Macho makengeza ni nini?

Macho makengeza (amblyopia) ni hali ya kupoteza uwezo wa kuona katika jicho moja. Kwa watoto na watu wazima, ni hali inayosababisha matatizo ya uoni kwa watu wengi. Hali hii inatokea kunapokuwepo na mkanganyiko kati ya jicho na ubongo. Ubongo unashindwa kutambua picha zinazotumwa kutoka katika jicho moja, na kwa sababu hii, ubongo unajifunza kutegemea zaidi na zaidi picha kutoka katika jicho zuri pekee – na wakati huo, uoni wa jicho jingine unaendelea kupungua siku hadi siku. Hali hii inaitwa macho makengeza kwa sababu, jicho zuri linafanya kazi vizuri kuliko jicho jingine.

Ni nini kinasababisha macho makengeza?

Macho makengeza ni hali inayoanzia utotoni, na inasababisha matatizo ya uoni kwa watoto wengi. Karibu watoto 3 kati ya 100 huwa na tatizo hili. Habari njema ni kuwa, matibabu ya mapema yanaweza kurekebisha tatizo hili kabisa.

Katika visa vingi, madaktari hawajui sababu ya macho makengeza. Lakini wakati mwingine, tatizo jingine linalosababisha uoni hafifu linaweza kuchangia kutokea kwa hali hii.

Kwa kawaida ubongo unatumia picha kutoka katika macho yote mawili ili kuunda picha unayoiona kwenye ubongo. Lakini kama kuna shida yoyote inayosababisha picha moja kutoka katika jicho moja kuwa imefifia, ubongo unaanza kujifunza kuipotezea.  Ubongo unajifunza kutegemea zaidi picha kutoka katika jicho zuri linaloleta picha nzuri zaidi.

Macho makengeza yanaweza kutokea kama mtoto ana jicho moja linalojigeuza kuangalia upande mmoja au jicho moja lenye uoni hafifu kuliko jingine. Tatizo hili pia linaweza kusababishwa na kukua kwa uvimbe pembeni mwa jicho au yote mawili na kusababisha asione vizuri.

Nitajuaje kama mtoto ana macho makengeza?

Kama unadhani mtoto ana matatizo ya macho, ongea na daktari mara moja. Kuanza matibabu mapema kunaweza kupunguza uwezekano wa kupoteza uwezo wake wa kuona. Unapaswa kuongea na daktari kama mtoto wako:

  • Anavisogeza vitu karibu na uso ili kuviangalia / kuviona
  • Ana finya au kugeuza kichwa upande ili kuona vitu
  • Ana macho ambayo hayajakaa sawa, yanaonekana kama yanaangaliana au yanacheza cheza kwenda upande mmoja
  • Anashindwa kukufuatalia unapokuwa unatembea kuelekea upande mwingine wa chumba

Je, daktari atatambua vipi kama mtoto ana tatizo hili?

Kama mtoto hawezi kuona kitu kilicho karibu au kama anapata shida kuona chart inayotumiwa na daktari kupima uoni wa watu. Daktari anaweza kumwagiza mtoto aende kwa daktari wa macho ili kupimwa. Watoto wote wenye umri kati ya miaka 3 na 5 wanapaswa kufanyiwa uchinguzi na daktari angalau mara 1.

Je, macho makengeza yanatibiwaje?

Macho makengeza hutibiwa kwa kuvaa kifuniko (patch) na kufunika jicho zuri ambalo halina matatizo kwa muda au kutumia dawa ya matone ya macho kwenye jicho zuri kwa siku kadhaa.

Kufunika jicho zuri au kuweka dawa ya matone kama “atropin” inafanya uoni wa jicho zuri kupungua (kuweka ukungu) na kwa sababu hii kunamlazimisha mtoto kutumia jicho lililo na tatizo kuona. Kulazimisha ubongo kutumia picha kutoka katika jicho lililo na tatizo husaidia kurejesha mlingano.

Baada ya mtoto kuanza matibabu haya, ataanza kuona matokeo baada ya wiki kadhaa, lakini inaweza kuchukua miezi ili kupata matokeo bora zaidi.

Baadhi ya watoto wanahitaji kufanyiwa upasuaji ili kupona. Daktari atakusaidia kuamua mpango sahihi kwa ajili ya mtoto wako. Ni muhimu kuonana na daktari wa macho mapema ili kuchunguza macho ya mtoto, hata baada ya matibabu

Vyanzo

https://medlineplus.gov/amblyopia.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *