Maelezo ya jumla
Kikope (stye) ni uvimbe mwekundu unakuwa juu au ndani ya ukingo wa kope ya jicho lako, uvimbe huu unaouma huwa unaaanza kuvimba na kuongezeka ukubwa ndani ya siku kadhaa. Uvimbe huu huwa unatokana na maambukizi ambayo huwa yameanzia kwenye shina la unywele wa kope (eyelash). Inaweza ikawa ngumu kufungua jicho au unaweza kuanza kujihisi kama kuna kitu ndani ya jicho, hasa unapo fumba na kufungua jicho. Jicho lako linaweza kuwa linatoa machozi na mwanga unaweza kuwa unakuumiza ukiuangalia. Kikope huwa kinakua na baadae kinapasuka, kinapopasuka maumivu huanza kupungua, japo kuna baadhi ya vikope huwa vinaisha tu vyenyewe hata kabla ya kupasuka.
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe ukiwa na kikope
Vikope huwa mara nyingi kina pona chenyewe ndani ya siku chache. Lakini ukifuata hatua zifuatazo itasaidia kupunguza maumivu na kuounguza uwezekano wa kusambaza maambukizi
- Usikifikiche au kusugua jicho au kuminya Vikope ili kutoa usaha uliomo. Unaweza kuweka kitambaa kilichochovywa kwenye maji ya moto ili kiive mapema.
- Chukua kitambaa kisafi kiloweke kwenye maji ya uvuguvugu, ambayo hayaunguzi kiganja cha mkono wako, kikamue kisha kiweke kwenye kope.
- Unaweza kurudia mara nyingi kadri inavyowezekana kwa angalau dakika 10-15, ukikipasha kitambaa kila kinapopungua joto.
- Unaweza kurudia mara kadhaa kwa siku mpaka kikope kitakapopasuka
- Baada ya kikope kupasuka, osha kope zako kwa maji ya uvuguvugu na kisha pakaushe
- Nawa mikono yako vizuri mara kwa mara na epuka kushika shika jicho lako kadri unavyoweza
- Usipake vipodozi kwenye jicho lililoathirika
- Kama unatumia Contact lens usiziweke wakati unapokuwa na kikope
Ukiwa na kikope mwone daktari kama:
Panga kumwona daktari kama:
- Kama kikope hakijapona chenyewe au hata baada ya matibabu ndani ya wiki moja
- Kama kikope kinaanza kusambaa na kuanza kuhusisha ngozi inayozunguka ya kope
- Kama unapata vikope mara kwa mara
Jinsi ya kuzia kikope:
Kama unapata vikope mara kwa mara unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kuzuia
- Nawa mikono yako mara kwa mara na epuka kushika macho yako mara kwa mara. Jitahidi kila mara utumie dodoki lako mwenyewe wakati wa kuogea na taulo
- Kama una vipodozi vya zamani ni vizuri ukavitupa, hasa vipodozi vya kimiminika kama Mascara. Ni vizuri usichangie vipodozi na watu wengine. Ondoa au osha vipodozi vyote ulivyopaka kabla ya kulala
- Kama unatumia Contact lens, kuwa makini , zioshe vizuri na zitunze kwa usahihi
Good 😍
Asante, karibu sana. unaweza kujiunga kuwa mmoja wa wachangiaji katika jukwaa letu.
Stay blessed for this good information
Asante sana, karibu pia, jiunge tuelimishe umma kwa pamoja. Unaweza kuandika makala kisha ukaipakia hapa ili umma uweze kuiona. Asante na karibu.