Maelezo ya jumla
Kuvuja damu sana ni jambo linalomwogopesha mwathirika na mtu anayemsaidia. Mara nyingi hali ya kuvuja damu hutokana na jeraha kubwa kwa vile kuchomwa kisu, kupigwa kwa nguvu au kukatwa sana. Lengo kuu ni kuzuia damu kuvuja na kuendelea kufuatilia hali ya mwathirika kwa ukaribu. Kama kiasi kikubwa sana cha damu kitapotea inaweza kuwa Hatari na hata kuhatarisha maisha.
Mambo unanyoweza kufanya wewe mwenyewe baada ya kuvuja damu sana
Wakati ukiendelea kusubiri msaada wa kitabibu au kujiandaa kumpeleka mwathirika kwenye kituo cha afya, kipaumbele chako ni kutambua eneo damu inapotokea na kuizuia isiendelee kutoka. Baada ya kufanya hilo unatakiwa kufunga eneo la jeraha kwa kutumia kitambaa safi ili kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi. hakikisha kuwa kitambaa au ”bandage” uliyoifunga haizuii damu kupita.
- Hakikisha unaomba msaada. Vaa glavu kama zipo au osha mikono vizuri. Funga au weka shinikizo kwenye eneo la jeraha kwa kutumia kitambaa safi ili kuzia damu kutoka. Nyanyua eneo lililoumia juu kidogo ya usaa wa moyo ili kupunguza kiasi cha damu kinachofikia huko. Kama kuna kitu kimebakia kwenye jeraha; mfano kisu, usikitoe; Bonyeza kutoka kila pande ili kujaribu kukutanisha ncha za jeraha na kupunguza kuvuja damu.
- Msaaidie mwathirika ili alale chini, hakikisha eneo lenye jeraha linaendelea kubakia juu ya usawa wa moyo. Endelea kushikilia na kuweka shinikizo kwenye eneo la jeraha kwa mpaka dakika 10
- Baada ya kuona kuvuja damu kumeanza kupungua, funika eneo la jeraha kwa kutumia ‘’gauze’’ na kufunga kwa kutumia ‘’bandage’’ au unaweza kufunika na kufunga kwa kutumia kitambaa safi. Hakikisha kuwa haujakaza sana kitambaa au bandage ukazuia damu kupita.
-
- ANGALIZO: Kuwa makini usifunge sana mpaka ukaziba mishipa ya damu ‘’touniquet’’. Kama kuna kitu kimebakia kwenye jeraha; kwa mfano kisu, weka ”gauze” au kitambaa kwa makini kukizunguka huku ukihakikisha haukisukumi kwenda ndani zaidi.
- Kagua kama damu inapita kuelekea upande wa pili wa jeraha kila baada ya dakika 10. Bonyeza juu ya kucha au ngozi ya upande wa pili mpaka rangi ififie, na kisha achia. Kama rangi ya kawaida ya wekundu haitarudi, au kama itarudi polepole, hii inamaanisha umekaza sana kitambaa au ”bandage” na damu haipiti vizuri. Ilegeze kidogo, ili kuruhusu damu kupita.
- Kama kuvuja damu kutaendelea, ongeza vitambaa zaidi juu ya ile ya kwanza. Kama damu itaendea kuchuja na kuvuja kupita vitambaa vya kwanza na hivi vya pili, viondoe vyote ili uweke vipya vizuri. Bana vizuri, hasa eneo damu inapotokea.
- Kama unaweza, fuatilia na rekodi kiwango cha upumuaji , kiwango cha mapigo ya moyo na kama anajitambua. Angalia kama kuna dalili za kupata mshtuko unaotokana na kupoteza damu nyingi sana na kama ikibidi nyanyua miguu yake pia ili iwe juu kidogo ya usawa wa moyo. Kama akipoteza fahamu , jiandae pia kufanya CPR
Angalia pia: kutokwa damu nyingi
Angalia pia: Nini cha kufanya mgonjwa akipoteza fahamu
Angalia pia: Angalia hapa jinsi ya kufanya CPR
- MAKALA TAJWA HAPO JUU ZINAADALIWA, RUDI TENA BAADA YA SIKU 2 KUJIFUNZA NASI, ASANTE