Maelezo ya jumla

Kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa (mkundu), ni hali inayoleta karaha sana na inaweza kuaibisha kwa sababu unapata hamu kubwa ya kutaka kujikuna. Ngozi inayozunguka mkundu inaweza kuwa nyekundu na inayouma, na inaweza kuvuja damu na hata kupata maambukizi kama utapakuna sana. Kuwashwa mara nyingi huwa kunazidi baada ya kujisaidia na usiku. Mtu anaweza kuwashwa mkundu kwa sababu ya harara inayotokana na bidhaa za kujitawadhia au marashi anayotumia, jasho, unyevu unyezi au vipande vya mavi vinavyobakia kwenye ngozi kuzunguka eneo la kutolea haja kubwa. Watu ambao wana uzito mkubwa, wanaotokwa jasho jingi sana au wanaovaa chupi zinazobana sana wako kwenye hatari zaidi ya kuwashwa. Wakati mwingine aina fulani za vyakula, zinaweza kuchangia tatizo hili. Bawasiri na minyoo inayoitwa ‘’pinworm’’ ni sababu pia za tatizo hili.

Kama una tatizo la kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

  • Unatokwa na damu kwenye eneo linalozunguka sehemu ya kutolea haja au kama kuna vitu kama kamasikamasi vinatoka huko
  • Una maumivu na/ au uvimbe mk*nduni au au eneo linalozuunguka mkundu

kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kama una tatizo la kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa

Tatizo la kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa, kwa kawaida linaweza kudhibitiwa kwa matibabu kadhaa nyumbani, matibabu haya yanaweza pia kuzuia tatizo hili lisijirudie

  • Jitahidi na epuka kujikuna. Kata kucha ziwe fupi na ukiweza vaa glavu wakati wa usiku ili usijikwaruze utakapojikuna ukiwa usingizini
  • Unaweza kutumia madawa yenye ‘’antihistamine’’ ili kupunguza kuwashwa na kukupatia usingizi. Madawa haya yanapatikana kama kidonge au dawa ya kunywa, zitumie ili zikusaidie ulale.
  • Safisha eneo la mkundu asubuhi na jioni kwa kutumia maji ya kawaida na kisha pakaushe vizuri. Hakikisha kuwa eneo limekausha vizuri. Unaweza kutumia ‘’hair dryer’’ kupakausha’
  • Unaweza kupaka mchanganyiko unaotumika kudhibiti bawasiri ‘’hemorrhoid preparation’’ ili kupunguza kuwashwa. Madawa haya yana ‘’phenylephrine’’ ambayo inasaidia kupunguza uvimbena mwasho unaosababishwa na bawasiri na ‘’hydrocortisone’’ ambayo inapunguza uvimbe. Usitumie madawa haya kwa zaidi ya siku 5-6.
  • Jisafishe vizuri kila baada ya kujisaidia. Kama kujisafisha haiwezekani kwa wakati huo, tumia kitambaa kilicholoweshwa au karatasi laini za chooni zilizolowanishwa kujisafisha. Tumia ‘’toilet paper’’ kujikausha vizuri ili kuondoa unyevu nyevu baada ya kukojoa.
  • Vaa kufuli/chupi zisizo bana zilizotengenezwa kwa pamba, na badili kila siku na ikibidi mara kadhaa kwa siku. Euka kuvaa suruali zinazobana au ‘’pantyhose. Ukiweka upindo wa kitambaa au tishu laini karibu na sehemu ya kutolea njia ya haja kubwa itanyonya na kuondoa unyevunyevu wote.
  • Jaribu kutafuta na kutambua aina za vyakula au vinywaji ambavyo vinaweza kuwa vinachangia kukusababishia tatizo hili la kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa. Vinywaji na vyakula kama vile bia, kahawa, nyanya na vyakula vyenye pilipili nyingi.

Kama una tatizo la kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

  • Kuwashwa hakujapungua baada ya wiki moja ya kufuata mbinu zilizoelekezwa hapo juu
  • Unaona kuna dalili nyingine zinaanza kujitokeza kwako au kama mwanafamilia mwingine amenza kupata shida kama yako

Vyanzo

https://www.healthline.com/health/itchy-anus

Shares:
14 Comments
  • Festo
    Festo
    September 10, 2021 at 11:30 pm

    itching anal what is causing

    Reply
  • Halima
    Halima
    December 5, 2021 at 5:16 pm

    Hi naomba kujua dawa zenye zitanisaidia sehemu yakutolea haha kubwa yaniuma nikitoka haja kubwa ilikuwa naomba usaidizi

    Reply
    • Dr.Mniko
      Dr.Mniko
      December 24, 2021 at 10:13 am

      Mara nyingi kama umepata kinyesi kigumu, unaweza kuhisi maumivu baada ya kujisaidia
      Maumivu haya huisha baada ya muda, ila yanaweza kukukera sana
      Kinyesi kuwa kigumu sana ni dalili kuwa hauli chakula chenye nyuzi nyuzi za kutosha, vyakula vilivyokobolewa ugali, wali, ngano vinachangia sana tatizo hili
      Jaribu kubadili utaratibu wako wa mlo, kula mapapai, ugali uliopikwa wa unga usiokobol3lewa n.k , mboga na magunda huongeza pia nyuzinyuzi na usisahau maji

      Reply
  • Aloyce Assey
    Aloyce Assey
    January 21, 2022 at 7:17 am

    Habari jamani,sehemu ya haja kubwa kuwasha kama ina chomachoma wakati wa kutembea tatizo linasababishwa na nini ?

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      January 30, 2022 at 9:16 pm

      Sababu zipo nyingi , kama mambo ya kufanya tuliyopendeeza hapa hayajakusaidia kupunguza dalili zako, mwone daktari tafadhali, atambue shida yako akusaidie

      Reply
  • Fedrick Yohana
    January 28, 2022 at 5:21 pm

    Mwili unatoa harufu hasa Zaid sehem yakutolea haja kubwa unatoa unyevu mwingi

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      January 30, 2022 at 9:15 pm

      Pole sana, kama njia tulizokuelekeza hapa hazijakusaidia ni vizur kumwona dakatari aangalie tatizo ni nini

      Reply
  • Mohamed Hamis
    March 10, 2022 at 11:04 am

    1: Ivi sehemu ya haja kubwa kuwasha na kutokwa na vitu kama kamasi inasabishwa na nini??
    2: Je ni njia gani kuepukana na hali hii??

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      March 27, 2022 at 9:12 pm

      Inategemea na sababu ni nini? zip[o sababu nyingi za kuwashwa sehemu ya haja kubwa. maambukizi, majeraha, majipu, uvimbe, saratani na mengine mengi. ni vizuri kutambua sababu ni nini na kisha uishughulikie

      mwone daktari kama unashindwa kujua sababu wewe mwenyewe

      Reply
  • Magreth joseph
    Magreth joseph
    April 5, 2022 at 5:21 am

    Habari naomba kujua sababu za kutokwa mshikaji kama makamasi sehemu ya haja kubwa tatizo itakuwa ni nini

    Reply
  • Lameck
    Lameck
    April 14, 2022 at 8:25 pm

    Darasa zuri sana. Hili Tatizo la bawa sili limekuwa shida sana tunapata mowasho isiyo ya kawaida hasa ukitoka kujisaidia yani tunaomba tuzidi kujua matibabu yake.

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      April 15, 2022 at 10:19 pm

      Karibu

      Reply
  • Baraka
    Baraka
    May 1, 2022 at 10:13 pm

    Kwahiyo wali sio mzuri p1 n tambi?

    Reply
  • Said kayoka
    Said kayoka
    July 11, 2022 at 12:25 am

    Habar Dr,mm hua nawashwa mara kwa mara eneo linalozunguk haja kubwa yaani mpk kero hiv husababishwa na nn haswa?

    Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *