Maelezo   ya jumla

Kuvimba kilimi / Kuvimba kimeo ni hali inaweza kukera sana . Kuvimba kilimi (uvulitis) mara nyingi huambatana na kuvimba kwa eneo la koromeo (phyrinx), mafindofindo (tonsilitis), kidaka tonge (epiglotis)  au kaakaa la mdomo (palate). Kilimi ni tishu ndogo yenye umbo kama ulimi inayoning’inia kwenye sehemu ya nyuma ya mdomo.

Visababishi vya kuvimba kimeo ni:

Kuvimba kwa kilimi mara nyingi husababishwa na maambukizi ya bakteria – Bakteria ambao husababisha tatizo la kilimi, ndio hao hao husababisha ugonjwa wa homa ya mapafu ”pneumonia”, homa ya uti wa mgongo “Meningitis” na maambukizi katika Mfumo wa damu.
Sababu nyingine ni pamoja na:

  • Kuunguzwa na vinywaji vya moto
  • Kuumia eneo la koo
  • Mzio ”allergy” unaotokana na kizio kama vile chamvua za mimea, vumbi, chakula kama vile njugu au mayai au manyoya ya wanyama
  • Kuvuta au kumeza aina fulani za kemikali
  • Uvutaji wa sigara

Dalili za kuvimba kimeo ni pamoja na:kuvimba kimeo

Dalili zinazoweza kuonekana ni kama ifuatavyo:

Utambuzi wa kuvimba kimeo :

Ili kutambua kama kilimi kimevimba daktari atakufanyia uchunguzi wa mwili na kuangalia sehemu ya nyuma ya mdomo ili kukagua kilimi na koo. Daktari anaweza kuagiza ufanyiwe vipimo vifuatavyo:

  • Kuchukua sampuli kwenye sehemu ya nyuma ya koo ”throat swab” ili kuchunguza ni aina gani ya bakteria wanaosababisha kilimi kuvimba
  • Vipimo vya damu
  • Vipimo vya kuangalia kama una mzio

Matibabu ya kuvimba kimeo :

Kwa wakati fulani kuvimba kwa kimeo/kilimi kunaweza kupona kwenyewe bila matibabu yoyote. Ili kukupatia matibabu yanayostahili daktari atakupatia dawa kulingana na sababu ya ugonjwa:

  • Antibiotiki ili kutibu maambukizi
  • ”Steroids” ili kupunguza uvimbe wa kilimi
  • ”Antihistamines” kutibu mzio kama imegundulika kuwa una mzio ”allergy”

Daktari anaweza pia kupendekeza ufanye mambo yafuatayo nyumbani ili kupunguza karaha na kupata nafuu:

  • Pumzika
  • Kunywa vinywaji kwa wingi
  • Sukutua kwa kutumia maji yaliyotiwa chumvi ili kupunguza uvimbe
  • Tumia dawa za maumivu kama ”acetaminophen” au ”ibuprofen” ili kupunguza maumivu
  • Usivute sigara na epuka kukaa karibu na mtu anayevuta, moshi unaweza kusababisha hali kuwa mbaya zaidi

Kama uvimbe kwenye kilimi hautapungua hata baada ya kutumia dawa, daktari anaweza kupendekeza ufanyiwe upasuaji. Upasuaji huu hufanyika ili kukata/kuondoa sehemu ndogo ya kilimi.

Matarajio baada ya kuvimba kilimi

Kwa kawaida mgonjwa mwenye tatizo la kuvimba kilimi hupona baada ya siku 1 au 2 bila matibabu au baada ya matibabu

Matatizo yanayoweza kutokea

Kama tatizo la kuvimba kilimi litaendelea kuwepo bila kutibiwa, linaweza kuababisha shida ya kupaliwa na hata kuzuia au kuathiri upumuaji wa mgonjwa

  • Kuathiri mfumo wa upumuaji – Kilimi kinapovimba huweza kuzuia hewa kuingia kwa uhuru, hali hii inaathiri kiwango cha hewa ya oksijeni mwilini. kushindwa kwa mfumo wa upumuaji  kufanya kazi ipasavyo huongeza hewa ya kabonidioksidi ambayo ni sumu mwilini.
  • Kuenea kwa maambukizi: Maambukizi ya bakteria yanaweza kuenea maeneo tofauti tofauti ya mwili, na kuathiri mapafu, uti wa mgongo au mfumo wa damu.

Wakati gani umwone daktari?

Ni vizuri kutafuta msaada wa kitabibu kama:

  • Unashindwa kula vizuri
  • Dalili hazipungui au unaona hali inazidi kuwa mbaya zaidi
  • Una homa kali
  • Dalili zinaanza kurudi tena baada ya kumaliza tiba uliyopangiwa na daktari

Kama unapaliwa au unakabwa na unashindwa kupumua vizuri, omba msaada ufikishwe kituo cha afya haraka. Katika hali kali sana, daktari anaweza kukuwekea mpira kupitia kooni ili kusaidia kuingiza hewa kwenye mapafu.

Kuzuia

Kama una mzio ”allergy” na kitu chochote, jaribu kukiepuka ili usikutane nacho. Kizio ni kitu chochote ambacho ukikutana nacho kinasababisha upate tukio kali la mzio ”allergic reaction”

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001257.htm


Imeandaliwa na:  Dr joh.

Shares:
15 Comments
  • Dr.Mniko
    Dr.Mniko
    April 6, 2021 at 11:59 pm

    Kazi nzuri sana Dr.

    Reply
  • Dr johnson
    Dr johnson
    April 7, 2021 at 7:29 am

    Shukran mkuu

    Reply
  • DR NYARIGO
    DR NYARIGO
    April 9, 2021 at 5:58 pm

    very good DR joh

    Reply
    • Dr.Mniko
      Dr.Mniko
      April 11, 2021 at 12:27 pm

      Kafanya kazi nzuri

      Reply
  • Anonymous
    Anonymous
    May 3, 2021 at 10:45 am

    Samahani lkn hiyo picha sio ya kimeo,, kimeo kipo nyuma ya ulimi km unaelekea kwenye koo

    Reply
  • Kanyika
    Kanyika
    August 22, 2021 at 6:17 am

    Asante Sana doctor

    Reply
    • Dr.Mniko
      Dr.Mniko
      December 24, 2021 at 10:28 am

      Karibu

      Reply
  • Hafidhi
    Hafidhi
    November 1, 2021 at 12:19 pm

    Good job doc Joh

    Reply
    • Dr.Mniko
      Dr.Mniko
      November 13, 2021 at 12:20 pm

      Asante kwa mrejesho

      Reply
  • meshack emmanuel
    meshack emmanuel
    November 14, 2021 at 2:08 pm

    ningependa kujua hospitali gani zko na dawa

    Reply
    • Dr.Mniko
      Dr.Mniko
      December 24, 2021 at 10:19 am

      Dawa gani?

      Reply
  • Mansour wazir
    Mansour wazir
    April 7, 2022 at 6:24 pm

    Dokta mm samhaan mm nahisi dalili zote nnazo ila nliwahi kufanywa operation ila hli bado naona haijakaa sawa mpaka leo

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      April 12, 2022 at 6:31 pm

      pole sana, kma unaona unazo dalili , ni vizuri kumwona daktari akuchunguze na akibidi kuandaa mpango wa matibabu pamoja nae

      Reply
  • Jack
    Jack
    April 23, 2022 at 8:12 am

    Doctor mm nmegundua kilimi changu kuwa kimerefuka sanaa na shingon km kitu kimekwama n saut imeanza kubadilika natarajia j3 niende hospital na leo ndo nmekigundua yn mpk nmeogopa sanaa kimenikosesha amn vp nkiwa nasubr kwend hospital kunadawa yyt nawez tumia au njia nyingn yyt ambayo naweza tumia nikiwa nyumbn ili kipungue maan kinanikera shingon

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      May 10, 2022 at 1:15 am

      hapana

      ni vzuri kwenda kwa daktari kama una wasiwasi ili akuchunguze. ni uamuzi mzuri kwenda kwa daktari

      Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *