Mapafu na mfumo wa upumuaji
Unapovuta hewa ndani, hewa yenye oksijeni inapitia kwenye pua na mdomo na kusafiri mpaka kwenye mapafu.
Wakati wa kutoa hewa nje, hewa chafu ya ukaa ‘’carbondioxide’’ na uchafu mwingine hutolewa nje.
Mtu ambaye ameshindwa kupumua, hufa baada ya dakika 4 -5.
Hewa inapofika kwenye mapafu, husafiri kutoka kwenye vifuko vidogo vya hewa vinavyoitwa alveoli na kuingia kwenye damu.
Wakati huohuo carbondioxide husafiri kutoka kwenye mtiririko wa damu na kuingia kwenye alveoli tayari kwa kutolewa nje.
Shughuli hii ya kubadilishana hewa kati ya mapafu na damu huondoa hewa chafu na kuingiza hewa safi kwenye damu.
Kupumua sio hiari
Kupumua ni lazima
Linda mfumo wako wa upumuaji
- Usivute sigara
- Epuka kukaa sehemu zenye uchafuzi mkubwa wa hewa
- Jikinge na maambukizi; nawa mikono, vaa barakoa, pata chanjo n.k
- Fanya mazoezi ili kuboresha kazi ya mapafu
- Kula mlo kamili
- Mwone daktari unapohisi unaumwa