Kutawaliwa (kupata uraibu) ni nini?

Kutawaliwa (kupata uraibu) ni tatizo la mtu kutoweza kuacha kunywa pombe au kutumia mihadrati/dawa za kulevya hata kama angependa kufanya hivyo. Haja/tamaa/hamu ya kunywa au kutumia mihadrati/dawa za kulevya ni ngumu sanakudhibiti hata kama anajua kwamba mihadrati/dawa za kulevya zinamletea madhara yeye mwenyewe au familia yake.

Watu wanapoanza kunywa au kutumia mihadrati/dawa za kulevya huwa hawapangi Kupata uraibu . Huwa wanapenda namna inavyowafanya wahisi raha. Wengi wao huwa wanaamini kwamba wanaweza kudhibiti kiasi cha dawa na mara ngapi wazitumie hizo dawa. Lakini kadri anavyoendelea kutumia, mihadrati/dawa za kulevya hubadilisha ubongo. Watumiaji mihadrati/dawa za kulevya wanaanza kuitegemea mihadrati/dawa za kulevya ili tu kurudi katika hali ya kawaida. Uraibu wa dawa au pombe unaweza kutawala kabisa maisha ya mtu na kuvuruga kabisa mwenendo wa maisha haraka sana.

Kutawaliwa (kupata uraibu) ni ugonjwa wa ubongoKutawaliwa (kupata uraibu)

Kutawaliwa ni ugonjwa wa ubongo

  • Mihadrati/dawa za kulevya hubadilisha jinsi ambavyo ubongo hufanya kazi.
  • Mabadiliko haya kwenye ubongo yanaweza kuwepo kwa muda mrefu sana, hata baada ya kuach kutumia dawa/mihadarati
  • Mabadiliko haya yaliyo ubongoni yanaweza kusababisha matatizo kama kubadilika kwa hisia, kupoteza kumbukumbu/fahamu na kushindwa kufikiri na kufanya maamuzi.

Kutawaliwa/uraibu  ni ugonjwa, kama tu kisukari na saratani. Kupata uraibu si udhaifu tu. Watu wa matabaka yote, wawe tajiri au maskini, wanaweza kupata uraibu. Kutawaliwa (kupata uraibu) kunaweza kutokea katika umri wowote, hata hivyo huwa inaanza wakati mtu angali mdogo.

Madhara yanayotokana na tatizo la kutawaliwa (kupata uraibu)

Wakati mtu ametawaliwa na mihadrati/dawa za kulevya au pombe, unywaji pombe au utumiaji mihadrati/dawa za kulevya huweza kuwa ndicho kitu muhimu zaidi katika maisha yake, muhimu kuliko kula au kulala. Haja/tamaa ya kupata na kutumia mihadrati/dawa za kulevya unaweza kujaza nafasi ya kila wakati katika maisha ya mtu.

Kutawaliwa (kupata uraibu) kule huchukua nafasi ya kila kitu ambacho mtu yule alikuwa anafurahia. Mtawaliwa anaweza kufanya kitu chochote—kudanganya, kuiba au kuumiza watu—ili aendelee kunywa au kutumia mihadrati/dawa za kulevya ule. Vitu hivi huweza kumfanya mtu huyo akamatwe. Kwa upande mmoja, kupata uraibu huhisi vizuri sana kiasi cha kwamba huwa wanataka kutumia nyingi zaidi. Kwa upande mwingine, Kutawaliwa (kupata uraibu) husababisha athari mbaya.

Nini cha kufanya kama umeamua kuacha kutumia mihadarati/dawa za kulevya?

Watu huacha kutumia mihadrati/dawa za kulevya na pombe wanapogundua kuwa imewadhuru na kuwaathiri vibaya kabisa. Unapogundua kuwa umedhurika na kuathirika vibaya na unajuta, uko tayari kuacha.

Ikiwa unahitaji msaada au unajua yeyote anayehitaji msaada kutibu Kutawaliwa , unaweza kupiga simu au kumpeleka kwa daktari wa kituo cha afya kilichopo karibu ili upate maelezo/matibabu/usaidizi.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/druguseandaddiction.html

Shares:
2 Comments
  • Asia khalfan
    Asia khalfan
    March 10, 2025 at 10:25 am

    Thanks you

    Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *