Mambo 10 mzazi anayopaswa kuongea na mwanae kuhusu bangi

  1. Bangi sio dawa ya kawaida kama dawa nyingine. Ubongo wa vijana wanaobalehe bado unakua, na kuvuta bangi kunaweza kusababisha ubongo kukua vibaya.
  2. Vijana walio kwenye balehe wanaotumia bangi mara kwa mara wanapatwa na matatizo ya akili, ikiwa ni pamoja na uraibu, sonona na wendawazimu.
  3. Hakuna tafiti za kuaminika kuhusu matumizi ya bangi kwa vijana walio kwenye balehe, kwa hiyo sababu za matumizi zinazofaa, kiwango cha bangi kinachotosha, madhra na maudhi yanayoweza kutokea hayafahamiki vizuri sana.
  4. Matumizi ya bangi kwa watoto na vijana wadogo ni kinyume na sheria ya nchi yetu, na akifunguliwa mashtaka inaweza kuathiri mwenendo wake wa shule, kazi n.k.
  5. Usiendeshe gari ukiwa umevuta bangi au usipande gari la dereva unayefahamu amevuta bangi. Vijana na watu wazima hupata ajali mbaya kwa sababu ya kuendesha baada ya kuvuta bangi.
  6. Moshi wa bangi ni hatari, sawa na moshi wa tumbaku.
  7. Kwa wazazi; Wewe ni kioo cha mtoto wako, na matendo yako yanafundisha mengi kuliko maneno. Kwa hiyo, usivute bangi mbele ya watoto. Ni rahisi watoto kuiga kutoka kwako, haijalishi kama umewaambia wasivute.
  8. Kwa wazazi: Ni muhimu kutunza mbali na watoto bidhaa zote za bangi. Kama ilivyo kwa dawa nyingine na sumu nyingine, zitunze mbali na watoto. Kumbuka; sheria ya nchi yetu inakataza kuvuta bangi.
  9. Kwa wazazi:Kumbuka kuwa kujihisi raha ni sehemu ya matokeo ya kuvuta bangi. Kuvuta bangi kunaweza kusababisha ukafanya maamuzi yasiyo sahihi kama mzazi au ukashindwa kuweka mazingira salama kwa ajili ya mwanao, hasa akiwa mtoto mchanga.
  10. Kwa wazizi: Kama mtoto wako akikuuliza moja kwa moja kama umewahi kutumia bangi, jibu fupi na la ukweli litatosha kumfanya mtoto awe huru kuzungumza na wewe kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya. Hata hivyo ni bora kuepuka kumsimulia habari zako za kipindi ukitumia bangi. Ni bora kuzungumza nae kwa kutoa mifano, itasaidia.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001975.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *