Maelezo ya jumla

Kupoteza fahamu ni tatizo linaloweza kutishia maisha. Tatizo hili linaweza kusababishwa na sababu nyingi, hii ni pamoja na jeraha baya la kichwa; kuvuja damu nyingi sana; kupungua kwa mzunguko wa damu mwilini; sumu; matatizo ya upumuaji; au ugonjwa mkali sana. Mtu ambaye amepoteza fahamu hawezi kushtushwa na kelele kubwa. Macho yanaweza kuwa yamefungwa. Kama mgonjwa atakuwa amelala mgongo (chali), kuna hatari ya ulimu kurudi nyuma na kuziba njia ya hewa, na kupaliwa kama akitapika. Kama akiacha kupumua, anahitaji kupatiwa msaada kupumua.

Mwone daktari haraka sana

  • Kama mtu yeyote amepoteza fahamu. Mtu ambaye amepoteza fahamu anahitaji msaada wa kidharura.

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe nyumbani

Lengo lako kuu ni kumfikisha mgonjwa katika kituo cha afya ili apate matibabu, lakini pia kuangalia upumuajia, na kusaidia njia ya hewa kubakia wazi mpaka msaada utakapofika au mpaka utakapomfikisha mgonjwa kituo cha afya. Ni muhimu sana kumsaidia ili asipaliwe na ulimi au kitu kingine chochote kwenye njia ya hewa. Unapaswa pia kuangalia kama ana jeraha lolote linaloonekana ulitibu na ujiandae kumsaidia mgonjwa kama ataacha kupumua na/au kama mzunguko wa damu utapungua. Fanya yafuatayo;

  1. Ongea kwa nguvu ili usikike na muulize mgonjwa swali la kawaida kama vile ‘’unaitwa nani?’’ Mwambie mgonjwa afungue macho. Mtikise kidogo mabega (kwa watoto unaweza kupiga piga mabega au miguu kwa kiganja chako). Kama akikuitikia, mwache mgonjwa kama ulivyomkuta. Omba msaada ili kumfikisha kituo cha afya na kisha mtibu majeraha yoyote aliyonayo.

ANGALIZO: Kupoteza fahamu – Mgonjwa yeyote ambaye amepoteza fahamu anaweza kuwa ameumia au amepata jeraha kwenye shingo, kwa hiyo unapomuhudumia kuwa makini sana. Ukimtikisha au kumuhamisha inaweza kusababisha shida kuwa kubwa zaidi. Kama ni muhimu kumuhamisha omba msaada ili kupunguza mtikisiko wa shingo kadri inavyowezekana

  1. Kama mgonjwa hakuitika, piga kelele kuomba msaada. Saidia kufungua njia ya hewa kwa kuweka mkono mmoja kwenye paji lake la uso na kubinua kichwa chake kuelekea nyuma (kama inavyoonekana kwenye picha) Kama kuna kitu chochote kinachoziba njia ya hewa mdomoni kiondoe na unyanyue kidevu chake kwa vidole vyako. Kagua kama anapumua kwa kumwangalia au kusikiliza kifua au kwa kusogeza uso karibu na pua kwa angalau sekunde 10.kupoteza fahamu
  2. Kama mgonjwa anapumua, mgeuze na mweke mkao wa kupumzika ”recovery position” kama ilivyooneshwa kwenye picha hapo chini. Angalia kama ana sehemu aliyoumia na uitibu, kama vile kuvunjika, au kuvuja sana damu. Endelea kufuatilia na kurekodi mapigo ya moyo na upumuaji wake mara kwa mara mpaka mgonjwa atakapofika hospitalini.kupoteza fahamu

Angalia pia: Kuvuja damu sana

Angalia pia: Kuvunjika au kuteguka

  1. Kama mgonjwa hapumui, omba msaada ili umfikishe mgonjwa kituo cha afya. Mpulizie pumzi mbili mdomoni baada ya kuziba pua. Angalia kama mzunguko wa damu uko vizuri kwa angalau sekunde 10. Kama mgonjwa hapumui na mzunguko hauko vizuri, Anza kukanda kifua (Angalia CPR kujifunza mbinu hii). Baada ya kumfikisha kituo cha afya, eleza kila kitu kilichotokea na ulichoweza kufanya.

Angalia pia: Namna ya kufanya CPR – makala inaandaliwa

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000022.htm

Shares:
3 Comments
  • Philipo Muhozi
    Philipo Muhozi
    October 26, 2022 at 1:07 am

    Hi jaman mi naomba msaada nikilala usiku nakuja amka naambiwa nilipoteza fahamu iki kitu kinatokea usiku tu najikuta uchovu mkubwa saaana na nakuwa na kitu kama kinapanda kooni na kinanifanya kukohoa saana kwa mfururizo nin tatizo na matibabu jmn

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      November 4, 2022 at 6:01 pm

      pole sana. ni vzr kufanyiwa uchunguzi na daktari. kuna matatizo mengi yanayoweza kusababisha ikawa ngu,u kupumua usiku. hasa kwa watu wanaokoroma wanaweza kuwa na tatizo linaloitwa sleep apnea ambalo husababisha iwe ngumu usiku. mwone dakatri

      Reply
  • Philipo Muhozi
    Philipo Muhozi
    October 26, 2022 at 1:08 am

    Naomba msaada wa mawazo

    Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *