Maelezo ya jumla

Chawa wa nywele kichwani ni wadudu wenye rangi ya kijivu–kahawia, wanalingana ukubwa na mbegu ya ufuta. Wanaishi kwenye nywele, hasa kwenye shina la nywele karibu kabisa na ngozi ya kichwa. Wanatotoa mayai na yakianguliwa yanatoa chawa wengine wadogo.  Wakishaanguliwa, wanaacha maganda ya mayai meupe, yakiwa yamegandia kwenye shina la nywele. Ukiyaangalia maganda ya mayai ya chawa yanaonekana kama mba, lakini inakuwa ngumu kuyaondoa hata ukichana nywele. (ni rahisi kuondoa Mba kuliko haya mayai ya chawa).
Kwa sababu chawa wa nywele kichwani wanaweza kuruka kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa urahisi, hasa kwa watu wanaoishi pamoja au wanaokutana mara kwa mara. Chawa wanaweza kumpata mtu yeyote, lakini watoto ndio huathirika zaidi na shida  hii. Mwanao akiwa na chawa wa nywele kichwani utamwona akikuna kichwa mara kwa mara. Mwasho huu unaweza usianze mpaka chawa wakiwa wengi kichwani.

Mwone daktari kama:

Unapaswa kupanga kumwona daktari kama hauna uhakika kuwa ulio nao ni chawa au shida nyingine au kama una chawa na unashindwa ni dawa gani au njia gani utumie kuwaondoa

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kuondoa chawa kichwani

Unaweza kuwaondoa chawa wa nywele kichwani mwenyewe, lakini ni muhimu ujue kuwa utahitajika kujitibu kama utakuta chawa wakiwa hai, kama wamekufa hauhitaji kujitibu

Hatua ya 1

  • Hatua ya kwanza ni kuwatambua chawa, fanya yafuatayo ili kujua kama una chawa au la: (utahitaji mtu mwingine akusaidie kukagua nywele, ni vizuri kuomba msaada)
    • Sio rahisi kuwaona chawa kwa kuangalia tu nywele kwa macho, kwa hiyo fuata hatua zinazofuata hapa ili kujihakikishia. Inaweza kukuchukua kama dakika 15 -30 hivi
    • Kama una nywele ndefu paka shampoo nywele na kisha zisuuze, baada ya hapo zipatie conditioner ya kutosha na kisha chana kwa chanuo ya kawaida vizuri
    • Chukua chanuo yenye meno yaliyo karibu karibu sana, iweke hiyo chanuo chini kabisa kwenye mizizi ya nywele kisha ilaze kabisa chali kwenye ngozi ya kichwa, baada ya hapo anza kivuta kuja juu mpaka kwenye ncha ya nywele.

chawa wa nywele kichwani

    • Kila unapochana nywele kutoka chini mpa juu, kagua kichanua na kama kuna chawa waondoe kwa kufutie kwenye kitambaa maalumu ulichoandaa
    • Hakikisha unachana kichwa kizima bila kuacha mahali, unapokuwa unachana nywele , tunashauri ujifunike kwa taulo nyeupe ili kama chawa wakianguka unapokuwa unachana nywele uweze kuwaona na kuwaondoa
    • Kama umekuta chawa baada ya kuchana nywele, suuza tena nywele, ziache zikauke na baada ya hapo kuna njia mbili za kupambana na hao chawa
    • Moja ya hizo njia ni kupaka mchanganyiko maalumu wa kuua chawa na nyingine ni kuchana nywele mpaka uwatoe chawa wote waishe kwenye nywele

Hatua ya 2

  • Ukikuta kuna chawa walio hai kwenye nywele unaweza kusuuza nywele, kisha ukarudia kuchana tena nywele. Rudia kama mara 3 hivi kila baada ya siku 4. Kama utakuta chawa ambao wako hai tena baada ya kurudia kuchana nywele rudia tena kucha mara tatu kila baada ya siku 4 mpaka utakapo ona hakuna chawa wowote
  • Kama wakati wa kukagua umekuta kuna chawa walio hai, wakague na wanafamilia wengine na waambie watu wote ambao walikuwa karibu nawe au mtoto mwenye chawa kichwani ili na wao watibiwe ikilazimu
  • Kama utaamua kutumia mchanganyiko maalumu kuua chawa, kwa kawaida utatakiwa kuupaka huu mchanganyiko kwenye nywele na kichwa kizima, kisha unauacha kwa muda (muda unategemea unatumia bidhaa gani, hakikisha unasoma vizuri maelekezo). Baada ya hapo shampoo nywele na kisha unachana nywele ili kuwaondoa chawa walio kwisha kufa. Unaweza kuhitaji kupaka dawa tena kwa mara ya pili
  • Kama una ujauzito au kama unanyonyesha mtoto au kama unataka kumtibu mtoto aliye na miezi chini ya miezi 6, ni bora usitumie mchanganyiko wa kuua chawa. Baadala yake, tumia njia ya kuchana nywele, njia ya kuchana nywele ni mbadala mzuri kama hauhitaji kutumia madawa ya kuulia wadudu
  • Chawa wa nywele kichwani huwa wanakufa haraka baada ya kutolewa kichwani, lakini kwa tahadhari ni vizuri kuosha vizuri brashi, vitana, chanuo, taulo na hata vitambaa vya mito, ni vizuri msichangie kofia, skaff, vitana na chanuo na mtu mwingine

Unahitaji msaada wa daktari kama:

Ni vizuri kupanga kumwona daktari kama:

  • Kama utakuta kuna chawa walio hai kichwani baada ya kutumia mchanganyiko wa kuua chawa siku 2 au 3 baada ya kupaka dawa
  • Kama utakua chawa walio hai kwenye nywele baada ya kutumia njia ya kuchana nywele kuwaondoa mara kwa mara kwa muda wa wiki 2

Vyanzo

https://medlineplus.gov/headlice.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *