Maelezo ya jumla
Kichomi ni maumivu ya kifua yanayotokea hasa wakati wa kuvuta pumzi ndani au kukohoa, maumivu haya husababishwa na kuvimba kwa utando mdogo (pleural) unaofunika kifua na mapafu.
Je! Nini dalili za kichomi?
Dalili kuu ya kichomi ni maumivu kifuani. Mara nyingi maumivu hutokea unapovuta pumzi ndani au kukohoa. Watu wengine wanaweza kuhisi maumivu kwenye bega. Kuvuta pumzi ndani, kukohoa na mjongeo wowote wa kifua hufanya maumivu kuwa mabaya zaidi.
Kuvimba kwa utando unafunika mapafu kunaweza kusababisha maji kujikusanya ndani ya kifua. Hii inaweza kusababisha kupumua kwa shida na kusababisha dalili zifuatazo:
- Ngozi kubadilika na kuwa ya bluu kwa sababu ya kukosa oksijeni ya kutosha kwenye damu
- Kukohoa
- Kupumua kwa shida
- Kupumua haraka haraka
Kichomi husababishwa na nini?
Kichomi hutokea mapafu yanapovimba kwa sababu ya maambukizi kama nimonia au kifua kikuu. Mara nyingi tatizo hili ni ishara ya kuwepo maambukizi ya virusi kwenye mapafu.
Pia, maumivu ya kichomi yanaweza kusababishwa na:
- Magonjwa yanayosababishwa na asibesiti (asbestos)
- Saratani fulani
- Jeraha / kuumia kifuani
- Magonjwa ya yabisi-baridi (Rheumatic diseases)
Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata kichomi?
Ikiwa una ugonjwa wa mapafu, kama vile nyumonia au kifua kikuu, uko katika hatari kubwa ya kupata kichomi.
Wakati gani utafute matibabu ya haraka?
Mwone mtoa huduma wa afya ikiwa una dalili za kichomi. Kama unapata shida kupumua au ngozi yako inageuka bluu, tafuta huduma ya matibabu haraka sana.
Utambuzi wa kichomi
Unapokuwa na kichomi, utando laini unaofunika mapafu na kifua unakuwa mgumu na unaoparura. Tando hizi mbili husuguana kila unapovuta pumzi na inaweza kutoa sauti ya mpapruro anayoweza kuisikia daktari kwa kutumia kifaa cha kusikiliza kifua.
Mtoa huduma ya afya anaweza kufanya vipimo vifuatavyo:
- Complete blood count – kipimo hiki hufanyika ili kutambua kama kuna maambukizi kwenye damu,
- Thoracentesis – kipimo hiki hufanyika ili kupunguza maji kifuani au kwa ajili ya kuyapima ,hili hufanyika kwa kuchoma sindano ndefu kwenye kifua ili kupunguza maji hayo
- Ultrasound ya kifua – kipimo hiki hutumia nguvu ya mawimbi ya sauti kupiga picha ya kifua
- Eksirei ya kifua – picha ya eksirei husaidia kutambua sababu ya tatizo hili.
Uchaguzi wa matibabu ya kichomi
- Mtoa huduma wa afya anaweza kuondoa maji kwenye mapafu kwa thoracentesis na kuyachunguza kuangalia kama kuna ishara za maambukizi.
- Matibabu yanategemea kinachosababisha kichomi. Maambukizi ya bakteria yanatibiwa kwa antibiotiki . Maambukizi mengine ya bakteria yanaweza kuhitaji upasuaji ili kutoa maji yote yenye uambukizo.
- Kichomi kinachosababishwa na maambukizi ya virusi kwa kawaida hupona tu chenyewe bila bila dawa. Wagonjwa mara nyingi wanaweza kudhibiti maumivu kwa dawa za maumivu kama vile paracetamol au ibuprofen.
Nini cha kutarajia unapokuwa na kichomi?
Matarajio ya kupona tatizo hili hutegemea limesababishwa na nini.
Matatizo yanayoweza kutokea ukiwa na kichomi
- Kupata shida kupumua
- Kuharibika kwa mapafu kwa sababu ya jeraha baada ya thoracentesis
- Matatizo yanayotokana na ugonjwa uliosababisha kichomi
Kuzuia kichomi
Kutibu mapema maambukizi ya bakteria kwenye njia ya hewa itasaidia kuzuia kichomi.
