Kutoka kwa mimba/ujauzito ni nini?

Kutoka kwa mimba/ujauzito ni hali inayotokea ujauzito unapoacha kukua. Hali hii inatambuliwa baada ya mwanamke kutokwa damu katika hatua za mwanzo za ujauzito, au inaweza kutambuliwa wakati wa vipimo vya kawaida.

Kutoka kwa mimba/ujauzito kunatokea kwa ujauzito ambao kwa hali ya kawaida usingekuwa na afya kwa sababu ambazo ziko juu ya uwezo wako. Hali hii haisababishwi na msongo wa mawazo au shughuli za kawaida kama vile kucheza michezo au kufanya ngono.

Ni nini hutokea wakati wa Kutoka kwa mimba/ujauzitoKUTOKA KWA MIMBA

Kama mimba yako inatoka na tishu hazijatoka zote, kuna machaguo matatu ya matibabu;

  1. Kuendelea kuangalia na kusubiri; Unasubiri mimba itoke yenyewe
  2. Kutumia dawa: tumia dawa inayoitwa misoprostol kusababisha mimba itoke haraka
  3. Kufanyiwa utaratibu wa kusafishwa: Daktari atatoa tishu za ujauzito kwa kufanya utaratibu mdogo kwenye ofisi yake

Machaguo haya matatu yote ni salama na hayataathiri iwezo wako wa kupata ujauzito baadae.

Wakati wa Kutoka kwa mimba/ujauzito nichague njia gani?

Aina ya matibabu utakayopata itategemea ni aina gani ya Kutoka kwa mimba/ujauzito uliyonayo;

  • Mimba inayoendelea kutoka – Tishu za ujauzito zinapoanza kutoka zenyewe. Tumia njia ya kuangalia na kusubiri, tishu za ujauzito zinatoka zenyewe na kuisha kwa 90% ya visa, lakini mchakato huu unaweza kuchukua wiki kadhaa. Ukitumia dawa za misoprostol, tishu zinatoka kwa 90% ndani ya wiki moja.
  • Mtoto kufia tumboni – Ni pale ujauzito unaposimama kukua na hautoki wenyewe. Kutumia njia ya kuangalia na kusubiri, aina hii ya Kutoka kwa mimba/ujauzito, ujauzito utatoka wenyewe kwa 75% visa. Ukitumia dawa ya misoprostol, tishu zinatoka kwa 90% visa ndani ya wiki moja.
  • Mfuko wa mtoto usio na kitu (empty sac) –Ni pale ujauzito unaposimama kukua kabla mtoto hajatengenezeka, unatengenezeka mfuko wa kumbebea tu, ndani hakuna mtoto. Kutumia njia ya kuangalia na kusubiri, aina hii ya Kutoka kwa mimba/ujauzito inatoka yenyewe 66% ya visa, lakini itachukua wiki kadhaa. Kutumia misoprostol, tishu zitatoka kwa 80% ya visa ndani ya wiki moja.

Wanawake wengi huchagua njia ya kuangalia na kusubiri kama chaguo lao la kwanza. Kama ikichukua muda mrefu, unaweza kurudi kwa daktari ili kuchagua njia nyingine. Kama dawa hazijasaidia, unaweza kurudi kwa daktari kufanyiwa utaratibu wa kusafishwa mji wa mimba kwa kutumia vifaa. Njia ya kusafisha inafanya kazi ya kutoa mabaki ya tishu kwa 100% ya visa kwa aina yoyote ya kutoka kwa mimba.

Baada ya kuchagua matibabu, nitegemee nini kitokee?

Nini cha kutegemea kama umeamua kuangalia na kusubiri:

Kukaza kwa tumbo na kutoka kwa damu kunaweza kuanza wakati wowote. Mara nyingi maumivu ya tumbo yanazidi kuongezeka na damu inayotoka inazidi kuwa nzito kuliko ya hedhi inavyokuwa. Kutokwa damu nzito sio hatari na inatoka kwa masaa matatu mpaka matano. Kutoka damu nyepesi kunadumu kwa muda wa wiki moja mpaka mbili na inaweza kusimama kutoka na kuanza tena mara kadhaa. Kutumia dawa za maumivu kama vile ibuprofen kunasaidia.

Nini cha kutarajia kama umeamua kutumia dawa:

Vidonge vya misoprostol vinawekwa ukeni wakati utakapoamua. Kwa kawaida maumivu ya tumbo na kutokwa damu huanza baada ya masaa mawili mpaka sita baada ya kuwekewa kidonge na kudumu kwa masaa matatu mpaka matano. Ukiweka maji ya moto kwenye chupa na ukaiweka tumboni, kutumia dawa za ibuprofeni na/au kutumia dawa nyingine za maumivu kunaweza kukupunguzia karaha.

Baadhi ya wanawake wanapata kichefuchefu, kutapika, au kuhisi baridi baada tu ya kutumia misoprostol. Hali hii itaisha baada ya masaa machache. Kutumia dawa ya ibuprofen husaidia kupunguza baadhi ya maudhi. Damu inayotoka inaweza kuwa nzito kuliko inayotoka wakati  wa hedhi. Kutokwa na damu zito sio hatari; hii inamaanisha kuwa dawa inafanya kazi. Damu inapoanza kutoka nyepesi inaweza kuchukua wiki moja mpaka mbili, na inaweza kusimama kutoka na kuanza tena mara kadhaa.

Nini cha kutegemea ukiamua kufanyiwa utaratibu wa kusafishwa kizazi

Kutumia dawa za maumivu kabla ya kufanyiwa utaratibu huu hupunguza maumivu ya tumbo. Mwanzo wa utaratibu unafanana na ule unaofanyika wakati wa kukupima njia ya uzazi au wakati wa kufanyiwa uchunguzi sehemu za siri. Ili kupunguza maumivu, unaweza kuchomwa sindano ya kupunguza maumivu kuzunguka mlango wa shingo ya kizazi. Mlango wa kizazi unapanuliwa ili kufunguka na tishu zinaondolewa kwa kutumia vifaa maalumu.

Utaratibu huu kwa kawaida unatumia dakika 10 hivi. Baada ya kupumzika dakika 15 mpaka 30, unaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani. Wanawake wengi wanaweza kuendelea na shughuli zao za kawaida siku inayofuata baada ya utaratibu huu. Ni kawaida kuhisi maumivu ya tumbo au kutokwa damu nyepesi kwa siku kadhaa baada ya utaratibu huu.

Ni nini hutokea baada ya kutoka kwa mimba?

Utapatiwa maelekezo kabla hujaruhusiwa kwenda nyumbani. Ongea au kamwone daktari kama una matatizo yafuatayo:

  • Kuvuja damu nyingi inayosababisha kulowa kwa maxi pad mbili ndani ya saa moja, kwa masaa mawili mfululizo
  • Joto la mwili au homa zaidi ya 1020F / 380C (Homa ya kufikia 380C au chini kidogo ya hapo ni kawaida kwa watu wanaotumia dawa za misoprostol)
  • Kujisikia kuumwa, maumivu sehemu ya chini ya tumbo baada ya maumivu makali na kutokwa damu

Baadae ukirudi tena hospitali kwa mara ya pili, daktari atahakikisha kuwa mimba ilitoka yote kwa kutumia ultrasound, kipimo cha damu, au vyote kwa pamoja. Miadi hii ya mara ya pili ni furusa ya kuongea kuhusu hisia zozote ulizonazo baada ya mimba kutoka.

Baada ya mimba kutoka, unaweza kujaribu kupata ujauzito pale tu mtakapojisikia tayari wewe na mwenzi wako mko tayari kupata mtoto tena. Kama haujisikii kupata mtoto kwa wakati huu, hakikisha unatumia njia ya uzazi wa mpango.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/miscarriage.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *