Maelezo ya jumla

Damu huwa inavilia chini ya ngozi inayozunguka jicho kama umepata jeraha la jicho baada ya kupigwa na kitu, kama vile ngumi moja kwa moja kwenye jicho. Kwa sababu damu imevilia chini ya ngozi, eneo linalozunguka jicho linaoneka jeusi kuliko kawaida ‘’black eye’’ kwa sababu eneo hili ni rahisi kuumia. Mara nyingi utakuta eneo lililopata jeraha linaanza kuvimba, kuuma na hata damu kuvujia ndani au chini ya ngozi muda mfupi tu baada ya jeraha. Baadae, kope na eneo linalozunguka linabadilika rangi na kuwa la bluu na baadae weusi, taratibu rangi nyeusi inafifia kuelekea kwenye rangi ya zambarau, baadae manjano jeraha linapoanza kupona. Mara nyingi weusi huu kwenye jicho huwa unaondoka baada ya siku 10-14.

Kama una jeraha la jicho baada ya kupigwa mwone daktari haraka kama

kama una jeraha la jicho baada ya kupigwa, ni vizuri kumwona daktari kama

  • Kama unashindwa kuona vizuri au unaona maluweluwe au unaona vitu viwiliviwili
  • Kama jicho au ukope wako umeumia
  • Kama umepoteza fahamu, hata kwa muda mfupi
  • Kama haujui uliumiaje jicho au kama una wasiwasi wowote kuhusu hali yako

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kama una jeraha la jicho baada ya kupigwa

Kama umepata jeraha la jicho baada ya kupigwa na tukio ni dogo tu, unaweza kuanza kutumia njia hizi mapema iwezekanavyo ukiwa nyumbani ili kupunguza uwezekano wa damu kuvia na kupunguza karaha

  • Unaweza kuweka barafu kwenye eneo lililoumia ili kupunguza uvimbe na kuvuja damu
    • Weka kitu chochote chenye ubaridi mapema iwezekanavyo ili kupunguza uvimbe na kuvuja damu chini ya ngozi
    • Unaweza kuchukua barafu ukaiweka kwenye kitambaa kisha ukaweka kwenye eneo lililoumia au unaweza kuchukua kitambaa ukakiloweka kwenye maji ya baridi, kikamue kisha ukiweka kwenye jicho au unaweza kuchukua kopo la kinywaji baridi ukaweka kwenye eneo lililoumia

jeraha la jicho

    • Unaweza kushikilia kitambaa hicho cha baridi kwenye eneo hilo kwa dakika 10-15 bila kukandamiza
    • Unaweza kurudia utaratibu huu mara 8 hivi kwa masaa 24 mapaka 48 ya mwanzo baada ya kuumia
  • Tumia mto utakapokuwa umelala usiku, ni vizuri kichwa chako kiwe juu kuliko mwili wako ili kupunguza uvimbe
  • Kama ni muhimu (kama unazihitaji) tumia dawa za maumivu ili kupunguza maumivu. Madawa kama ”acetaminophen” au ”ibuprofen” yanapunguza uvimbe na kupunguza karaha. EPUKA kutumia ”ASPRIN” kwa sababu inaweza kusababisha kuvuja damu kuongezeka
  • Epuka kupuliza pua zako kwa nguvu, kwa sababu ukifanya hivi inaongeza mzunguko wa damu kwenda usoni na inaweza kusababisha uvimbe kuzunguka jicho kuongezeka

Kama una jeraha la jicho baada ya kupigwa tafuta ushauri wa daktari kama

Ni vizuri kumwona daktari kama:

  • Kama unaona weusi haujaanza kupungua baada ya siku kadhaa, kama unaona panaanza kuwa pa-moto au kama panaanza kuvimba au kutengeneza usaha
  • Kama unaona kuna mabadiliko kwenye uwezo wako wa kuona
  • Kama una maumivu yasiyoisha au maumivu ya kichwa

Vyanzo

https://medlineplus.gov/eyeinjuries.html

Shares:
5 Comments
  • Kama weusi na wekundu hujaweza kuisha tutumie njia gani kuisha
    Kama weusi na wekundu hujaweza kuisha tutumie njia gani kuisha
    April 5, 2021 at 6:15 pm

    Kama weusi na wekundu hujaweza kuisha tutumie njia gani kuisha

    Reply
    • Dr.Mniko
      Dr.Mniko
      April 5, 2021 at 7:05 pm

      Kama umetumia barafu na uvimbe umepungua na hauna maumivu ya kichwa
      Kuwa na uvimilivu , baada ya muda utaisha, ipe muda

      Reply
  • Sam
    Sam
    February 15, 2022 at 6:30 am

    Kama maumivu ya kichw hayapo ila ukiona mwanga mkali jicho linauma unafanyaje?? Na maumivu yameanza masaa 42 baada ya jicho kuumia kwa kupgwa

    Reply
  • Martha Stanley
    Martha Stanley
    October 9, 2022 at 2:35 pm

    Iv jicho likivilia damu likawa jekundu,baadae linaweza kuwa sawaa?

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      November 4, 2022 at 6:09 pm

      ndio ndio, baada ya wiki 1-3 linakaa sawa

      Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *