Kuziba kwa utumbo ni nini?
Kuziba kwa utumbo ni hali ya kuwepo kizingiti kinachozibba utumbo mwembamba aua utumbo mpana na kuzuia chakula kupita
Ni nini sababu za kuziba kwa utumbo?
Moja ya matatizo hatari zaidi yanayoweza kusababishwa na kuziba kwa utumbo ni kukatwa/kushindwa kwa damu kufika kwenye mfumo wa kumeng’enya chakula. Kwa sababu shemu hiyo inashindwa kupata damu, inaweza kufa na kuanza kuoza. Kama hili litatokea, shinikizo linaweza kuwa kubwa sana na kusababisha kupasuka kwa utumbo, kunaweza kusababisha kusambaa kwa vimelea kwenye mwili na kwenye damu. Aina hii ya maambukizi inaweza kutishia maisha.
Ni zipi dalili za kuziba kwa utumbo?
Moja ya dalili zinazowapata watu wengi ni kushindwa kujamba au kushindwa kupata kinyesi, na kichefuchefu, kutapika, tumbo kujaa/kufura, tumbo kuvimba na maumivu ya tumbo. Maumivu ya mtu mwenye tatizo la kuziba kwa utumbo yanakuja na kuondoka (kama vile mawimbi, na baadae yanatulia , kisha yanarudi tena)
Ni nani yuko kwenye hatari ya kupata tatizo la kuziba kwa utumbo?
Watu ambao wamewahi kufanyiwa upasuaji wa tumbo wako kwenye hatari kwa sababu ya makovu yanayobakia baada ya upasuaji. Mwambie daktari kama umewahi kuwa na ngiri. Kuziba kwa utumbo kunaweza pia kusababishwa na uvimbe/kansa, kwa hiyo dakatari anaweza kupendekeza kufanyiwa vipimo ili kujihakikishia.
Nifanye nini kama ninadhani nina shida hii
Mpigie simu daktari au nenda kamwone haraka
Daktari atafanya nini?
Daktari atakuchunguza na kukuuliza maswali kuhusu historia yako ya kimatibabu, hii ni pamoja na upasuaji uliowahi kufanyiwa. Anaweza kuagiza ufanyiwe kipimo cha eksirei au computed tomography (CT) scan.
Kuziba kwa utumbo mara nyingi kunatibiwa kwa kuingiza mrija kupitia kwenye pua mpaka kwenye tumbo. Ni muhimu kupata maji ya kutosha, kwa hiyo utaongezewa maji kupitia kwenye mishipa. Unaweza kuhitajika kuangaliwa na daktari bingwa wa upasuaji ili kuangalia kama unahitaji upasuaji ili kufungua sehemu ya tumbo iliyoziba.
Nina kila dalili za hii shida