Maelezo ya jumla
Darubini (Microscope) ni chombo kinachotumika kuangalia vitu ambavyo ni vidogo sana kuonekana kwa macho pekee . Sayansi ya kuchunguza vitu vidogo kwa kutumia chombo hiki inaitwa microscopy. Neno microscopic humaanisha vitu vidogo sana, visivyoonekana kwa jicho isipokuwa kwa msaada wa darubini.
Darubini ya kwanza iliyofaa kwa matumizi ilitengenezwa huko Uholanzi miaka ya 1600.
Aina ya kawaida ya darubini -na ya kwanza kutengenezwa-ni optical microscope. Darubini hii huwa na lensi moja au zaidi zinazokuza na kuzalisha picha ya kitu kilichowekwa ili kichunguzwe. Hata hivyo, kuna miundo mingine mingi ya darubini.