Maelezo ya jumla
Malengelenge ‘’blisters’’ kwa kawaida hutokea kwenye miguu na mikono, na husababishwa na msuguano au shinikizo. Mwanzoni ngozi inabadilika na kuwa nyekundu inayouma, kisha majimaji huanza kujikusanya chini ya ngozi na kutengeneza kimfuko kidogo kilichojaa majimaji. Unaweza kupata malengelenge kwenye visigino, unyayo au kwenye vidole kama umevaa viatu visivyokutosha vizuri, au kama ni vipya. Lengelenge kwenye mikono mara zote husababishwa na kufanya kazi ngumu za mikono. Malengelenge kwa kawaida hupona haraka: ngozi mpya unapoanza kutengenezeka chini yake hufyonza majimaji na ngozi ya mahali hapo kukauka na hatimaye kubanduka.
Tafuta masaada wa kitabibu kama una malengelenge na:
Panga kumwona daktari kama:
- Una lengelenge ambayo Imetokea tu yenyewe bila kusababishwa msuguano au shinikizo na/au una dalili nyingine
- Malengelenge yanaanza kuwa mekundu, yanayouma, na kuvimba , na kutoa usaha au damu
- Una lengelenge Inayojirudia jirudia au yanayochelewa kupona
- Una ugonjwa wa kisukari
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kama una malengelenge
Unaweza kufuata utaratibu ufuatao kutibu malengelenge. Yakinge ili kuzuia msuguano zaidi ili yapone.
- Usipasue lengelenge au kukata ngozi iliyo juu yake. Ngozi husaidia kuzuia maambukizi.
- Safisha na kukausha lengelenge, na ikiwezekana ifunge kwa ‘’adhesive tape’’.
- Hudumia lengelenge taratibu ili usitoboe ngozi na hakikisha panabakia safi na pakavu ili kupunguza uwezekano wa kupata maambukiai.
- Osha eneo lenye lengelenge kwa umakini kwa kutumia maji. Kasha eneo hilo kwa kuweka pamba safi ili kunyonya maji
- Funika eneo lenye malengelenge kwa kutumia ‘’adhessive dressing’’, hakikisha kuwa inafunika lengelenge lote.
- Kama malengelenge yakipasuka, usijaribu kuondoa ngozi inayoizunguka. Pasafishe, pakaushe na kisha pafunike kwa kitambaa safi au ‘’dressing’’ na hakikisha unabadilisha kila siku mpaka utakapopona. Ni vizuri kupaacha wazi wakati wa usiku ili pakauke.
Kuzuia
Unaweza kuepuka kupata malengelenge kwa kufuata maoendekekzo yafuatayo. Mapendekezo haya yatasaidia kulinda miguu na mikono na kupunguza msuguano au shinikizo.
- Vaa viatu vinavyokutosha vizuri, na ni vizuri kuzoesha kiatu kipya taratibu. Weka sponji ndani ya kiatu katika maeneo ambayo unadhani yanaweza kusababisha malengelenge
- Kama unapanga kutembea umbali mrefu, vaa soksi safi na nzito ili kupunguza msuguano, ikiwezekana vaa mbili kwa pamoja.
- Kama unafanya kazi ngumu ya mikono, vaa glavu za kufanyia kazi