Kutoboa/kutoga mwili ili kuweka urembo ni nini?
Kutoboa/kutoga mwili ni hali ya kutoboa tundu kwenye ngozi ili kuweka urembo kama pambo.
Ni maeneo gani ya mwili yanayohusika wakati wa Kutoboa/kutoga mwili?
Kutoga sehemu laini ya sikio ili kuweka hereni ndio sehemu inayotogwa zaidi. Baadhi ya watu wanatoga sehemu ya juu ya sikio (sehemu ngumu). Baadhi ya sehemu nyingine zinazotogwa ni pamoja na:
- Sehemu ya nyusi za jicho
- Pua
- Ulimi
- Midomo
- Kitovu na
- Via vya uzazi (sehemu za siri)
Je, Kutoboa/kutoga mwili ni hatari?
Kwa baadhi ya nyakati, watu wanaweza kuambukizwa maambukizi mabaya, maambukizi kama ya virusi vya ukimwi (VVU) na Homa ya ini yanaweza kusambazwa wakati wa kutogwa mwili.
Matatizo mengine ni pamoja na kuvuja damu, kuvimba, kupata makovu na kupata mzio mkali kutokana na mapambo unayovaa.
Kuvunjika au kusagika kwa meno na kuumia kwa fizi kunaweza kutokea kwa watu waliotoga ulimi na midomo. Vito vya thamani vilivyowekwa kwenye mdomo au pua vinaweza kumezwa wakati wowote.
Kwa nini ni hatari kutoga sikio sehemu ya juu?
Unapotoboa sikio sehemu ya juu, unaweza kutoboa gegedu na ikawa ngumu kupona. Aina hii ya utoboaji ni hatari sana kuliko kutoboa sehemu laini ya sikio. Kuna hatari zaidi ya kupata maambukizi ukitoboa sehemu ya juu, na inaweza kuwa ngumu kutibu maambukizi ya aina hii kuliko kama umetoboa sehemu laini.Β Kama gegedu linalotengeneza sikio litapata maambukizi, inaweza kuharibu kabisa mwonekano wa sikio.
Nitajuaje kama sehemu niliyotoga mwili imepata maambukizi?
Kama sehemu uliyotoga mwili itakuwa imepata maambukizi itakuwa nyekundu na kuvimba. Inaweza kuwa inauma ukiigusa, na kunaweza kuwepo majimaji ya njano, yanayonuka yanayotokea kwenye shimo ulilotoboa. Kama una homa au dalili yoyote kati ya hizi, ni vizuri kuoana na daktari.
Je, maambukizi yanatibiwa vipi?
Maambukizi ya kawaida yanaweza kutibiwa kwa dawa za kupaka za kununua duka la dawa. Kama una maambukizi makali sana, daktari anaweza kukuandikia dawa kali zaidi. Baadhi ya watu wenye maambukizi makali zaidi wanaweza kuhitaji upasuaji ili kuwa sawa.
Ni nini kinaweza kuongeza hatari wakati wa Kutoboa/kutoga mwili?
Kuma mambo mengiΒ yanayoweza kuathiri uwezo wa mwili kupambana na maambukizi. Ni vizuri kumwambia mtu anaye kutoboa/kutoga mwili kuwa una kisukari, matatizo ya moyo, au matatizo mengine ya afya. Kama unatumia dawa aina ya steroids au dawa za kuzuia damu kuganda (blood thinners), ongea na daktari kabla ya kutoga.
Ni nani anapaswa kunitoga mwili?
Kama unakwenda Kutoboa/kutoga mwili, ni vizuri kumtafuta mtaalamu mwenye sifa nzuri. Tafuta mtu anayejali usafi na ayetakasa vyema vifaa anavyotumia. Utoboe mwili mwenyewe, na usimruhusu mtu yoyote ambaye sio mtaalamu ku kutoboa/kutoga mwili. Usiharakishwe kufanya uamuzi wa Kutoboa/kutoga mwili. Chagua sehemu ya mwili unayotaka kutoga kwa umakini.
k3v8a7