Entamoeba histolytica ni kimelea anaeweza kuishi kwenye utumbo mkubwa (koloni) bila kusababisha ugonjwa. Hata hivyo, wakati mwingine, huvamia kuta za koloni na husababisha uvimbe, kuhara damu au kuhara kwa muda mrefu. Maambukizi yanaweza pia kuenea kupitia damu mpaka kwenye ini na, kwa mara chache, kwenye mapafu, ubongo na viungo vingine. Hali hii inapatikana mahali popote ulimwenguni, lakini inapatikana zaidi katika maeneo ya kitropiki, yenye msongano mkubwa wa watu wanaoishi katika mazingira duni na yenye usafi hafifu. Afrika, Mexiko, sehemu za Amerika ya Kusini, na India zina matatizo makubwa ya kiafya yanayohusiana na ugonjwa huu. Entamoeba histolytica inaenea kwa njia ya chakula au maji yaliyochafuliwa na kinyesi. Hii inatokea zaidi kama kinyesi cha binadamu kinatumika kama mbolea.

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa amiba?

Sababu zifuatazo zinakuweka katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa amiba kali :

  • Ulevi
  • Saratani
  • Utapia mlo
  • Uzee
  • Mimba/Ujauzito
  • Kuishi katika maeneo ya kitropiki kama Tanzania
  • Kutumia dawa aina ya corticosteroid zinazopunguza kinga ya mwili

Utambuzi wa ugonjwa wa amiba

Uchunguzi wa tumbo unaweza kuonesha ini lililovimba au tumbo linalouma sana likiguswa. Vipimo hujumuisha :

  • Vipimo vya damu ili kutambua amiba (serology)
  • Uchunguzi wa sehemu ya ndani ya utumbo mkubwa kwa kutumia kamera (sigmoidoscopy)
  • Uchunguzi wa kinyesi kwa kutumia darubini

Ukiwa na amiba ni wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone mtoa huduma wako wa afya ikiwa unaharisha.

Kuzuia ugonjwa wa amiba

Weka mazingira yako kuwa safi , kunywa maji yaliyosafishwa au yaliyochemshwa, usile mboga ambazo hajipikwa vyema na osha matunda kabla ya kuyala. Maji yanayotumiwa na wanajamii yanapaswa kutibiwa na mfumo wa maji taka kudhibitiwa.

amibaUchaguzi wa matibabu

Madawa hutumika kutibu amiba. Uchaguzi wa madawa hutegemea ukali wa maambukizi. Dawa za kumeza za Metronidazole hutumiwa kwa siku 10 kwa maambukizi yasiyo makali. Kama unatapika, unaweza kuchomwa sindano kwenye mshipa mpaka utakapoweza kumeza dawa. Dawa za kupunguza kuharisha mara nyingi hazipendekezwi maana zinaweza kusababisha hali kuwa mbaya zaidi. Baada ya matibabu, kinyesi kinatakiwa kupimwa tena ili kuhakikisha kuwa umepona.

Nitarajie nini nikiwa na ugonjwa wa amiba?

Matokeo ni mazuri baada ya matibabu.

Matatizo yanayoweza kutokea

  • Jipu la ini
  • Madhara yanayotokana na madawa, ikiwa ni pamoja na kichefuchefu
  • Kuenea kwa vimelea kupitia damu mpaka kwenye ini, mapafu, ubongo, au viungo vingine

 

YAFUATAYO NI MAELEZO YA ZIADA KWA UFUPI

Ugonjwa wa amiba ni maambukizi yanayosababishwa na kimelea aina ya protozoa anayesababsha matatizo ndani na nje ya utumbo

Sababu za ugonjwa wa amiba

Entamoeba histolytica

Epidemiolojia ya ugonjwa wa amiba

  • Unatokea duniani kote, hasa maeneo ya kitropiki.
  • Unatokea zaidi maeneo yenye uchumi duni, kwenye taasisi za wagonjwa wakili na watu wanaoshiriki ngono ya jinsia moja
  • Ugonjwa mkali wa amiba unawapata zaidi vijana.
  • Ni kwa nadra chini ya miaka 5 ya umri, na hasa chini ya miaka 2

Njia ya uambukizo ya ugonjwa wa amiba

Kwa kula chakula au kunywa maji yaliyochafuliwa kwa kinyesi chenye mayai ya vimelea vya amiba

Muda mpaka dalili za ugonjwa wa amiba kuanza kuonekana

Inategemea, kuanzia siku kadhaa mpaka miezi kadhaa au miaka; kwa kawaida ni wiki 2 – 4.

Muda wa uambukizo wa ugonjwa wa amiba

Mtu anaweza kuendelea kuambukiza wengine kwa kipindi chote anachotoa mayai ya Entamoeba histolitica kwenye kinyesi, na hii inaweza kuwa kwa miaka mingi

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa ugonjwa wa amiba

Watu wote

  • Mchakato wa uambukizo – life cycle
  1. Unapokunywa au kula chakula kilichochafuliwa na mayai
  2. Mayai yanaanguliwa tumboni na kutoa vilimbwende vinavyoitwa trophozoites
  3. Trophozoites zinazaliana na kuongezeka tumboni
  4. Trophozoites zinajitengenezea gamba na kuwa yai
  5. Mayai yanatoka nje kwenye kinyesi
  6. Kinyesi chenye mayai kinachafua mazingira tayari kwa uambukizo

Dalili za ugonjwa wa amiba

  • Inaanza na vipindi vya kuhara, maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kutapika na hisia kuwa unataka kujisaidia haja kubwa na wakati hakuna kitu.
  • Ukianza kupata kinyesi cha damu, kinyesi kwa kawaida kinakuwa cha majimaji chenye kamasi kamasi na damu.

Utambuzi wa ugonjwa wa amiba

  • Kunakuwepo na mayai au trophoites wa Entamoeba histolytica kwenye kinyesi

Matibabu ya ugonjwa wa amiba

Metronidazole au Tinidazole

Kuzuia ugonjwa wa amiba

  1. Kutibu kikamilifu wagonjwa
  2. Kuwezesha upatikanaji wa maji safi
  3. Matumizi bora ya choo na kunawa mikono baada ya matumizi ya choo
  4. Kuosha vizuri mbogamboga kabla ya kuzila – hasa kama unakula mbichi

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000298.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *