Maelezo ya jumla
Kutoa/ kuondoa kitu jichoni – kama ukiingiliwa na kitu jichoni, kinaweza kuleta usumbufu , kikasababisha wekundu kwenye jicho, kutokwa machozi na hata kupunguza uwezo wa kuona. Mara nyingi utakuta kitu kilichoingia jichoni ni kidogo sana, kama vile unywele wa kope, kipande cha vumbi au uchafu, na hivi huoshwa na kuondolewa na machozi unapofumba na kufumbaua macho. Kama kikibakia kwenye sehemu nyeupe ya jicho na una uhakika hakuna uharibifu zaidi, kwa kawaida unaweza kukitoa mwenyewe au ukaomba msaada wa mtu mwingine akusaidie kukitoa.
Mwone daktari haraka kama
Ni vizuri kumwona daktari haraka kama
- Kama kitu kilichoingia jichoni kimeng’ang’ania ndani au kwenye jicho
- Kama unadhani kuwa kuna kitu kimeingia kwenye jicho wakati unatumia kifaa cha umeme kufanyia kazi, kwa mfano msumeno, nyundo au vifaa vya kuchimba mbao ‘’chisel’’. Kipande kidogo cha kifaa kinaweza kukatika kikapenya kama risasi na kuingia sehemu ya ndani ya jicho na kuleta matatizo makubwa
Kuondoa kitu jichoni – unachoweza kufanya mwenyewe
Fanya mambo yafuatayo kuondoa uchafu au vumbi kwenye sehemu nyeupe ya jicho
- Usifikiche jicho lililoathirika. Nawa mikono yako vizuri. Kama umevaa lenzi za macho ‘’contact lens’’ zivue haraka.
- Kama unamsaidia mtu mwingine, mwambie akae mahala mbapo pana mwanga wa kutosha na kisha chunguza kama utaona kitu kilichoingia jichoni kwa kufungua kope ya chini ya jicho na kisha mwambie aangalie juu na kisha kushoto na hatimae kulia. Rudia hatua hii kwenye kope ya juu, kwa kuvuta na kufungua kope ya juu, kisha mwambie aangalie chini, kushoto na kulia. Ili kujikagua mwenyewe , kaa mbele ya kioo na kisha vuta kope ya juu juu na kope yako ya chini chini
- Kama haujaweza kutoa kitu kilichoingia jichoni kwenye sehemu yenye weupe ya jicho, jaribu ‘’ku- flush’’ jicho kwa kutuma maji
- Ili kuondoa kitu kilichoingia kwenye jicho unaweza ku-flush jicho kwa maji kwa kutumia njia zifuatazo
- Kama unamsaidia mtu mwingine, kwanza mfunike kwa taulo kwenye mabega ili maji yanayomwagika yasimlowanishe sana. Mwambie aegemeze kichwa kuelekea upande wa jicho lililoathirika. kisha mwaga maji taratibu kwenye kona ya jicho iliyo karibu na pua ili kuruhusu maji yamwagike kupitia kona ingine.
-
- Kama unajitibu mwenyewe, jaza glass ndogo kwa maji, weka taulo kwenye mambega ili usilowane kwa maji. Kisha weka jicho ndani ya glass iliyojaa maji huku umelifumbua. Fanya kama unamwaga maji ndani ya jicho ili yaweze kusafisha kabisa
- Kama njia hii ya ku –flush haijakiondoa, jaribu kukiondoa kwa kukiondoa kwa kutumia upande wa nguo, kitambaa cha mkononi kilicholowanishwa au tishu
- Kama kitu chenyewe kiko sehemu ya ndani ya kope ya juu ya jicho, shika nywele za kope na uibinue ili kuona sehemu ya ndani na kisha kiondoe kwa kuifuta
Kuondoa kitu jichoni – mwone daktari kama
Ni vizuri kupanga kumwona daktari kama:
- Kama unaona kitu kilichoingia jichoni hakitoki au hakitolewi kwa urahisi
- Kama unapata maumivu, wekundu wa jicho, kuumizwa sana na mwanga ukiuangalia au kama unashinda kuona vizuri baada ya kuondoa kitu kutoka jichoni
Je kope iliyo inamia kwenye jicho naitoaje inakwangua jicho