aMaelezo ya jumla

Damu kwenye mkojo (mkojo wenye damu) ni hali ya kuwepo seli nyekundu za damu kwenye mkojo. Kama kiasi cha damu kilichopo kweny mkojo ni kidogo sana, mkojo unaweza kuonekana wa kawaida, lakini chini ya darubini inaonekana. Mtu mwenye kiasi kingi cha damu kwenye mkojo, inaweza kuonekana kwa macho bila kutumia darubini. Mkojo unaweza kuwa mwekundu au wenye rangi kama soda ya cocacola

Ni zipi dalili za damu kwenye mkojo ?

  • Kutokwa na mabonge ya damu au mkojo unaoonekana na rangi nyekundu sana
  • Kutokwa na mawe kwenye mkojo
  • Inaweza kutokea asubuhi sana au siku nzima
  • Unaweza kuwa na maambukizi au historia ya kuwa na maambukizi ya kwenye koo hivi karibuni

Ni nini husababisha mkojo wenye damu?

Kuna matatizo kadhaa yanayoweza kusababisha damu kwenye mkojo , mengi yao ni matatizo ya kawaida. Kwa mfano, mazoezi yanaweza kusababisha ukakojoa damu, na inaisha ndani ya masaa 24. Watu wengi wanapata mkojo wenye damu bila kuwa na tatizo jingine lolote. Mara nyingi hakuna sababu mahususi inayopatikana. Lakini kwa sababu damu kwenye mkojo  inaweza kuwa matokeo ya kansa au tatizo jingine baya, ni muhimu kuonana na daktari ili afanye utambuzi.

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata damu kwenye mkojo (mkojo wenye damu)?

Watu wa rika zote, hii ni pamoja na watoto, wanaweza kupata mkojo wenye damu. Baadhi ya mambo yanawea kuongeza uwezekano wa kupata damu kwenye mkojo .

  • Maambukizi ya hivi karibuni. Ugonjwa wa figo unaotokea baada ya kupata maambukizi – ugonjwa huu husababisha kuvimba kwa sehemu muhimu za figo na kusabisha damu kuchuja na kuingia kwenye mkojo – glumerulonphritis
  • Mazoezi: Watu wanaokimbia mbio za masafa marefu wako kwenye hatari zaidi ya kuwa na mkojo wenye damu
  • Umri: Kuongezeka kwa ukubwa wa tezi dume kwa wanaume wenye umri zaidi ya miaka 50 unaweza kusababisha damu kwenye mkojo
  • Jinsi: 50% ya wanawake wote wanapatwa na maambukizi kwenye njia ya mkojo angalau mara moja katika kipindi cha maisha yao, na maambukizi haya yanaweza kusababisha damu kwenye mkojo (mkojo wenye damu).

Utambuzi wa damu kwenye mkojo (mkojo wenye damu)Damu kwenye mkojo (mkojo wenye damu)

Ili kutambua sababu ya damu kwenye mkojo (mkojo wenye damu), au kutambua sababu nyingine zinazoweza kusababisha shida hii, daktari ataagiza ufanye vipimo mbalimbali, hii ni pamoja na kipimo cha mkojo, vipimo vya damu, kipimo cha picha za figo, na kuingiziwa kamera ndongo kwenye kibofu ili kuchunguza.

Kipimo cha mkojo ni kipimo kinachoangalia seli mablimbali na kemikali zilizo kwenye mkojo. Pamoja na kuangalia kama kuna seli nyekundu za damu, daktari anaweza kukuta kuna seli nyeupe za damu ambazo huashiria kuwa kuna maambukizi kwenye mkojo au anaweza kukuta seli zilizojiumba kama mirija ya figo (casts) – hizi huashiria kuwa kuna matatizo kwenye figo.

Vipimo vya damu vinaweza kuonesha kama kuna ugonjwa kwenye figo unaosababisha figo zishindwe kuchuja uchafu vizuri kutoka kwenye damu.

Kupiga picha za figo hujumuisha ultrasound, compterized tomography (CT) scan, intravenus pyelogram. Picha zote hizi zinafanyika ili kuangalia kama figo zina umbo sawia na zinafanya kazi ipasavyo. Kama una uvimbe, mawe kwenye figo, saratani, kuongezeka kwa ukubwa wa tezi dume, au sehemu yoyote iliyoziba; vipimo hivi vitasaidia kutambua.

Ni wakati gani unapaswa kumwona daktari haraka?

Damu kwenye mkojo haipaswi kupuuzwa hata siku moja. Ongea na daktari kuhusu dalili hii na pata vipimo vinavyohitajika, hasa kama unaona uzito wa mwili unapungua bila sababu ya msingi, kujisikia vibaya unapokuwa unakojoa, kukojoa mara kwa mara kuliko ilivyo kawaida, au kama unakimbia kwenda kukojoa / hauwezi kusubirisha mkojo.

Tafuta kuongea na daktari haraka sana kama:

Ongea na daktari pia kama:

  • Kama unapata maambukizi unapokuwa unashiriki tendo la ngono au unapata hedhi nzito sana – tatizo linaweza kuhusiana na via vya uzazi
  • Una mkojo unaodondoka kidogo kidogo bila kujizuia, unajikojolea wakati wa usiku, au unashindwa kuanza kukojoa – tatizo linaweza kuhusiana na tezi dume

Uchaguzi wa matibabu

Matibabu ya mkojo wenye damu yanategemea hali hii imesababishwa na nini. Kama sababu ni ya kawaida, basi hauhitaji matibabu yoyote.

Matarajio ya mgonjwa ni yapi?

Matarajio hutegemea ukali wa sababu ya tatizo la damu kwenye mkojo . Kutafuta sababu ya tatizo hili ndio huamua matarajio ya matibabu na ugonjwa.

Mtatizo yanayoweza kujitokeza?

Kwa sababu tatizo la mkojo wenye damu lina sababu nyingi, matatizo yanayoweza kujitokeza yatategemea sababu ya tatizo.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/lab-tests/blood-in-urine/

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *