Maelezo ya jumla
Jipu (abscess) ni mkusanyiko wa usaha katika sehemu yoyote ya mwili, ambayo mara nyingi huisababisha ivimbe.
Je! Ni nini dalili za jipu?
Dalili hutegemea hasa mahali lilipo. Dalili za kawaida ni kama zifuatazo:
- Maumivu kwenye eneo
- Kuhisi baridi
- Homa
- Kupungua kwa uwezo wa kufanya kazi katika eneo lililoathirika
- Kujisikia vibaya, wasiwasi, au hisia mbaya
- Kichwa kuuma
- Kuvimba katika eneo na tishu za eneo hilo hukakamaa
- Kupoteza hamu ya kula
- Kupoteza hisia katika eneo lililoathirika
- Kichefuchefu na kutapika
- Kuvimba
Jipu husababishwa na nini?
Majipu hutokea wakati tishu za eneo la fulani la mwili zinapopata maambukizi na mfumo wa kinga ya mwili ukijaribu kupigana nayo. Seli nyeupe za damu hutambaa katika kuta za mishipa ya damu mpaka katika eneo la maambukizi na kujikusanya ndani ya tishu zilizoharibiwa. Wakati wa mchakato huu, usaha hutengenezeka. Usaha ni mkusanyiko wa ugiligili (fluid), seli nyeupe za damu zilizo hai na zilizo kufa, tishu zilizokufa na bakteria au vitu vingine vigeni. Majipu yanaweza kutokea mahali popote mwilini. Kweye ngozi,ndani ya ngozi na kwenye meno ndio maeneo yanayoathirika kwa zaidi. Majipu yanaweza kusababishwa na bakteria,kimelea na kitu kigeni ndani ya mwili. Majipu ya kwenye ngozi ni rahisi kuonekana. Ni mekundu, yanavimba na yanauma. Majipu katika maeneo mengine ya mwili inaweza isiwe rahisi kuyaona, lakini yanaweza kusababisha uharibifu mkubwa. Zifuatazo ni aina maalumu za majipu:
- Jipu la
- Tumbo (Abdominal abscess)
- Ini linalosababishwa na Amoeba
- Njia ya haja kubwa (Anorectal abscess)
- Ubongo (Brain abscess)
- Tezi ya bartholin (Bartholin’s abscess)
- Tukwa (Peritonsillar abscess)
- Ngozi (Skin abscess)
- Uti wa mgongo (Spinal cord abscess)
- Jino (Tooth abscess)
Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata majipu?
Watu walio na historia ya maambukizi ya hivi karibuni, wako kwenye hatari kubwa ya kupata jipu.
Wakati gani utafutae matibabu ya haraka ya jipu?
Mwone mtoa huduma ya afya ikiwa unafikiri una aina yoyote ya majipu.
Utambuzi wa majipu
Mara nyingi, sampuli ya maji maji itachukuliwa kutoka kwenye jipu na kupimwa ili kuona ni aina gani ya kimelea imesababisha tatizo.
Uchaguzi wa matibabu
Matibabu yanatofautiana, lakini mara nyingi upasuaji mdogo unahitajika kuondoa usaha na baadae antibiotiki.
Nini cha kutarajia ?
Matarajio hutegemea eneo la maambukizi, aina ya vimelea vinavyosababisha jipu na hali ya kiafya ya mgonjwa (umri, hali ya kingamwili na kama ana ugonjwa wowote wa kudumu). Lakini mara nyingi majipu hupona baada ya upasuaji mdogo na kozi ya antibiotics
Matatizo yanayoweza kutokea
Jipu linaweza kupasuka na kuenea mwili mzima kupitia damu (septicemia), hii inaweza kuwa hatari