sMaelezo ya jumla
Fangasi ukeni aina ya canidida ni fangasi ambaye hukaa kwenye tabaka la juu la ngozi au kwenye utando ute, na kusbabisha kwepo utando mweupe mdomoni au kuvimba kwa uke.
Sababu za fangasi ukeni
- Candida albicans (inasabaisha zaidi)
- Candida tropicalis (mara chache inasabisha)
Epidemiolojia ya fangasi wa ukeni
Unapatikana dunia nzima. Fangasi aina ya candida albicans ni sehemu ya kawaida ya fangasi wanaopatikana mwilini ambao kwa kawaida huwa hawasababishi matatizo yoyote.
Uambukizo wa fangasi wa ukeni
Kukutana na majimaji kutoka mdomoni, ngozi, uke au kinyesi, kutoka kwa watu wenye ugonjwa au waliobeba fangasi hawa na hawana dalili. Unaweza kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.
Muda kabla dalili kuanza
Inategemea / hakuna muda kamili unaofahamika
Muda wa uambukizi wa fangasi wa ukeni
Tunafikiria kuwa mtu anaweza kuambukiza zaidi kama kuna vidonda
Nani yuko kwenye hatari ya kupata fangasi ukeni
Hatari ya kuambukizwa ni ndogo sana kwa watu wenye kinga imara ukilinganisha na wasio na kingamwili imara. Unatokea sana kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari. Wanawake walioambukizwa UKIMWI, wako kwenye hatari zaidi. Watu wanaotumia dawa za kupanga uzazi, watu wanotumia dawa aina ya steroid kwa muda mrefu wako kwenye hatari pia.
Dalili za fangasi ukeni
- Kuwashwa sana ukeni
- Kutoa majimaji ukeni (meupe, njano, mazito kama mtindi, hayanuki sana)
- Kuuma kwa uke kwa sababu ya kujikuna
- Kufanyiwa uchunguzi ukeni -speculum exam – kuna uchafu mweupe umejishikiza kwenye ukuta wa uke
- Ukijaribu kukwangua uchafu mweupe, damu inatoka mahali hapo lakini mlango wa kizazi uko vizuri
Utambuzi
- Kwa kuangalia dalili
- Kuchunguza sampuli ya uchafu wa ukeni kutumia darubini – yeast cells
- Culture
Matibabu
- Dawa za kuweka ukeni kama – Nystatine vaginal pessary AU Miconazole AU clotrmazele creams AU Keto conazole AU
- Kama unajirudiarudia kutumia dawa ya kumeza au sindano – Fluconazele
Kuzuia
- Tibu wagonjwa
- Tibu tatizo lililosababisha au kuongeza hatari ya kupata fangasi wa ukeni