Maelezo ya jumla
Ugonjwa wa homa ya bonde la ufa (Rift valley fever) ni ugonjwa mkali unosababishwa na virusi unaosababisha homa kwa wanyama wa kufugwa kama vile ng’ombe, kondoo, ngamia na wanadamu. Homa ya bonde la ufa inahusishwa na mlipuko wa mbu unaotokea baada tu ya mvua nyingi.
Ugonjwa homa ya bonde la ufa ulitambulika kwa mara ya kwanza nchini Kenya mwaka 1915, lakini kirusi anayesababisha ugonjwa huu hakutambuliwa mpaka mwaka 1931. Milipuko ya homa ya bonde la ufa inatokea mara nyingi kwenye ukanda wa chini ya jangwa la sahara. Mwaka 1977-78, ulitokea mlipuko mkubwa wa ugonjwa huu huko Misri, na watu milioni kadhaa waliambukizwa na maelfu kufa. Kenya mwaka 1998, ugonjwa huu ulisababisha vifo vya wakenya 400. Mwaka 2000 mlipuko ulitambuliwa nchini Saudi Arabia na Yemen.
Sababu ya ugonjwa wa homa ya bonde la ufa ni?
Homa ya bonde la ufa inasababishwa na virusi “rift valley virus”. Wanadamu kwa kawaida wanaambukizwa virusi hawa kwa kung’atwa na mbu wenye maambukizi na
Wanadamu wanaweza pia kupata ugonjwa huu kama watagusa damu, majimaji ya mwili, au tishu za mnyama aliyeambukizwa. Kugusana moja kwa moja na wanayama kunatokea wakati wa kuchinja mnyama au wakati wa kumtibu au wakati wa kumsaidia kujifungua. Maambukizi kupitia hewa yamewahi kutokea kwenye mazingira ya maabara.
Homa ya bonde la ufa inapatikana zaidi katika sehemu za mashariki na kusini mwa afrika ambapo kondoo na ng’ombe wanafugwa.
Mambo yanayoongeza hatari ya kupata ugonjwa wa homa ya bonde la ufa?
Tafiti nyingi zimeonesha kuwa, kulala nje katika maeneo yenye mlipuko kunaongeza uwezekano wa kuumwa na mbu na wadudu wengine wenye maambukizi. Wachungaji wa wanayama na waangalizi wa mifugo wako kwenye hatari kubwa kama wanaishi kwenye maeneo yenye ugonjwa huu.
Watu wanaofanya kazi zinazoongeza uwezekano wa kupata ugonjwa kama vile wataalamu wa mifugo na watu wanaochinja mifugo, wana uwezekano mkubwa wa kuambukizwa kutoka kwa mnyama mwenye maambukizi.
Wasafiri wa kimataifa wanakuwa katika hatari ya kuambukizwa kama watatembelea maeneo yenye mlipuko wa homa ya bonde la ufa.
Hali ya ugonjwa wa homa ya bonde la ufa, matatizo na matarajio
Kwa kawaida mgonjwa anapona ndani ya siku 2-7 baada ya maambukizi. Karibia 1% ya watu wote wanaoambukizwa homa ya bonde la ufa wanakufa kutokana na ugonjwa.
Wanyama wanakufa zaidi. Wanyama wenye mimba wanapata matatizo zaidi, karibia 100% ya Wanyama wenye mimba, ujauzito utatoka wakipata maambukizi haya.
Moja ya tatizo linalowapata watu wengi wanaopata maambukizi ya homa ya bonde la ufa ni kuharibiwa kwa retina – hii ni sehemu ya jicho inayounganisha mishipa ya fahamu inayotoka kwenye jicho kwenda kwenye ubongo. Kama sehemu hii itaharibiwa, karibia 1% – 10% ya watu wote waliogua watapata maatatizo ya kudumu ya kuona / kupungua kwa uwezo wa kuona/ upofu.
Utambuzi wa ugonjwa wa homa ya bonde la ufa
Kwa wanadamu walioambukizwa homa ya bonde la ufa wanaweza kuwa na dalili zenye ukali tofauti tofauti. Wengi wa wagonjwa wanaweza wasiwe na dalili kabisa au wanaweza kuwa na dalili za kadri kama vile homa, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli na matatizo ya ini.
Kwa watu wachache (< 2%), ugonjwa unaweza kuendelea na kusababisha wakaanza kuvuja damu na kusababisha kuvimba kwa utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo, au kuathiri macho.
Mgonjwa anayejihisi kuumwa kwa kawaida anahisi homa, uchovu, maumivu ya mgongo, kizunguzungu, na kupungua kwa uzito wa mwili baada ya ugonjwa kuanza. Kwa kawaida tunategemea wapone ndani ya siku 2-7.
Matibabu ya ugonjwa wa homa ya bonde la ufa
Hakuna matibabu kwa ajili ya homa ya bonde la ufa. Kumekuwepo na majaribio ya kutumia dawa ya kudhibiti virusi inayoitwa ribavirin – hii imeonesha mafanikio makubwa katika tafiti zilizohusisha nyani na wanyama wengine.
Tafiti pia zinaonesha dawa aina ya interferon na immune modulators zinaweza kusaidia kutibu wagonjwa wa homa hii.
Madaktari hutibu ugonjwa huu, kwa kudhibiti dalili ulizonazo, na kuruhusu kinga ya mwili wako kupambana na virusi.
Kuzuia ugonjwa wa homa ya bonde la ufa
Uwezekano wa kuambukizwa homa ya bonde la ufa unaweza kupunguzwa kwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na mbu na wadudu wengine wanyonyao damu kwa;
- Kutumia dawa za kufukuza wadudu (repellants)
- kulala chini ya chandarua.
- Vaa nguo za mikono mirefu, suruari ndefu, na kofia ili kujikinga unapokuwa maeneo yenye kupe, mbung’o, vaa viatu vinavyofunika
- Jikague mwili na nguo kama kuna kupe au viroboto
Epuka kukutana na damu au tishu za wanyama walioambukizwa, hasa kama unafanya kazi na wanyama katika eneo lenye mlipuko wa homa ya bonde la ufa