Maelezo ya jumla

Ajali zote zinaweza kuua, kusababisha ulemavu na uharibifu wa mali, hivyo basi kuleta umasikini kwa watu na Taifa kwa ujumla.

Takimwi za ajali

Katika kipindi cha Novemba 2011 na Desemba 2012, jumla ya majeruhi 9,311 wa ajali mbalimbali walionwa katika hospitali za MOI, Morogoro, Mtwara, Kigoma, Musoma na Korogwe (sawa na jeruhi mmoja kila saa moja). Ajali za barabarani ziliongoza kwa asilimia 47.5%, zikifuatiwa na kuanguka (asilimia 27.9%), na ugomvi au kupigwa (asilimia 17.4%). Asilimia 66.7% ya majeruhi wote walilazwa hospitali, na asilimia 2.4% walikufa mapokezi kutokana na kuumia vibaya au kuchelewa kufika hospitali.

Jinsi ya kuzuia ajali

Ajali za kuanguka

  • Watoto wawe na waangalizi muda wote nyumbani na michezoni
  • Hakikisha watoto wanacheza mahali salama na wanachezea vifaa vilivyo salama
  • Sakafu nyumbani isiachwe ikawa ya kuteleza sana
  • Hakikisha mwanga wa kutosha hasa kwenye ngazi
  • Vaa viatu visivyo na soli za kuteleza
  • Pima macho kama hayaoni vizuri, na kwa wasioona kabisa ni vizuri wawe na waangalizi

Ugomvi au kupigwa

  • Epuka kujihusisha kwenye ugomvi wa aina yoyote
  • Epuka ulevi wa aina yoyote (madawa, pombe nk), kwani unachangia ugomvi
  • Tuache kujichukulia sheria mkononi, kwa kuwapiga wahalifu.

Ajali za moto

  • Watoto wadogo wasiachwe bila uangalizi, kwani ni rahisi kuungua na maji ya moto, n.k
  • Kwa wagonjwa (mfano kifafa, wazee sana), wawe na waangalizi na wasikae karibu na moto
  • Wafanyakazi wa umeme zingatia sheria zote za usalama na tumia vifaa vya kuzuia ajali
  • Ulevi wa kupindukia unaweza kusababisha ajali ya moto

Wanyama au Nyoka

  • Kwa wanaokaa vijijini na waliozungukwa na vichaka kuwa mwangalifu na wanyama, nyoka na mamba mitoni
  • Epuka kutembea peke yako usiku wakati wa giza

Mazingira ya kazi

  • Kuvaa vitu vya kuzuia ajali kazini – miwani, viatu (boots)
  • Kuvaa mikanda ya kujifungia kwenye viti ndani ya gari
  • Kuhakikisha ya kuwa mazingira ya kucheza watoto ni salama.

 Ajali za barabarani

  • Usiendeshe gari bovu
  • Zingatia alama za barabarani hasa kutokuendesha kasi
  • Jifunge mkanda wa kiti
  • Vaa kofia ikiwa kwenye pikipiki
  • Usiendeshe gari ukiwa umekunywa pombe
  • Zima na usiinue simu ikiwa unaendesha.

Ajali zote zinaweza kuua, kusababisha ulemavu na uharibifu wa mali, hivyo basi kuleta umasikini kwa watu na Taifa kwa ujumla.

Vyanzo

National Bureau of Statistics (NBS) [Tanzania] and ICF Macro. 2011. Tanzania Demographic and Health Survey 2010. Dar es Salaam, Tanzania: NBS and ICF Macro.

https://medlineplus.gov/woundsandinjuries.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *