Maelezo ya jumla
Kuwashwa macho – macho yanayowasha mara nyingi utakuta ni mekundu, yanawasha na unahisi kama yanaungua hivi. Unahisi kujikuna kila mara. Kitu chochote kinachosumbua macho, kama vile hali ya hewa, vumbi au maambukizi, kinaweza kusababisha kuwashwa macho. Mzio unaosababishwa na chemvua za mimea au mjibizo mbaya unaotokana na ”chlorine” inayowekwa kwenye mabwawa ya kuogelea, vipodozi, au madawa ya macho yanaweza kusababisha mwasho pia. Wakati mwingine utakuta ni ncha za kope tu ndizo zilizoathiriwa. Hali hii inaitwa ”blepharitis”, inasababisha kidonda ambacho hutoa majimaji yanayogandia kwenye nywele za kope. ”Blepharitis” huwa inawapata zaidi watu wenye matatizo ya ngozi au mba. Unaweza pia kuwashwa macho kama utakuwa umevaa lenzi machoni (contact lens)
Mwone daktari kama
Ni vizuri kumwona daktari ili atambue kwa nini , kama una tatizo la kuwashwa macho
Unachoweza kufanya mwenyewe nyumbani ukiwa na tatizo la kuwashwa macho
Hatua zifuatazo zinaweza kusaidia kuleta nafuu au zinaweza kutumika pamoja na matibabu utakayokuwa umepewa na daktari
- Epuka kufikicha au kusugua macho, unaweza kusababisha hali ikawa mbaya zaidi au kusambaza maambukizi
- Kama una mzio na unasababisha kuwashwa macho, chukua barafu, iweke kwenye kitambaa na kishaiweke kwenye jicho. Unaweza kuloweka kitambaa kwenye maji ya baridi, ukakamua kisha ukakilaza kwenye jicho au macho kwa dakika kadhaa. Uanaweza kurudia mara nyingi kadri ianavyowezekana
- Unaweza kutumia machozi ya bandia ili kutuliza mwasho au usumbufu kwenye macho unaosababishwa na moshi au vumbi. Machozi ya bandia (artificial tear drops & gels)) ni kimiminika ambacho unaweza kukinunua kwenye duka la dawa ambacho huwa kina ”hydroxylpropyl methylcellulose” ambayo inasaidia kuongeza unyevu kwenye macho na kupunguza mwasho. Usivae contact lens unapokuwa unatumia dawa hizi.
- Jaribu kutambua kama mwasho umesababishwa na sabuni, vipodozi vya uso au nywele, kisha ACHA kuvitumia, rudisha kimoja kimoja kuona kama tatizo litajirudia. Tupa au acha kutumia vipodozi vya macho vya zamani: usibaki na mascara kwa zaidi ya miezi 6
- Kama unaona kope zimevimba au unaona kuna uchafu umegandia kwenye nywele za kope, unaweza kujitibu kwa kufuata hatua zifuatazo:
- Kama daktari wako hajakukataza, unaweza kufauata hatua zifuatazo kudhibiti blepharitis:
- Lowanisha kitambaa kisafi kwenye maji ya uvuguvugu, kikamue, kisha kiweke kwa kukandamiza kidogo kwenye kope ya jicho lako likiwa limefungwa kwa angalau dakika 5. Hii inasababisha matongotongo na uchafu uliogandia kulowana na kuachia
- Unaweza kuchanganya maji na ”baby shampoo” kwa usawa. Kisha chovya pamba kwenye huo mchanganyiko, ikamue na kisha izungishe kutoka kona ya upande mmoja mpaka mwingine wa kope ili kuondoa uchafu na matongotongo. Baada ya hapo, suuza jicho kwa kutumia maji safi na kisha jifute kwa kutumia taulo mpya
- Rudia kwa kutumia pamba nyingine mpya kwa jicho la pili
- Safisha macho kwa kutumia kitambaa kisafi kila asubuhi na kila unapolala mpaka utakapoona kuna nafuu au kumepona na kisha mara moja kwa siku ili kuzuia hali hii isijirudie
- Kama daktari wako hajakukataza, unaweza kufauata hatua zifuatazo kudhibiti blepharitis:
Mwone daktari kama una tatizo la kuwashwa macho
Panga kuonana na daktari kama:
- Dalili zako zitaendelea kwa zaidi ya masaa 48