Jicho jekundu ni nini?

Jicho jekundu ni hali inayotokana na kuvimba kwa utando mwepesi unaofunika jicho na sehemu ya ndani ya kope. Jicho jekundu ni hali inayotambulika pia kama konjaktivaitisi. Kwa kawaida hali hii inasababishwa na maambukizi ya kawaida. Visa vingi vya Jicho jekundu vinasababishwa na virusi, lakini pia yanaweza kusababishwa na vimelea wengine (kama vile bakteria, au fangasi) au kizio (kama vile chamvua au vumbi).

Ni zipi dalili za Jicho jekundu?

Dalili zifuatazo ndizo zinazowapata zaidi watu wenye Jicho jekundu:

  • Wekundu na kuhisi kama macho yanaungua
  • Kutokwa na majimaji au uchafu wa njano unaosababisha kope kugandiana pamoja, hasa wakati wa kuamka
  • Uoni hafifu / kushindwa kuona vizuri au kuumizwa na mwanga
  • Kuvimba kwa kope
  • Maumivu kuzunguka macho

Unapaswa kumwona daktari kama dalili zitadumu kwa zaidi ya siku tatu au zaidi.

Jicho jekundu yanatibiwa vipi?

Matibabu yanategemea sababu. Jicho jekundu lililosababishwa na virusi linapona jenyewe ndani ya wiki moja hata kama usipopata matibabu. Jicho jekundu lililosababishwa na bakteria linaweza kupona jenyewe bila matibabu, lakini daktari anaweza pia kukuandikia dawa ya kuweka kwenye macho kama una hali kali sana.

Kama inasababishwa na kizio /aleji, unapaswa kukaa mbali na vitu vinavyosababisha dalili kuwa mbaya zaidi. Daktari anaweza kupendekeza utumie dawa ya kuweka kwenye macho ili kuyapooza na kupunguza kuwashwa.

Je, ugonjwa wa Jicho jekundu unaambukizwa?

Ugonjwa wa Jicho jekundu unaosababishwa na mzio hauambukizwi, lakini ugonjwa wa Jicho jekundu unaosababishwa na vimelea unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine. Unaweza kuambukizwa kwa kugusana moja kwa moja na mtu mwenye ugonjwa.

Kwa mfano, unaweza kuupata kwa kufikicha macho kwa vidole vya mikono vilivyokuwa na vimelea, kwa kukohoa au kupiga chafya, au kwa kuogelea katika bwawa moja na mtu mwenye Jicho jekundu. Unaweza pia kuupata kwa kuchangia vitu binafsi kama vile taulo au vipodozi

Nifanye nini nisisambaze ugonjwa huu?

Ni muhimu kuwa unawe mikono vizuri na utumie karatasi za tishu kujifutia. Usichangie vitu binafsi. Kama una Jicho jekundu au kama yanatoa uchafu, usivae lenzi za macho “contact lens”. Hauna haja ya kukaa mbali na watu wengine, ila inaweza kuwa vizuri kuwazuia watoto wasiende shuleni kama macho yao ni mekundu ya yamesababishwa na vimelea.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/pinkeye.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *