Ni nini maana ya figo kushindwa kufanya kazi?

Figo kushindwa kufanya kazi ni tatizo linalotokana na figo kushindwa kutekeleza majukumu yake vizuri, na kwa sababu hiyo, taka mwili zilizopaswa kutolewa nje zinabakia mwilini. Shinikizo la damu linaweza kuongezeka, na mwili unaweza kujaa maji. Kama hali ya figo kushindwa kufanya kazi itagundulika mapema, matibabu yanaweza kupunguza kasi ya uharibifu wa figo.

Ni zipi dalili za figo kushindwa kufanya kazi?

Watu wengi wenye tatizo la figo kushindwa kufanya kazi hawapati dalili mpaka ugonjwa anapokuwa mkubwa. Baadhi ya dalili za kaida ni pamoja na:

Tatizo la figo kushindwa kufanya kazi yake hakusababishi maumivu, lakini wagonjwa wanaweza kuwa na maumivu kutokana na matatizo mengine ya kitabibu waliyonayo.

Tatizo la figo kushindwa kufanya kazi linatibiwaje?

Moja ya njia inayotumika ni kusafisha damu kwa mashine (dialysis), lakini njia hii inapendekezwa pale tu figo zinapoonekana zimeshindwa kabisa kufanya kazi yake. Njia ya kusafisha damu kwa mashine haimfai kila mtu. Daktari atakusaidia kuamua kama ni njia bora kwako au la. Kupandikizwa figo mpya kutoka kwa mfadhili (kidney transplant) ni njia nyingine inayopendelewa kwa baadhi ya wagonjwa

Nini matarajio ya mgonjwa mwenye tatizo la figo kushindwa kufanya kazi?

Hali ya figo kushindwa kufanya kazi itaendelea kuwa mbaya kadri muda unavyokwenda. Daktari atahitaji kuongeza au kupunguza dozi ya dawa zako mara kwa mara. Hakikisha unamwambia daktarin dawa zote unazotumia, hii ni pamoja na dawa unazonunua mwenye we duka la dawa au dawa za kienyeji na dawa ulizoandikiwa na dakatari.

Watu wenye tatizo la figo kushindwa kufanya kazi wanaweza kuishi miaka mingi kama damu yao inachujwa kwa mashine (dialysis). Lakini wanaweza kupata matatizo yatokanao na tiba au ugonjwa mara kwa mara. Kama una ugonjwa mkali wa figo kushindwa kufanya kazi, ni vizuri kuandika wosia na kama ni muhimu chagua mtu mwenye nguvu ya maamuzi kuhusu afya yako kisheria utakapokuwa hujiwezi (power of attorney for health care).

Wosia uliouandika ukiwa na akili timamu utawasaidia madaktari kufanya maamuzi ya kitabibu sawa na matakwa yako. Kumpatia nguvu ya kisheria mtu unayemwamini ya kufanya maamuzi kuhusu afya yako hasa utakapokuwa hujiwezi ni jambo jema, hasa kama unahisi itakuwa ngumu kwa watu waliokaribu yako kufanya maamuzi ambayo ungependa yafanyike. Ni vizuri kuongea na wanafamilia na marafiki kuhusu mapendeleo yako kabla hali haijawa mbaya zaidi.

Baadhi ya watu wanaamua kuwa hawataki kuendelea kusafisha damu kwa mashine (dialysis). Watu hawa wanaweza kutunzwa na kuangaliwa hospitalini au nyumbani. Huduma ya kuwaangalia wagonjwa wa ina hii ina lengo la kuboresha maisha kadri inavyowezekana wanapouendea mwisho wa maisha yao, na huduma hii inamtegemeza mgonjwa na familia yake katika kipindi kigumu cha kuagana na mpendwa wao.

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/kidneydiseases.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *