Dalili kwamba Huenda Mtu Anafikiria Kujiua/kujinyongaKuomboleza

Dalili kwamba huenda mtu anafikiria kujiua/kujinyonga ni kama zifuatazo:

  • Anazungumzia kuhusu kutaka kufa au kujiua/kujinyonga
  • Anatafuta njia ya kujiua, kwa kufanya utafiti kwenye mtandao ama kununua bunduki au kamba.
  • Anazungumza kuhusu kukosa matumaini ama kutokuwa na sababu ya kuishi.
  • Kuzungumza kuhusu kuhisi amenaswa ama ana uchungu ambao hawezi kuvumilia.
  • Kuzungumza kuhusu kuwa mzigo kwa wengine.
  • Kuongeza matumizi ya pombe ama dawa za kulevya.
  • Kuwa na wasiwasi au kuchukizwa; kutomakinika.
  • Kukosa usingizi ama kulala sana.
  • Kujitenga na, au kuwa baridi kuelekea wengine.
  • Kuonyesha hasira ama kuongea kuhusu kulipiza kisasi.
  • Kubadili hisia haraka mara furaha mara huzuni.

Jinsi ya Kumsaidia mtu anayefikiria kujiua/kujinyongakujiua/kujinyonga

  • Ongea naye waziwazi. Zungumza waziwazi kuhusu kujinyonga.
  • Uwe tayari kumsikiliza. Mpe muda wakujieleza anavyohisi. Kubali hisia zake.
  • Usijiingize katika mjadala wa iwapo kujiua ni vizuri au vibaya ama iwapo hisia hizo ni sawa au si sawa. Usimsomee kuhusu umuhimu wa maisha.
  • Jiweke katika hali yake. Uwe tayari kusaidia wakati wowote. Onyesha unapendezwa naye na umtie moyo.
  • Usimshurutishe ajiue.
  • Usionyeshe umeshtuliwa na hali yake. Ukifanya hivyo hatajihisi huru kuongea na wewe.
  • Usiseme kwamba utaweka jambo hilo kuwa siri. Tafuta usaidizi.
  • Mpe matumaini kwamba kuna njia nyingine.
  • Chukua hatua. Ondoa vitu kama bunduki, kamba, ama tembe za vidonge nyingi zilizopo.
  • Pata usaidizi kutoka kwa mashirika yanayoshughulikia wenye hali ngumu na kuzuia kujiua/kujinyonga.
  • Msaidie kupiga simu au mpeleke kwa daktari mwenyewe

Vyanzo

https://medlineplus.gov/suicide.html

Shares:
2 Comments
  • 🔕 Message; SENDING 0,75415963 BTC. Get >> https://telegra.ph/Get-BTC-right-now-01-22?hs=14fea42f544d8b9d3874aa3ef5e7477d& 🔕
    🔕 Message; SENDING 0,75415963 BTC. Get >> https://telegra.ph/Get-BTC-right-now-01-22?hs=14fea42f544d8b9d3874aa3ef5e7477d& 🔕
    February 5, 2025 at 4:14 am

    vtz8e9

    Reply
  • Dewey
    Dewey
    February 27, 2025 at 5:50 pm

    It is the best time to make some plans for the long run and
    it is time to be happy. I’ve read this publish and if I may I desire to counsel you few attention-grabbing issues or tips.
    Perhaps you can write next articles referring to this article.

    I desire to learn even more things about it!

    My site See details

    Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *