Melezo ya jumla
Kuwashwa ukeni au eneo linalozunguka uke ni tatizo linaloleta karaha na kukera sana mchana na linaweza kusababisha usilale wakati wa usiku. Eneo la uke linaweza kuwa kavu, jekundu na kuvimba na unaweza kupata maumivu wakati wa kukojoa na wakati wa ngono. Hali ya kuwashwa huwa inazidi zaidi wakati wa joto. Kuwashwa mara nyingi hutokana na sabuni au perfume za chooni, lakini wakati mwingine inaweza kuwa kwa sababu ya maambukizi, matatizo ya ngozi au hata kutokujikausha vizuri baada ya kutoka chooni.
Kuwashwa ukeni – mwone daktari kama
Panga kumwona daktari kama:
- Kuna uchafu usio wa kawaida unatoka ukeni au kama unapata maumivu wakati wa kukojoa
- Unawashwa mahala pengine pia na/au una tatizo la mzio au kuvimba ngozi kunakotokana na ugonjwa wa ‘’psoriasis’’
- Unapungua uzito bila sababu ya msingi na /au kama unakunywa au kukojoa mara nyingi zaidi kuliko kawaida
- Una alama au vidoti vyeusi kwenye nywele za sehemu za siri (mavuzi)
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe
Unaweza kujaribu kufanya mambo yafuatayo ili kupunguza karaha ya kuwashwa ukeni na kupunguza uvimbe
- Weka barafu sehemu inayowasha. Chukua barafu iliyo kwenye kifuko na uifunge kwenye kitambaa au taulo lililoloweshwa au liliodumbukizwa kwenye maji ya barafu na uiweke sehemu inayowasha mara nyingi unavyoweza. Unaweza pia kukalia maji ya baridi au ya uvuguvugu kwa muda wa dakika 10-15.
- Unaweza pia kutumia ‘’moisturizer’’ ili kupooza eneo lililovimba. ‘’Water based moisturizers’’ zinaweza kupoza ngozi iliyosumbuliwa au unaweza kupaka ‘’gel’’ iliyotengenezwa na ‘’Aloe-vera’’
- Unaweza kutumia madawa aina ya ‘’antihistamine’’ kukusaidia upate usingizi. Dawa hizi zinapunguza mwasho na kuongeza usingizi, zitumie wakati wa kulala.
- Unaweza kutumia kilainishi kama unahisi uke umekauka na unapata maumivu wakati wa kushiriki ngono. Kutumia kilainishi kunapunguza karaha, weka kilainishi muda mfupi tu kabla ya kushiriki ngono.
- Jitahidi na epuka kujikuna. Ukiwa umelala vaa gauni la kulalia bila kuvaa chupi ili hewa iingie sehemu za siri.
Kuwashwa ukeni – kuzuia
Unaweza kuepuka kuwashwa sehemu za siri kwa kuepuka visababishi na kuwa makini wakati wa usafi binafsi
- Usitumie sabani zenye marashi, ”bubble baths” na marashi ya kuweka ukeni. Nawa sehemu za siri mara moja au mara mbili kwa siku kwa kutumia maji tu au kwa kutumia sabuni ya kawaida na maji. Jipeti kwa taulo ili kujikausha vizuri.
- Jifute kutoka mbele kwenda nyuma baada ya kujisaidia haja kubwa na jikaushe kikamilifu baada ya kukojoa. Tumia tishu laini za chooni na zisizo na rashi.
- Unaweza kumwomba mwenzi wako atumie kondomu ambazo hazijatengenezwa kwa latex kama unadhani ndizo zinazokusababishaia shida. Usitumie bidhaa za hedhi/ pad zilizoweka marashi.
- Vaa chupi ya pamba inayokuacha huru na ibadili kila siku. Usitumie jeans inayobana sana.
Tafuta usaidizi wa daktari
Panga kumwona daktari kama:
- Harara au kuwashwa kutaendelea kuwepo zaidi ya siku 3-4
Jaman me nawashwa ii ck y 2 nawashwa tu sijuwa shda nn et
pole sana, ni vzir kuangalia unawashwa kwa sababu gani. ila kwa kupunguza mwasho zipo dawa za kupaka na kumea nunua moja wapo itakusaidia. kama mwasho unaendelea mwone daktari