Nimeelewa mm huwa napata kichomi hasa upande wa kulia kifuani kwa na huwa nakipata nikianza kufanya movement zangu baada ya kuamka .Ninapopata hata mkono kuunyenyua huwa nitabu .Je kujipepea na feni mda mrefu kunaweza sababisha kichomi.asnte
FAN INASABABISHA KICHOMI?
Asante kwa swali lako
Kuna faida na harasa kadhaa za kulala chini ya fan usiku, LAKINI kwa ujumla hakuna madhara ya kudumu yanauoweza kusababishwa na kulala chini ya fana
FAIDA ZA KULALA CHINI YA FAN
》Kwa baadhi ya watu upepo mwanana unaotoka kwenye fan unawafanya wapate usingizi mapema , kwa hiyo kupumzika vizuri
》 Kupunguza joto ndani ya nyumba ni faida ingine ,hii inasababisha usingizi mzuri pia
》 kuna baadhi ya watu, kelele nyepesi zinazosababishwa na fan zinasababisha wanapata usingizi mzuri
HASARA
》 Kwa baadhi ya watu wakilala chini ya fan wanapata shida,shida zenyewe mara nyingi ni ndogo tu lakini zinaweza kukera
■Baadhi wanaamka wakiwa wamechoka sana
■Kwa sababu ya upepo, unasababisha pua na midomo kukauka sana, kwa sababu hyo mtu anaamka akiwa kama ana mafua na kunakuwa na mwasho kooni, anakuwa anakohoa kidogo ili kuliweka sawa koo
■Kwa sababu ya upepo , unaweza kupuliza vumbi iliyo ndani ya nyumba ikasababisha matatizo kwa watu walio na mzio au allergy ya vumbi
Kwa hiyo kama unavyoona kuna faida na hasara za kutumia fan, na sio kila mtu anapata dalili zilizo sawa, kwa sababu tunatofautiana
Siwezi kusema kuwa fan inakusababishia kichomo na siwezi kukataa pia kuwa haisababisho, kwa sababu inawezeka ikawa
Ninakushauri, kama unadhani fan ndio inasababisha kichomi,acha kuitumia kwa siku kadhaa ili uangalie , kama kisipo poa mwone daktari akusaidie kutafuta sababu
Asante, endelea kuwa nasi
Nikipata tatizo la kichomi upande wakulia kwenye titi nilimeenda ospitali wakasema nina nimonia nikapewa dawa na sindano klistapeni nimamaliza ila maumivu yanaondoka mda kidogo yanaludi pia natokwa jasho jingo nikilala maeneo ya kifuani kizunguzungu na mara nyingi nakuwa naogopa bila sabàbu naombeni ushauri
Asante kwa kutuelimisha..ila m pia natatizo la kichomi ila kinanshika nkiwa nakimbia tena vitatu pembeni ya diaphragm,katikati na kwenye pega moja la kushoto..nshawahi kuumwa neumonia apo nyuma ya joto,saiv kichwa kinaniuma kwa mbele na naskia mwili kama unakosa nguvu iv sa sijui inaeza ikawa neumonia imerud au laaa…ila mafua sina wala kikohozi
yeah. ata mm hiyo hali inanipata sasa sjajua n nn. til now naumwa sana kifua upande w kushoto na nyuma ya bega. na katikati y kifua kunakuwa na kichomi.
pole sana
Hata m leo cku nzima kmeniuma, upande wa kushoto Kwenye diaphragm, sasa cjui kmesababisha na nn, coz cjawai umwa before. Nikivuta pumzi inauma
Mimi nimeelewa ila mi huwa napatwa na kichomi upande wa kushoto mbavuni karibu na kwapa ni nini kinachoweza kusababisha?????
pole sana
Mimi huwa nahisi maumivu upande wa kushoto wa moyo mara nyingine inapanda mpaka mkono wa kushoto na shingoni.nifanyaje mkuu
Itakuwa vigumu kujibu swali hili bia kupata taarifa za nyongeza, ila kama una wasiwasi mwone dakatari atakushauri vizuri zaidi. Kwa uzoefu tu: Watu wengi huhisi maumivu ya kushtua karibu na moyo na huwa ni kwa sababu hawafanyi mazoezi, kushughulisha mwili kunasaidia kukuweka sawa zaidi.
Mimi huwa inanipata kwenye kichomi kabisa asubuhi asubuhi nikiamka Kama vile na njaa sana
pole sana
Mm na pata kichomi kwenye mbavu zangu za kulia Yan ni maumivu usiku silali ni tumie dawa gani
Kichumi ni dalili ya ugonjwa wa kifua, inaweza kuwa nyumonia, kifua kikuu, mafua n.k., kwa hiyo huwa ni vyema kutambua sababu yake. ila kwa watu wengi kichomi ni hali ambayo hutokea bila sababu kubwa, wengi inatokea kwa sababu ya hali ya hewa na mafua. kama una kichomi unaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu kama vile paracetamol au ibuprofen. kama maumivu hayatapoa au kama bado una wasiwasi ni vizuri kumwona daktari
Dor ni miaka kumi kuna sehemu moja upande wa kushoto chini ya bega napata maumivu kama vile pana donda silali kabisa wakati mwingine vichomi vina sambaa mgongon na kifuani na kila hosptali et hawaoni ugonjwa napewa ampic napta nufuu siku 2 nabanywa tena naomba msaada please
Pole sana
Wasialiana nasi kwenye namba zetu hapo, nahitaji maelezo zaidi ili kukushauri
Pole sana
Mimi napata maumivu makali upande wa kushoto mwa kifua je ni ugojwa Gani?
Lakin pia nyumonia inasababiswa na Nini Mana nilipiga x-ray nikaambiwa Nina nyumonia nitumie dawa Gani?
Wasiliana nasi kwenye namba zetu, tutakusaidia baada ya maswali kadhaa
Pole sana
Namba zenu pls.
Nikipata tatizo la kichomi upande wakulia kwenye titi nilimeenda ospitali wakasema nina nimonia nikapewa dawa na sindano klistapeni nimamaliza ila maumivu yanaondoka mda kidogo yanaludi pia natokwa jasho jingo nikilala maeneo ya kifuani kizunguzungu na mara nyingi nakuwa naogopa bila sabàbu naombeni ushauri
Pole sana, kwa dalili ulizonazo, nadhani ni vzr ukanonana na daktari akufanyie uchunguz ili kufahamu sababu ya kichomi chako
Kichomi kina sababu nyingi, nimonia, kifua kikuu, kansa, mafua tu ya kawaida, jeraha kifuani, wakati mwingine kichomi hutokea bila sababu ya msingi
Ni vzr kujua sababu, mwone daktari ili kuoata matibabu sahihi
Nikipata tatizo la kichomi upande wakulia kwenye titi nilimeenda ospitali wakasema nina nimonia nikapewa dawa na sindano klistapeni nimamaliza ila maumivu yanaondoka mda kidogo yanaludi pia natokwa jasho jingo nikilala maeneo ya kifuani kizunguzungu na mara nyingi nakuwa naogopa bila sabàbu naombeni ushauri
Pole sana, kwa dalili ulizonazo, nadhani ni vzr ukanonana na daktari akufanyie uchunguz ili kufahamu sababu ya kichomi chako
Kichomi kina sababu nyingi, nimonia, kifua kikuu, kansa, mafua tu ya kawaida, jeraha kifuani, wakati mwingine kichomi hutokea bila sababu ya msingi
Ni vzr kujua sababu, mwone daktari ili kuoata matibabu sahihi
Hata mimi nikipata na ugonjwa huo nikipata tuba ila bado unaniludia mara kwa mara
Pole sana, kichomi ni tatizo linaloweza kujirudia kwa mtu yoyote, wakati mwingin3 inaweza kuwa hali ya kawaida
Au inaweza kuwa kwa sababu,.sababu au chanzo cha tatizo hili hakijaondolewa/kutibiwa/kushighulikiwa
Kama unaoata kichomi mara kwa marA, ni vzr kumwona.daktari atafute sababu upate tiba kamili
ninaskia kichomi upande wa kulia chini ya mbavu zangu,nikipumua ndani naumia sana.iyo inaweza kuwa ni dalili ya nyumonia ama
Ndio kichomi ni moja ya dalili za nimonia ila si wakati wote
Wakati mwingine kichomi kinaweza kuwepo tu bila sababu ya msingi, na kinaisha tu chenywewe
Kama hauna dalili nyingine na kichomi sio kikali sana na halijirudiii rudii hauna sababu ya kuogopa
Meza dawa za maumivu kama paracetamol au ibuprofen kisha subiri maumivu yatakwisha
Kama yataendelea mwone dkt
Docta mm natoa makohozi meupe,hapa kwenye koromeo panakua kama pana kizuizi furani na kunipa maumivu ya wastani pia huwa napata maumiv kwenye chembe ya moyo na maumivu kwenye Bega la kushoto hiyo nayo ni nn doctor naomba msaada wako naomba nipe hata namba nikupigie
07590789760