Maelezo ya jumla
Dalili hutofautiana kulingana na aina ya kimeta. Ugonjwa huu haumbikizwi kutoka kwa mtu moja mpaka mwingine kama ilivyo mafua. Watu walio kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ni wataalamu wa maabara na watu wanashughulika na wanyama. Utambuzi wa ugonjwa huu utafanyika kwa kuangalia dalili na kufanya vipimo. Matibabu yanaweza kuwa antibiotics na antitoksini. Kuna chanjo iliyoidhinishwa kuzuia ugonjwa huu, hata hivyo, chanjo hii hutolewa tu kwa watu walio kwenye hatari ya kupata kimeta.

Je,Ni nini dalili za kimeta?
Dalili za kimeta zinaweza kuwa tofauti, kulingana na aina ya ugonjwa:
Ngozi
- Hii ndio aina inayowapata watu wengi zaidi, mara nyingi mtu huipata baada ya chembe (spore) kuingia mwilini kupitia kidonda kwenye ngozi.
- Dalili ya kwanza ni mchubuko kwenye eneo la uambukizo na kisha lengelenge (blister) hutokea. Baada ya muda lengelenge litatengeneza kidonda chenye weusi katikati. Mchubuko,lengelenge na kidonda haviumi. Katika hali nyingine, dalili kama vile kichwa kuuma, maumivu ya misuli, homa na kutapika, huweza kutokea
- Kuna uwezekano mdogo wa maambukizi ya moja kwa moja kutoka kwenye kidonda cha mtu mmoja kwenda kwenye mwili wa mtu mwingine
Utumbo
Kwa ujumla aina hii hotokea baada ya kula nyama kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa. Dalili za kwanza ni sawa na za kula chakula chenye sumu, na zinaweza kujumuisha:
- Homa na kuhisi baridi
- Kuwa mwekundu na macho kuwa mekundu
- Kichwa kuuma
- Kupoteza fahamu
- Maumivu kwenye koo
- Kuhisi maumivu wakati wa kumeza kitu
- Sauti ku kwaruza kwaruza
- Kuvimba kwa shingo au tezi za shingo
- Kichefuchefu na kutapika, hasa kutapika damu
- Kuharisha au kuharisha damu
- Maumivu ya tumbo
- Tumbo kuongezeka ukubwa
Mapafu
- Aina hii ya kimeta haipatikani kwa urahisi, na ni mara chache sana inawapata watu,lakini ndio yenye kusababisha vifo vingi zaidi kuliko aina nyingine.
- Kwa kawaida maambukizi hutokea baada ya kuvuta hewa yenye chembe (spores) ya kimeta
- Dalili za kwanza baada ya kuvuta hewa yenye chembe za kimeta ni sawa na mafua,na zinaweza kujumuisha:
- Uchovu
- Kuuma kwa koo
- Maumivu ya mwili
- Kukohoa
- Homa na kuhisi baridi
- Kichwa kuuma
- Kupumua kwa shida
- Kijisikia vibaya kifuani
- Kichefuchefu, kutapika, au maumivu ya tumbo
- Kuchanganyikiwa au kizunguzungu
- Kutokwa jasho
- Aina hii ya kimeta haiwezi kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, kwa sababu maambukizi hutokea tu baada ya kuvuta hewa yenye chembe ya kimeta.
Kimeta cha sindano
- Dalili zake ni sawa na kimeta cha ngozi, lakini ugonjwa huu, unaweza kuenea kwa kasi mwili mzima
- Homa na kuhisi baridi
- Malengelenge au vipele vidogo vinavyowasha kwenye eneo ilipochomwa sindano.
- Kidonda kwenye ngozi chenye sehemu ya katikati yenye rangi nyeusi, sehemu hii nyeusi hutokea baada ya malengelenge na vipele.
- Uvimbe kuzunguka kidonda
- Kunaweza kukatokea jipu kwenye sehemu iliyochomwa sindano

Ni nini husababisha kimeta?
Wanadamu wanaweza kuambukizwa kimeta kutoka katika vyanzo viwili:
- Kimeta kutoka kwa wanyama
- Wanadamu wanaweza kuambukizwa kimeta kwa kushughulikia bidhaa kutoka kwa wanyama walioambukizwa au kwa kuvuta hewa yenye chembe za kimeta toka kwenye bidhaa za wanyama walioambukizwa,kama Manyoya.
- Watu wanaweza pia kuambukizwa aina ya kimeta inayoathiri utumbo kwa kula nyama ya wanyama walioambukizwa.
- Kimeta ikitumika kama silaha
- Kimeta inaweza kutumiwa kama Hii ilitokea Marekani mwaka 2001. Kimeta ilienezwa kwa makusudi kupitia mfumo wa posta, kwa kutuma barua zenye poda iliyokua na kimeta. Hii ilisababisha kesi 22 za maambukizi ya kimeta.
Kimeta haisambazwi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
Nani yuko kwenye hatari zaidi?
Watu wengine wanaweza kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa:
- Watu wenye kazi fulani:
- Daktari wa wanyama/Veterinari
- Wataalam wa maabara
- Wazalishaji wa mifugo
- Watu wanaoshughulikia bidhaa za wanyama
- Wafanyakazi wa posta, wafanyakazi wa kijeshi, na wafanyakazi wa huduma ya dharura ,hawa wanaweza kuambukizwa kama kuna tukio la kigaidi la kutumia kimeta kama silaha
- Wasafiri, hasa waendao kwenye maeneo kama vile:
- Amerika ya Kati na Kusini
- Afrika – kusini mwa Jangwa la Sahara
- Asia ya Kati na kusini-magharibi
- Ulaya ya Kusini na mashariki
- Caribbean
- Watu wanaotengeneza au kucheza ngoma zinazotengenezwa kwa ngozi ya Mifugo
Utambuzi wa kimeta
Ni watu waliokutana na chembe za kimeta pekee wanaoweza kuambukizwa kimeta. Utambuzi utafanyika baada ya uchunguzi wa mwili na vipimo. Vipimo vinaweza kujumuisha: [2]
- X-ray kifua
- CT scan
(Katika kesi fulani ya kimeta ya mapafu)
- Ili kuthibitisha utambuzi, vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa:
- Gram stain na culture
- Upimaji wa kingamwili (antibodies) au sumu katika damu
Magonjwa yenye dalili zinazofanana na kimeta
- Homa ya mafua (Influenza)
Wakati gani utafute matibabu ya haraka?
Kama unaonyesha dalili za maambukizi ya kimeta, mwone mtoa huduma wako wa afya mara moja.

Uchaguzi wa matibabu ya kimeta
Antibiotics huhitajika katika mpango wa kutibu aina yoyote ya kimeta. Antibiotcs zinaweza kuzuia kutokea kwa ugonjwa kwa watu waliokutana na chembe za kimeta ,kabla hawajaanza kuonesha dalili. Kwa hiyo, ni muhimu kutambua na kuanza matibabu mapema.
- Kuzuia ugonjwa baada ya kukutana na chembe ya kimeta
- Matibabu ni tofauti kwa mtu ambaye amekutana na chembe za kimeta ,lakini hajaanza kupata dalili yoyote.
- Watoa huduma ya afya watatumia antibiotics (kama vile ciprofloxacin, levofloxacin, doxycycline, au penicillin) pamoja na chanjo ya kimeta ili kuzuia maambukizi ya kimeta
- Chembe (spores) za kimeta zinaweza kukaa mwilini mwa mtu hadi siku 60 bila kusababisha maambukizi yoyote. Watu ambao wamekutana na chembe za kimeta,wanapaswa kutumia antibiotics kwa kipindi hiki chote. Hii itawalinda kutokana na chembe (spores) yoyote iliyodumaa mwilini.
- Matibabu baada ya maambukizi
- Kwa kawaida,matibabu ni kutumia antibiotics kwa siku 60
- Mafanikio hutegemea aina ya kimeta, na ni mapema kiasi gani tiba ilianza baada ya maambukizi
- Antitoksini inapaswa kutumika pamoja na chaguzi nyingine za matibabu, ili kupambana na sumu ya kimeta mwilini. Kwa bahati mbaya antitokisini ni chache na hazipatikani kwa urahisi.

Kuzuia ugonjwa wa kimeta
Kuna chanjo ( Anthrax Vaccine Adsorbed) inayoweza kukukinga dhidi ya kimeta ya ngozi na mapafu , hata hivyo haipatikani kwa umma. Chanjo hii haina bakteria yoyote na haiwezi kuambukiza kimeta. Mtu yeyote ambaye anahisiwa kuwa amekutana na chembe za kimeta anaweza kupewa chanjo hii. Watu kama wafanyakazi wa jeshi,wataalamu wa maabara,watu wanaosafiri kwenda kwenye maeneo yenye kimeta,wanaweza kupewa chanjo hii.
Matumizi ya dharura
- Katika hali fulani, kama vile shambulizi la kigaidi linalohusiana na kimeta, chanjo inaweza kupendekezwa ili kuzuia ugonjwa kutokea kwa watu waliokutana na chembe za kimeta.
- Kama hili litatokea, watu waliokutana na chembe za kimeta watapata sindano 3 za chanjo katika kipindi cha wiki nne ,pamoja na kozi ya antibiotics kwa siku 60.
- Wakati wa dharura, watu pekee ambao hawapaswi kupewa chanjo, ni wale ambao wamepata athari kubwa za mzio (allergy) baada ya chanjo ya mwanzo.
Mimba
- Wanawake wajawazito wanapaswa kupewa matibabu ya kinga sawa sawa na watu wengine,hii ni pamoja na antibiotics na chanjo.
Matumizi kwa watoto
- Chanjo ya kimeta haipaswi kutolewa sambamba na chanjo nyingine za utotoni wakati wa tukio la kimeta
Nini cha kutarajia ?
Matarajio ya kupona ugonjwa wa kimeta hutegemea mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na:
- Aina ya kimeta
- Ni mapema kiasi gani kimeta ilitambuliwa
- Aina ya bakteria anaesababisha kimeta
- Umri wa mgonjwa na afya kwa jumla.
Kuanza tiba ya kimeta mapema iwezekanavyo, bila kujali aina ya kimeta, inaboresha matarajio ya ugonjwa kupona.
Matatizo yanayoweza kutokea
- Kupata shida kupumua
MAELEZO ZAIDI KUHUSU UGONJWA WA KIMETA
Maelezo ya kumla
Ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria ambao hushambulia ngozi, lakini kwa nadra sana unaweza kushambulia koo, mfumo wa upumuji, kifua au utumbo
Sababu
Bacillus anthracis, bakteria
Epidemiolojia
Unapatikana dunia nzima. ni ugonjwa ambao unawapta zaidi wanyama wanaokula manyasi. Wanadamu na wanyama wanaokula nyama wanaupata kwa bahati mbaya. Unawapata zaidi wafanyakazi wanaoshughulika na nyasi za malisho, nywele (hasa za mbuzi), mifupa na bidhaa za mifupa na manyoya: na madaktari wa wanyama na wakulima na wafanyakazi wa mbuga za wanyama wanaoshughulika na wanyama walioambukizwa.
Kimeta kinachowapata wanadamu kinapatikana zaidi katika maeneo ambayo kuna ugonjwa wa kimeta kwa wingi kwa wanyama, hii ni pamoja nan chi za kusini na Ameika ya kati, kuni na mashariki mwa ulaya, Asia na frika.
Uambukizo
- Kimeta ya ngozi: Kukutana na tishu za wanyama (ng’ombe, kondoo, mbuzi, farasi, nguruwe na wengine) wanaokufa kwa ugonjwa. Kuumwa na wadudu ambao wamenyonya damu ya wanyama hao, nywele zilizochafuliwa, manyoya, nyasi za malishi au bidhaa zinazotengenezwa navyo kama vile ngoma au kushinga mchanga alipokuwa mnyama mwenye maambukizi.
- Kimeza ya mapadu: Kuvuta hewa yenye chamvua za vimelea katika mazingira hatarishi ya viwanda vinavyoshughulika na nyasi za malisho ya wanyama, au manyoya au mifupa, ambapo vimelea wa B. antracis wanaweza kurushwa na kuelea kwenye hewa.
- Kimeta cha utumbo au koo: kwa kula nyama yenye maambukzi; lakini hakuna Ushahidi wowote kuwa kunywa maziwa ya mnyama aliyeambukizwa yanaweza kuambukiza
N: B. Ugonjwa huu unasambazwa kati ya wanyama wanaochunga kwa kupitia:
- Mchanga na malisho, na kwa wanaokula mifupa au wasiofugwa kula mizoga ya wanyama wenye kimeta
- Ndege wanaokula mizoga wameonekana kusambaza vimelea kutoka sehemu moja kwenda nyingine
Muda kabla dalili kuanza
Masaa machache mpaka siku saba; kwa visa viingi ni ndani ya masaa 48
Muda wa uambukizo
Maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine ni nadra sana. Vifaa na mchanga uliochafuliwa na vimelea unaweza kuendelea kuambukizwa kwa miongo kadhaa
Dalili
Kimeta cha ngozi
- Karibu 95% ya visa vya kimeta ni vya ngozi, 5% ndio vya mapafu.
- Hupatikana katika maneo ya ngozi yaliyowazi (kichwa, shingo, uso na mikono)
- Kaupele kadogo kekundu hutokea
- Kaupele nakua kuwa upele mkubwa, baadae kuwa lengelenge au lengelenge lenye usaha ndani kwa wiki 1 inayofuata na kutengenezeka kwa kidonda chenye gamba jeusi na uvimbe vinavyozunguka kidonda
- Kaupele kwa kwanza kanaweza kuwasha lakini hakaumi
- Wagonjwa wengi hawana homa katika hali ya kawaida; katika hali kali, kuvimba kunaweza kuongezeka sana
- Mgonjwa anapona bia matibabu kwa 80-90% ya via v
- yote visivyotibiwa lakini kuvimba kunabakia kwa wiki kadhaa.
- Kwa 10-20% ya visa, maambukizi yanaendelea, bakteria wanakua na kwa mara nyingi vinahusiana na homa na kifo cha haraka
Kimeta cha mapafu
- Kutokwa na dalili kama za mafua kunaweza kusababisha iwe ngumu kuutambua mapema
- Dalili za mwanzo zinaanza baada ya siku 1-3. Huku homa ikiongezeka, kushindwa kupumua, kukorota, kukosa hewa ya oksijeni, kupungua kwa presha ya mwili na kupelekea kifo nadani ya masaa 24
Kimeta ya utumbo
Dalili zinatofautiana na zinajumuisha:
- Homa, kichefuchefu na kutapika, maumivu ya tumbo, damu, kuhara, na mara nyingine kujaa maji tumboni
- Kuhara, mgonjwa anaharisha kinyesi kingi sana
Kimeta cha koo
- Homa, kuumwa koo, ugumu kumeza, maumivu na mtoki, kushindwa kupumua vizuri kunaweza kutokea
- Upele wa mwanzi mara nyingi unakaa kwney tonsils
Utambuzi
- Kwa kutumia dalili na rekodi za kitabibu
- Kuchunguza kwa darubini majimaji ya kidonda – gram stain
- Kupandikiza damua u majimaji ya kidonda – culture
Matibabu
Kwa kimeta cha ngozi
- Penicillin-G IV kama uvimbe utapungua na baadae dawa ya kumeza ya penicillin ili kukamisha dozi. Kwa watu wasiotumia penicillin watumie, Ciprofloxacin, erythromycin, Tetracycline, Chloramphenicol
- Safisha na funika kidonda
Kwa kimeta cha mapafu, utumbo na koo
Kiwango kikubwa cha dozi ya penicillin kinahitajika
Kuzuia
- Takasa manyoya na nywele za mbuzi na boresha mazingira kwa wafanyakazi wanaoshughulika na bidhaa za wanyama
- Chanjo kwa makundi ya watu wanayoonekana yako hatarini
- Mizoga ya wanyama inapaswa kuzikwa ikiwa mizima bila kuikata
- Kuchinja mnayama mwenye maambukizi kusiruhusiwe
- Elimu kuhusu namna ya uambukizo na namna ya kushughulikia vidonda
- Tibu wanyama wenye maambukizi