Jinsi ya kukadiria kiasi cha mlo kwa kutumia mikono yako
Mikono yako inaweza kutumika kukadiria kiasi cha chakula unachotakiwa kula kwa mlo mmoja. Ufuatao ni muongozo wa kukadiria kiasi cha mlo kwa kutumia mikono kama kipimo:
- Vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi kama vile ugali, wali, viazi: Kiasi sawa na ukubwa wa ngumi moja
- Matunda: Kiasi cha matunda ni sawa na ngumi moja; mfano saizi ya kati ya chungwa, embe, kipande cha papai, tikiti-maji, au nanasi.
- Mboga-mboga: Kiasi cha mbogamboga kiwe kingi zaidi, kadiria kiasi cha kuweza kujaa katika viganja vya mikono yote miwili. Pendelea kula zaidi mboga mboga ambazo hazina kabohaidreti kama mchicha, kabichi lettuce. Mboga zenye kabohaidreti ni kama
- Vyakula vya jamii ya kunde na vile vyenye asili ya wanyama: Kiasi sawa na ukubwa wa kiganja cha mkono wako na unene uwe sawa na wa kidole kidogo cha mkono wako
- Mafuta: Ncha ya kidole gumba. Endapo unapendelea kunywa maziwa wakati wa mlo, hakikisha unakunywa maziwa yaliopunguzwa mafuta (low fat), kiasi kisizidi millilita 250