Unaweza kuambukizwa ugonjwa kwa kuogelea?
Kuogelea kwa kawaida ni shughuli nzuri na salama. Unaweza kupata ugonjwa kama maji unayoogelea yana vimelea na ukayanywa au wakaingia kupitia kwenye jeraha. Unaweza pia kupata maambukizi kwenye mabwawa ya kuogelea, hata kama maji yametibiwa vizuri kwa dawa ya chlorine. Kuna baadhi ya bakteria, virusi na vimelea kwenye mabwawa ya kuogelea wanaoweza kuendelea kuishi hata baada ya maji kutibiwa.
Ninaweza kupata aina gani ya ugonjwa?
Watu wengi wanougua baada ya kuogelea wana harisha. Mara nyingi mtu hupona bila matibabu yoyote. Unaweza pia kupata ugonjwa wa homa ya mapafu (nyumonia) na magonjwa mabaya ya ngozi kutokana na maji yaliyochafuliwa.
Ni wakati gani unapaswa kumwona daktari?
Ongea na daktari kama una harisha damu, unaharisha kwa zaidi ya wiki moja , au kama unakohoa na una homa. Onana na daktari haraka sana kama una dalili nyingine kali, kama vile homa na kukakamaa kwa shingo baada ya kuogelea kwenye mabwawa ya mtaani, au kama una ugonjwa mbaya wa ngozi na una homa. Hakikisha unamwambia daktari kuwa uliogelea kwenye maji hayo.
Nifanyeje nisiendelee kuugua kila nikiogelea?
- Usinywe maji unapokuwa ndani ya bwawa la kuogelea, ziwani, chemichemi, mto, bwawa au baharini.
- Usinye maji yasiyotibiwa kutoka kwenye ziwa, mito, chemichemi, bwawa, au visima visfupi.
- Hakikisha unasoma vibao vya tahadhari vilivyowekwa karibu au kuzunguka mabwawa kuhusu kuogelea humo na shughuli nyingine. Baadhi ya mabwaya yamechafuliwa na sio afya kuogelea humo.
Nitawakingaje wengine wasiugue baada ya kuogelea?
- Usiende kuogelea kama una harisha au kama umepona hivi karibuni. Hii ni muhimu sana kwa watoto wanaovaa nepi.
- Kama umepata ugonjwa wa kuhara unaoitwa giardiasis, usiogelee mpaka angalau wiki ipite baada ya kuacha kuhara.
- Oga kabla ya kuingia kwenye maji
- Wasafishe vizuri watoto (hasa matako) kwa kutumia sabubi na maji baada ya kujisaida au baada ya kuwabadili nepi.
- Wapeleke wanao chooni mara kwa mara na kagua nepi zao mara kwa mara
- Badili nepi za watoto ukiwa chooni, sio karibu na maji.
Vyanzo
https://medlineplus.gov/ency/article/000622.htm