Maelezo ya jumla

Jipu la ini (liver abscess) ni eneo kwenye ini lililojaa usaha.

Je! Nini dalili za jipu la ini?    

  • Maumivu ya kifua ( hasa sehemu ya chini-kulia)    
  • Kinyesi chenye rangi ya udongo mfinyanzi
  • Mkojo wenye rangi nzito  
  • Homa, kuhisi baridi    
  • Kupoteza hamu ya kula    
  • Kichefuchefu, kutapika    
  • Kwa kawaida mgonjwa huwa na maumivu ya tumbo kwenye sehemu ya juu –kulia au kwa mara chache maumivu yanaweza kuenea katika tumbo lote    
  • Kupungua kwa uzito bila sababu maalumu   
  • Uchovu   
  • Ngozi kubadilika kuwa rangi ya manjano -manjano

Ni nini husababisha jipu la ini?

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha jipu kwenye ini, ni pamoja na:    

  • Maambukizi kwenye tumbo kama vile ugonjwa wa kidole tumbo/kibole au kutoboka kwa utumbo
  • Maambukizi kwenye damu    
  • Maambukizi kwenye mirija inayotoa nyongo kwenye mfuko wa nyongo    
  • Kipimo cha ”endoscopy” kilichofanyika hivi karibuni ili kuchunguza mirija inayotoa nyongo kwenye mfuko wa nyongo. Kipimo hiki kinaweza kubeba na kuingiza ndani maambukizi ambayo yanaweza kusambaa.
  • Jeraha kwenye ini

Bakteria wanaosababisha majipu kwenye ini ni pamoja na:    

  • ”Bacteroides”    
  • ”Enterococcus”    
  • ”Escherichia coli”    
  • ”Klebsiella pneumoniae ”   
  • ”Staphylococcus aureus  ”  
  • ”Streptococcus”

Mara nyingi, zaidi ya aina moja ya bakteria husababisha kutokea kwa jipu kwenye ini.

Utambuzi wa jipu la ini

Vipimo vinaweza kujumuisha:    

  • ”CT scan” ya tumbo –hiki ni kipimo kinachotumia nguvu ya mionzi kupiga picha sehemu ya ndani ya tumbo, ili kumpa daktari nafasi ya kuchunguza bila kufanya upasuaji.
  • ”Ultrasound” ya tumbo –hiki ni kipimo kinachotumia mawimbi ya sauti kupiga picha sehemu ya ndani ya tumbo.   
  • Kipimo cha kuangalia kiwango ”bilirubin” kwenye damu – kipimo hiki huonesha kama ini linafanya kazi yake vyema ya kuondoa ”bilirubin” mwilini.
  • ”Blood cultur”e – damu ya mgonjwa hupandwa katika mazingira yatakayoruhusu bakteria walio kwenye damu kukua ili watambuliwe kwa urahisi.
  • ”Complete blood count” – kipimo hiki huhesabu seli zote kwenye damu, aina fulani za seli huongezeka kama kuna maambukizi mwilini
  • ”Liver biopsy”- Upasuaji/utaratibu mdogo hufanyika ili kuchukua sampuli ya nyama kidogo kwenye ini ili kupima
  • ”Liver function tests”- Kipimo hiki hufanyika ili kugundua kama ini linafanya kazi yake vyema (vipimo vya kazi ya ini)

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone mtoa huduma wa afya ikiwa una:    

Uchaguzi wa matibabu

Matibabu ya kawaida hujumuisha kuweka mrija kupitia kwenye ngozi ili kunyonya usaha kutoka kwenye jipu. Kwa mara chache sana upasuaji huhitajika. Utapewa dawa aina ya antibiotiki kwa wiki 4 hadi 6. Wakati mwingine, antibiotiki pekee zinaweza kutibu na kuondoa kabisa maambukizi kama ni kidogo.

Kuzuia

Matibabu ya haraka ya maambukizi ya tumbo na maambukizi mengine yanaweza kupunguza hatari ya kutokea kwa jipu la ini. Matukio mengi hayawezi kuzuilika.

Nini cha kutarajia?

Kwa baadhi ya wagonjwa, hali hii inaweza kuhatarisha maisha.  Hatari ya kupoteza maisha ni kubwa zaidi kwa watu ambao wana majipu mengi kwenye ini.

Matatizo yanayoweza kujitokeza

Maambukizi yanaweza kusambaa mwili mzima na kutishia maisha 

Vyanzo    

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000261.htm

 

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *