Maelezo ya jumla

Homa (fever) ni dalili inayotajwa mara kwa mara kuelezea ongezeko la joto la mwili kuliko kiwango cha kawaida (kiwango cha kawaida  cha joto la mdomoni ni 36.8 ± 0.7 ° C au 98.2 ± 1.3 ° F). Homa ni ongezeko la muda mfupi la joto la mwili, kwa kawaida huwa karibu 1-2 ° C. Homa sio ugonjwa bali dalili ya ugonjwa.

Ukiwa na homa joto lako la mwili linakuwa limeongezeka na kuvuka kiwango cha kawaida ambacho huwa 370C. Homaa ni moja ya njia ambayo mwili huitumia kukwambia kuwa una maambukizi, na mara nyingi husababishwa na ugonjwa unaoletwa na virusi kama vile mafua au maambukizi kwenye koo, kifua au kibofu. Homa inaweza kusababishwa na magonjwa mengine pia, kuungua jua sana  au kama mjibizo mbaya unaotokana na dawa ulizotumia.

Mwanzoni unapoanza kupata homa unahisi joto, lakini kama joto la mwili litaendelea kuongezeka, basi unaweza kuanza kuhisi baridi na hata kutetemeka, na baadae joto likianza kushuka tena unahisi joto tena na hata kutokwa jasho. Unaweza kuishiwa maji mwilini kama homaa itaendelea

Mama akipima joto la mtoto kwa kutumia kipima joto

Upimaji wa joto la mwili -homa

Mgonjwa anapokuwa au anapohisiwa kuwa na homa, joto la mtu huyo hupimwa kwa kutumia kipima joto (thermometer). Kipima joto huwekwa aidha kwapani, mdomoni, sikioni au kwenye njia ya haja kubwa. Mtu anasemekana kuwa ana homa kama:

  • Joto kwenye njia ya haja kubwa (rektamu) au sikioni liko zaidi ya 38.0 ° C (100.4 ° F)
  • Joto mdomoni liko zaidi ya 37.5 ° C (99.5 ° F)
  • Joto kwapani liko zaidi ya 37.2 ° C (99.0 ° F)

Mama anaweza kumgusa mwanae na kujua kama ana joto au la. Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa mguso wa mama unaweza kugundua mpaka nusu ya kesi za homa kwa kugusa tu.

Dalili za hatari ukiwa na homa

Ni vizuri kutafuta msaada wa daktari kama

Ni vizuri kumwona daktari kama una homa na una dalili nyingine kama vile maumivu ya sikio, upele au kikohozi chenye makahozi

homaUnaweza kufanya nini wewe mwenyewe ukiwa na homa?

Unaweza kufanya mambo yafuatayo nyumbani pamoja na matibabu yoyote uliyopewa na daktari

  • Pumzika; sio lazima ubaki kitandani, ila inapaswa usijichoshe sana, ni vizuri usiende kazini
  • Tumia madawa ya kupunguza homa, madawa kama vile Acetaminophen na ibuprofen, yatapunguza homa na kukupunguzia maumivu ya kichwa au misuli. Ni vizuri kuanza kutumia hizi dawa mara tu unapoanza kuhisi homa
  • Kunywa maji angalau glass 8 au juice yenye maji mengi ili kupunguza uwezekano wa kupungukiwa na maji. Jaribu kunywa glass 1 kila saa. Ni vizuri kuepuka vinywaji vya viwandani kama vile soda. Jaribu kunywa vitu kama supu au mtori kama unajihisi hauna hamu ya kula
  • Jaribu kukaa mahala penye joto la kawaida, usikae sehemu yenye baridi sana. Vaa nguo nyepesi zisizobana. Na kama kuna joto sana , tumia feni kupunguza joto
  • Kama unataka kujua una joto kiasi gani, tumia kipima joto (digital thermometer)
  • Kama unatetemeka, usijaribu kukaka karibu na moto au kwenye jua. Ni vyema zaidi ujifunika shuka au blanket jepesi
  • Kama unahisi joto limekuzidia na unatokwa jasho, chukua kitambaa kilicholoweshwa na maji ya uvuguvugu na ujikande usoni taratibuu

homaUkiwa na homa mwone daktari kama:

Kama ukiona mambo yafuatayo ni vizuri ukamwona daktari akupatie ushauri

  • Kama homa yako inaendele kupanda, japo kuwa umejaribu kuipunguza kwa njia hzo
  • Kama joto halijapungua baada ya siku 2/ kama umeanza kupata dalili nyingine

Vyanzo

https://www.wikidoc.org/index.php/Fever

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *