Maelezo ya jumla

Kuwashwa (itching) ni hali ya kuhisi mchonyoto unaokera kwenye ngozi anaokufanya utamani kukuna sehemu ilioathiriwa. Unaweza kuwashwa sehemu fulani ya mwili pekee au mwili mzima.

Kuwashwa husababishwa na nini?

Kuna sababu nyingi za kuwashwa, ikiwa ni pamoja na:

  • Kuzeeka kwa ngozi
  • Kuvimba kwa ngozi kunakosababishwa na mzio –atopic dermatitis
  • Kuvimba kwa ngozi kunakosababishwa na kugusa vitu vinavyosumbua na kuwasha ngozi (Kugusa sumu ya mti wa mwaloni au mwefeu)-contact dermatitis
  • Kugusa vitu vinavyoudhi au kuunguza ngozi (kama vile sabuni, kemikali, au pamba)
  • Ngozi kavu
  • Ugonjwa wa mabaka ngozini- hives
  • Kuumwa na wadudu
  • Vimelea kama vile minyoo, chawa wa mwili, chawa wa kichwa, au chawa wa mavuzi
  • Magonjwa ya ngozi kama pityriasis rosea au psoriasis
  • Upele
  • Kuunguzwa na mwanga wa jua
  • Maambukizi ya ngozi kama vile kuvimba kwa vinyweleo (folliculitis) au maambukizi yanayosababisha malengelenge (impetigo)

Kuwashwa mwili mzima kunaweza kusababishwa na:

  • Athari inayotokana na mzio (allergic reaction)
  • Maambukizi ya utotoni (kama vile tetekuwanga (chickenpox) au surua (measles))
  • Homa ya manjano (inayoashiriwa na ini kuvimba)- hepatitis
  • Upungufu wa damu (anemia) unaosababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini
  • Ugonjwa wa figo
  • Ugonjwa wa ini unaosababisha manjano
  • Ujauzito
  • Matokeo mabaya ya dawa na vitu kama vile antibiotiki (penicillin, sulfonamides), dhahabu, griseofulvin, isoniazid, opiates, phenothiazines, au vitamini A

Utambuzi

Daktari au muuguzi atakuchunguza na kuuliza maswali kadhaa kuhusu historia yako ya kimatibabu na dalili.
Unaweza kuulizwa maswali yafuatayo:

  • Umekuwa ukiwashwa kwa muda gani sasa?
  • Je! Unawashwa muda wote?
  • Je, kwuwashwa kunaongezeka makali au kuenea?
  • We unadhani ni nini kinasababisha unawashwa?
  • Je! Umeshawahi kuwashwa kwa namna hii huko nyuma? Ni nini kilichosababisha uwashwe kipindi hicho?
  • Je! Umekutana na kitu chochote kinachoweza kusababisha kuwashwa ngozi hivi karibuni?
  • Je! Una mzio na kitu chochote au uko-sensitive na kitu fulani?
  • Je, unatumia dawa gani?
  • Je! Umeanza kutumia bidhaa yoyote mpya hivi karibuni? Ni ipi?
  • Je! Umetumia sabuni mpya, kitambaa , marashi, manukato, au kemikali?
  • Je! Ulikuwa karibu na wanyama?
  • Je, umekula samakigamba (shellfish) au njugu/karanga hivi karibuni?
  • Je! Umeumwa na mdudu/wadudu hivi karibuni?
  • Je, unapaka losheni kwenye ngozi yako?
  • Je, umekaa kwa muda mrefu juani hivi karibuni?
  • Je! Unawashwa sehemu gani ya mwili wako?
  • Je, Unawashwa mwili mzima?
  • Je, unawashwa eneo gani la mwili? Ni eneo lipi?
  • Je! Sehemu ya ngozi inayowasha inaonekanaje?
  • Je, kuna upele? Ikiwa ndivyo, je, kuna malengelenge, magamba au ukurutu?
  • Je, unatibiwa ugonjwa au hali nyingine yoyote?
  • Je, Una dalili nyingine zozote?

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone daktari au muuguzi kama unawashwa na:

  • Una dalili nyingine zisizoeleweka
  • Makali ya muwasho yanaongezeka
  • Muwasho hauishi
  • Hakuna sababu ya dhahiri ya kuwepo huo muwasho

Mara nyingi mgonjwa anaweza kutathmini na kutambua ni nini kinachosababisha muwasho bila msaada wa daktari. Jaribu kutafuta sababu inayoweza kusababisha muwasho ukiwa nyumbani.
Wakati mwingine ni rahisi sana kwa mzazi kugundua sababu ya kuwashwa mtoto. Kuangalia kwa karibu ngozi kutakusaidia kutambua kama umeumwa na mdudu, upele, ukavu wa ngozi, au  ukurutu. Mara nyingi sababu ya kuwashwa iko wazi na dhahiri, kama vile kuumwa na mbu.
Hakikisha unamwona daktari mapema iwezekanavyo kwa uchunguzi, kama haujui sababu ya muwasho na unarudi mara kwa mara , kama unawashwa mwili mzima ,au una mabaka mwilini kila mara. Kuwashwa mwili kusiko na sababu inayojulikana kunaweza kuwa dalili ya ugonjwa hatari.

Uchaguzi wa matibabu kwa tatizo la kuwashwa

Kama muwasho ni mkali sana au unadumu kwa muda mrefu, ni muhimu kuonana na mtoa huduma wa afya kwa ajili ya utambuzi na matibabu.
Wakati huo huo, unaweza kuchukua hatua kadhaa ili kusaidia kukabiliana na muwasho:

  • Epuka kukuna au kusugua eneo linalowasha.
  • Hakikisha kucha zako ni fupi ili kuepuka kuchuna ngozi unapojikuna.
  • Vaa nguo za kuzuia baridi au mwanga, na vaa nguo zisizobana unapolala
  • Epuka kuvaa nguo zinazokwaruza kwaruza, hasa pamba, katika eneo lenye muwasho.
  • Oga kwa kutumia maji ya vuguvugu na sabuni kidogo.
  • Jipake losheni kulainisha na kupunguza ukavu wa ngozi
  • Ukavu wa ngozi ni chanzo kikubwa cha muwasho
  • Kama eneo linawasha sana unaweza kuweka kitambaa chenye barafu au ubaridi.
  • Epuka kukaa sana karibu na moto au joto kali.
  • Fanya shughuli nyingi mchana ili usiufikirie muwasho na kukuchosha sana ili ulale vizuri usiku
  • Unaweza kujaribu kutumia dawa zinazouzwa duka la dawa kama vile antihistamines mfano diphenhydramine, lakini uwe makini na madhara yanayoweza kutokana na dawa mfano usingizi.
  • Jaribu cream ya hydrocortisone kwenye sehemu zinazowasha .

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/003217.htm

Shares:
30 Comments
  • Samson Andrew
    Samson Andrew
    January 22, 2021 at 9:41 am

    Mm nina mwasho kichwani kwwnye kisogo, kwenye utosi hapo nywele zinapoanzia kwenye kidevu na kwenye pua pia kiunoni nizaidi ya mwaka sasa vjui nitumie dawa gani.nikijikuna vinatoka vpele vidogo vidogo vinatoa majmaji ambayo baada ua mda yanakauka kama utomvu fulani kama mchanga naombeni ushauri wenu

    Reply
    • Dr.Mniko
      Dr.Mniko
      January 23, 2021 at 2:53 am

      Habari Samson
      Nimejaribu kuelewa Swali lako lakini nimeshindwa, kwa hiyo sitaweza kukupatia jibu
      Tafadhali kama utaweza, tuandikie tena kwa kirefu jinsi unavyogonjeka
      ■Itapendeza kama utauliza swali kupitia ukurasa wetu wa mijadala ili tulijadili swala lako kwa pamoja na wataalamu wengine

      Reply
    • Abraham Tesha
      Abraham Tesha
      March 26, 2021 at 10:54 pm

      Kila napomaliza kuoga uwa na washwa mwili mzima ningependa fahamu inatokana na nini…?

      Reply
      • Dr.Mniko
        Dr.Mniko
        March 31, 2021 at 6:50 pm

        Pole sana
        Kwanza inabidi kujiangalia kama unavimba baada ya kuoga, kuna baadhi ya bidhaa za kuogea zinaweza kusababisha mzio kwa baadhi ya watu, kama ukiogea aina fulani ya sabuni na mwasho ukazidi basi badili
        Sababu kubwa ya tatizo hili ni ukavu wa ngozi, ngozi inapokuwa imekauka sana hasa baada ya kuoga, inawasha
        Ukioga maji ya moto na kutumia sabuni, unaondoa mafuta mengi kwenye ngozi na kuiacha ikiwa kavu kabisa, kwa watu ambao ngozi yao ni senstive wanawashwa
        Mambo ya kufanya
        ■ Usijifute maji kwa taulo unapojikausha, ni vizuri kuji peti peti badala ya kujifuta ili unyevu ubakie kwenye ngozi
        ■ Paka mafuta, lotion au moisturizer mara tu baada ya kuoga ili kuufungia huo unyevunyevu ndani ya ngozi yako
        ■ Epuka kuoga maji ya moto kama unaweza, maji ya ngizi yanaondoa kwa kiasi kikubwa mafuta kwenye ngozi na kuiacha ikiwa kavu sana
        Asante na karibu tena

        Reply
  • Hafsa Alifa
    Hafsa Alifa
    February 7, 2021 at 1:13 pm

    Nawashwaa usoniii nikiwaaa panavimbaa na sehem mbalimbali ya mwilii zaman sikuawah washwaa kabisaa na sijuii tatizoo nn mpakaa sasa

    Reply
    • Dr.Mniko
      Dr.Mniko
      February 24, 2021 at 12:46 pm

      Ooh pole sana , mara nyingi mwasho wa aina hiyo ambao haukuwepo zamani, unatokana na mzio kwa kitu kipya ulichoanza kutumia
      Angalia kama kuna kipodozi kipya ulichoanza kutumia au ondoa vipodozi vyote na mafuta anza kutumia kimoja kimoja ili uone ni kipi kinaleta shida

      Reply
  • Ahazi Mwaikambo
    Ahazi Mwaikambo
    February 24, 2021 at 1:34 pm

    Kuna Kaka angu muda wote anashinda anajikuna tu mwili mzima inaonesha Kama una ukurutu kutokana na kujikuna tumeshindwa kujua chanzo Ni Nini na tatizo litatibika vipi
    Naomba msaada wako Dr

    Reply
  • Antony
    Antony
    March 7, 2021 at 11:56 pm

    Habar Dr mi nawashwa najikuna sana mpaka vipere vinatokea usoni,kidevu,kiuno,kwenye vidole vya mkono mguuni mpaka kidonda kinatokea tena huwa nawashwa haswa saa 12jion mpaka ntakapo lala naomba msaada wKo

    Reply
  • ester mkoma
    ester mkoma
    March 23, 2021 at 12:46 am

    mimi nawashwa mwili mzima navimba kama vinundunundu tatizo lina mda mrefu

    Reply
  • Ivi kuna allergy ambayo inasababisha kutokwa na makovu mwilini yaani mfano kametokea kaupele kadogo mwilini afu ukawa unajikuna baadae linatokea kovu kubwa naomba kujua dawa yake
    Ivi kuna allergy ambayo inasababisha kutokwa na makovu mwilini yaani mfano kametokea kaupele kadogo mwilini afu ukawa unajikuna baadae linatokea kovu kubwa naomba kujua dawa yake
    May 19, 2021 at 5:16 am

    Naomba unisaidie kujua tatizo na suluhisho la mtu anaetokwa na makovu baada ya kuugua kaupele na badae kukakuna na kakaleteleza kovu mwilini hiyo inasababishwa na nn na huyo mtu anaweza akatumia dawa gani kuondokana na hilo tatizo

    Reply
  • Claud
    Claud
    May 21, 2021 at 6:36 am

    Samahani mimi napatwa shida sana ya kuwashwa hasa usiku mida nikitaka kulala sehemu za mapaja nmejaribu kutumia aina kidogo lakin kilakuwa kinapoza vmeisha muwasho bado upo palepale na hasa mda wa usiku nikitaka kulala tu sehemu za mapaja na muwasho wale ni ule nikijukuna natamani zaid kujikuna naomba msaada kujua shida ni nini

    Reply
    • Dr.Mniko
      Dr.Mniko
      May 23, 2021 at 11:01 am

      kama ukiweza, naomba uniandikie katika namba iliyopo hapo chini, ili tuzungumze vizuri na kwa kirefu ili kutafuta sababu ni nini?

      Reply
  • Abubakari iddi
    Abubakari iddi
    August 13, 2021 at 2:25 pm

    Mimi nawashwa pindi tu jua linaponichoma na pia nikipata msisimko tatizo ni nini?

    Reply
  • Anonymous
    Anonymous
    November 12, 2021 at 12:57 pm

    Mimi nawasha tuu mwili lakini sioni chochote

    Reply
    • Dr.Mniko
      Dr.Mniko
      November 13, 2021 at 12:15 pm

      Polee,ni vizuri kuonana na daktari achukue maelezo na vipimo akusaidie. pole sana

      Reply
      • Valeriani Fidelisi
        Valeriani Fidelisi
        October 17, 2022 at 6:24 pm

        Kujamiana kunaweza kupelekea muwasho wa mwili au nimehisi vibaya

        Reply
  • Mwashala
    Mwashala
    January 21, 2022 at 5:26 am

    Mimi nawashwa sehem za Siri nahisi Kuna wadudu doctor kabisa wadudu wapo nimejaribu kunyoa zoote lakin bado muwasho upo palepale sijui tatizo nini

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      January 30, 2022 at 9:17 pm

      Pole sana, zipo sababu nyingi sana za mwasho sehemu za siri. ni vizuri kumwona daktari aangalie tatizo ni nini akusaidie. Usiendelee kuvumilia

      Reply
  • Sigera
    Sigera
    March 12, 2022 at 6:52 am

    Na sumburiwa na ttzo lakuwashwa. Na ngozi nimejaribu kutmia dawa lkin naona bado

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      March 27, 2022 at 9:10 pm

      Ili kutibu mwasho ni vizuri kutambua kwanza sababu ni nini?

      kama unashindwa kutambua ni vizuri ukaongea na daktari

      Reply
  • Najat
    Najat
    April 14, 2022 at 9:53 pm

    Doc mim nawshwa kam week ya 3 natmiaa dawa nkiaacha vinarudi nmeend hsptl napew dawa lakn nado na nkijikuna oanafnya kam vipele yaan uvimbe af nakua mwekundu jaman msaaada nimechoka na hii hali

    Reply
  • Mseti kebwasi
    Mseti kebwasi
    June 13, 2022 at 7:57 pm

    Nina wiki 3 nawashwa mwili kwa kuruka ruka maeneo ya mwili,hasa nikiwa sehemu yenye joto naomba msaada

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      June 18, 2022 at 2:30 pm

      Ongea na daktari wetu, kupitia nmba iliyopo kwenye tovuti, utahitajika kutoa maelezo zaidi

      Reply
  • Emmanuel Alex
    July 6, 2022 at 8:53 pm

    Tatizo lako kama langu na kwa watu wengi pia limewakuta hili, kama mm na mwanangu wote tunajikuna balaa hasa usiku

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      July 11, 2022 at 12:50 pm

      Pole sana, kama ulivyosoma katika makala hii, kuwashwa kunasababu nyingi, na daktari anahitaji kuuliza maswali ya mwongozo kwa mgonjwa ili kutambua sababu ni nini kabla ya kutoa tiba. ni vyema kuongea na daktari wetu ili kupata ushauri unaokufaa wewe, ili kupta nafuuu. pole sana kwako na familia yako

      Reply
  • deusmusicenjoy@gmail.com
    deusmusicenjoy@gmail.com
    October 1, 2022 at 1:45 pm

    Kujikuna kila mda mtoto wa miaka 3 tatizo ni nini

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      October 2, 2022 at 12:22 pm

      Sababu zinaweza kuwa nyingi, kama umesomaakala hii unaweza kuwa na idea ni nini sababu

      Jaribu kushughulika na mambo ya kawaida yanayoweza kusababisha tatizo, ikishindikana mwone daktari

      Kama yuko kwenye jua mtoe hapo, kama kuna nyasi mtoe hapo, kama amevaa nguo mpya mbadilishie, kama umeenda ugenini kagua malazi anayolalia yanawza kuwa na wadudu, kama kuna upepo mkali mpake mafuta mwilini au jifukize kwa maji ili kuweka unyevu kwenye ngozi

      Unaweza pia kununua dawa za kupooza mwasho kama cetrizine au dawa za kupaka, ila ni vzr kutafuta sababu ni nin

      Reply
  • Bethsheba
    Bethsheba
    October 10, 2022 at 10:51 pm

    Hua ninawashwa nyayo ya mguu wa kushoto nimiaka mi2 sasa sijui chanzo ni nini naomba msaada au ushauli

    Reply
  • Sarah
    Sarah
    November 5, 2022 at 12:45 pm

    Naomba number yako ya simu nikupigie ili nikueleze tatizo langu

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      November 5, 2022 at 7:38 pm

      0759078960

      Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *