Fangasi za kucha ni nini?
Fangasi za kucha ni aina ya maambukizi yanayotokea kwenye kucha za vidole vya miguu au vidole vya mikono yayosababishwa na fangasi.
Kwanini unapata fangasi za kucha?
Madaktari sio mara zote wanajua sababu za kutokea kwake. Lakini fangasi huwapata zaidi watu wenye ugonjwa wa kisukari na matatizo mengine ya kitabibu, na wazee.
Nitafanya nini kama nina fangasi za kucha?
Kuna matibabu mengi ya tatizo hili. Hakuna tiba inayofanya kazi wakati wote, ni lazima kujaribu inayokufaa wewe.
- Daktari anaweza kukupatia vidonge vya kuua fangasi. Viidonge vinafanya kazi vizuri zaidi ukilinganisha na aina nyingine za tiba. Lakini unapaswa kuvimeza kila siku kwa miezi kadhaa. Unaweza kuhitajika kufanya vipimo mara kadhaa kuangalia madhara mabaya yanayoweza kutokana na dawa.
- Kama una fangasi kwenye nusu ya ukucha, kuna rangi za kucha maalumu zinazoweza kuua fangasi.
- Kuna matibabu pia yanayotumia miali ya laiser au mianga mingine maalumu ili kuua fangasi.
Haya ni aina ya matibabu mapya na madaktari wengi hawajafahamu jinsi ya kuyatumia bado.
Unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kupunguza uwezekano wa kupata zaidi fangasi wa kucha;
- Kausha miguu kwa taulo au kwa kikausha nywele baada ya kuoga
- Vaa viatu vilivyotengenezwa kwa ngozi. Usivae viatu vilivyoundwa kwa mpira, plastiki, au bidhaa nyingine zilizoundwa viwandani
- Vaa soksi zilizotengenezwa kwa malighafi zinazonyonya na kupunguza unyevu, kama vile, manyoya ya wanyama, nylon. Usivae soksi za pamba.
- Pulizia viatu dawa au poda za kuua fangasi. Unaweza kununua aina hii ya dawa kwenye duka la dawa muhimu bila cheti cha daktari.
- Usitembee peku unapokwenda chooni au maeneo mengine yenye unyevu
- Usitumie rangi za kucha au vifaa vya kurefusha kucha, kama vile acrylic au gel za kucha. Kama unahitaji kutengenezwa kucha nenda kwenye saloon unazoziamini, au nenda na vifaa vyako mwenyewe