Maelezo ya jumla

Minyoo inaishi kwenye tumbo na husambazwa kupitia mchanga, mikono, na wakati mwengine kupitia chakula ambacho hakijapikwa au kusafishwa vizuri. Kwa watoto, maambukizi ya minyoo husababisha uchovu, kuumwa tumbo na kufura kitambi. Kwa watu wazima, uwezo wa kufanya kazi unapungua kwa sababu ya mdororo wa afya unaotokana na minyo kuzuia au kutumia virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini.

Minyoo ni nini?

Minyoo inaishi tumboni nainaweza kuzuia chakula na madini kufika katika sehemu za mwili zinazostahili. Kama mtoto ameambukizwa minyoo anaweza kujihisi uchovu, maumivu ya tumbo na kumfanya jisikie vibaya. Kwa watoto, maambukizi ya minyoo huzuia mtoto asikue vizuri na kusababisha asihudhurie shuleni na hatimaye kupata matokeo duni.  Sawa na ilivyo kwa watoto, watu wazima wanaweza kupata shida kufanya kazi zao vyema siku hadi siku. Kuna aina tatu ya maambukizi ya minyoo: hookworm, roundworm, and whipworm.

Minyoo huambukizwaje?

Minyoo hutaga mayai ambayo hutoka tumboni mwa mtu kupitia kinyesi na yanayweza kusababisha maambukizi kupitia kwenye ngozi, chakula na mikono ambayo haikusafishwa vizuri baada kugusa kinyesi chenye mayai.

  • Mayai ya minyoo aina ya Hookworm yanaweza kujiangua na kimelea anaweza kutoboa ngozi na kuingia ndani ya mwili wa mtu kama ataingia chooni bila kuvaa viatu.
  • Mayai ya minyoo aina ya Roundworm na whipworm hugandia kwenye mikono, na kama mtu atakula chakula bila kusafisha mikono vizuri, basi mayai hayo yataingia tumboni na kuanguliwa kutengeneza minyoo wengine wakubwa.

Tunawezaje kuzuia tatizo hili la minyoo?

Minyoo inaweza kuzuiwa kwa njia tofauti:

  • Kutumia choo kila mara
  • Kunawa mikono baada ya kutumia choo, kuogesha au kuosha mtoto.
  • Kuvaa viatu.
  • Kutumia dawa za minyoo angalau mara moja kila mwaka

Matumizi ya choo huzuia watu wengine kukanyaga kinyesi na hatimaye kuambukizwa minyoo aina ya hookworm, na pia hupunguza uwezekano wa mtu kushika kinyesi. Mayai ya baadhi ya minyoo yanaweza kubakia kwa muda mrefu katika mazingira, na inawezekana mtu akashika kinyesi bila kutambua kama hautatumia choo.

Kunawa mikono na sabuni baada ya kwenda chooni huangua mayai ya minyoo kutoka kwenye mikono endapo yataganda kwenye mikono na hivyo kuifanya mikono kuwa salama. Minyoo mingine huishi kwenye mchanga, kwa hivyo ni vizuri kunawa mikono baada ya kucheza na mchanga au kutoka shambani.

Kuvaa viatu pia huzuia maambukizi ya minyoo aina ya hookworm ambazo huishi kwenye mchanga. Minyoo hii inaweza kutoboa ngozi na kuingia ndani ya mwili na kisha kutambaa mpaka tumboni.

Kupokea matibabu mara moja kila mwaka huangamiza minyoo katika mwili na hatimaye kupunguza idadi ya Minyoo. Madawa haya ni salama na unahitaji tu tembe moja! Tembelea kituo chako cha afya upate matibabu.

Minyoo ya Echinococcus na jinsi ya kuizuia

Echinococcus ni aina nyingine ya Minyoo ambayo kwa kawaida haishi kwa binadamu, bali huishi kwa mbwa na ng’ombe, kondoo na mbuzi. Kwa kawaida, njia ya maambukizi huwa ni kati ya mbwa na wanyama wanaofugwa, wakiambukizwa kupitia nyama ya ng’ombe ama mbuzi.

Mbwa anakula nyama ya ng’ombe au mbuzi iliyoambukizwa na anapata minyoo inayotengeneza mayai, ambayo hutoka kwenye kinyesi na baadae kuliwa na ng’ombe au mbuzi wakati anapokula nyasi. Mayai yanapoingia kwenye tumbo la ng’ombe au mbuzi huangua na minyoo hawa huingia kwenye nyama ya ng’ombe au mbuzi na kukua.

Wakati mwengine, watu huambukizwa kwa kula kinyesi cha mbwa kwa bahati mbaya na hatimaye kusababisha ugonjwa wa hydatid. Hii hutokea kutokana na uchafu, mikono michafu ama kunywa maji kutoka kwenye kidimbwi kilichoachwa wazi na kuchafuliwa.

Ni vigumu sana kutibu ugonjwa huu. Kwa hiyo, ni bora kinga kuliko tiba. Njia za kuzuia maambukizi haya ni kama ifuatavyo:

  • Kunawa mikono kila mara kabla ya kugusa chakula
  • Kutibu maji yaliyochotwa kutoka kwenye kidimbwi kilichowachwa wazi kabla ya kunywa.

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaii kuhus shida hii.

Vyanzo

https://www.who.int/health-topics/soil-transmitted-helminthiases

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *