Maelezo ya jumla
Mapigo ya moyo kwenda mbio – kwa kawaida moyo unapopiga huwa hatuna ufahamu au kuhisi kuwa unapiga, lakini unapoanza kwenda mbio au kupiga isivyo kawaida unahisi unaenda kwa kasi au unapiga isivyo kawaida. Kwa wakati mwingi hali hii ni ya kawaida. Sababu za hali hii ni pamoja na mazoezi, furaha, msongo, wasiwasi na kutumia viamsha mwili kama vile kahawa yenye kafeini au sigara yenye nikotini.
Katika hali ya kawaida mapigo ya moyo huenda mbio kwa sekunde au dakika kadhaa na baadae hupungua na hutokea bila kuwepo kwa dalili nyingine yoyote. Mapigo ya moyo yanapoenda mbio sio tatizo la kutia wasiwasi, lakini kama yakianza kwenda mbio bila sababu ya msingi au yakitokea sambamba na dalili nyingine au kama yataendelea kupiga kwa muda mrefu, yanaweza kuwa yanashiria kuwa kuna tatizo.
Mapigo ya moyo kwenda mbio – mwone daktari kama
Tafuta usaidizi wa kitabibu haraka sana kama:
- Mapigo ya moyo yanaenda mbio na unatokwa na jasho, unapata shida kupumua, maumivu ya kifua, unajihisi kizunguzungu au umezimia/kupoteza fahamu
- Una matatizo ya muda mrefu ya moyo
Panga kumwona daktari kama:
- Ni vizuri kupanga kumwona daktari mapema iwezekanavyo kama unaona mapigo yanapiga haraka kwa muda mrefu sana na/au unahisi yanaruka ruka mapigo / yanasita kupiga
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe
Kama mapigo ya moyo yanaenda mbio mara kadhaa, jaribu kufanya mambo yafuatayo ili kutambua sababu yake ili ushughulike nayo
- Tunza kumbukumbu kwenye kitabu, andika unapoona mapigo yanaenda kasi au yanapiga isivyo kawaida na vyakula ulivyokula au kunywa, mazoezi uliyofanya, kama una msongo, au sababu nyingine ambazo unaweza kuwa nazo kwa wakati huo
- Kama una msongo, jaribu kufanya mazoezi ya upumuaji ‘’deep breath exercise’’ na kutumia mbinu za kulegeza misuli ‘’muscle relaxation technique’’. BONYEZA HAPA KUJIFUNZA MBINU HIZO
- Pata usingizi wa kutosha. Kuchoka kunakotokana na kukosa usingizi wa kutosha kunaweza kusababisha au kuongeza ukali wa tatizo
- Punguza matumizi ya vinywaji vyenye kafeini. Vinywaji vyenye kafeini ni pamoja na kahawa, chai na cola. Punguza matumizi mpaka vikombe viwili au chini ya hapo kwa siku, lakini punguza taratibu, ukipunguza haraka unaweza kupata maumivu ya kichwa.
- Kabla haujatumia madawa ya kudhibiti kikohozi au za kutibu mafua, angalia kwenye ‘’label’’ vizuri. Baadhi ya madawa ya mafua yanaweza kusababisha moyo kwenda mbio.
- Punguza matumizi ya pombe; matumizi makubwa ya pombe yanaweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda mbio
- Jaribu kuacha kuvuta sigara, kwa sababu ‘’nicotine’’ inaweza kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kusababisha moyo kwenda mbio
- Usitumie madawa ya kulevya kama vile ‘’amphetamines’’ au ‘’cocaine’’, kwa sababu madawa haya yanaweza kusababisha moyo kwenda mbio
Mapigo ya moyo kwenda mbio – mwone daktari
Panga kumwona daktari kama:
- Bado unaendelea kupata matukio ya mapigo ya moyo kwenda mbio au moyo kupiga isivyo kawaida japo umejaribu kupunguza au kuondokana na vitu vinavyoweza kusababisha
- Unaona kuna dalili nyingine zinaambatana na tatizo hili, kama vile kupungua uzito au uchovu
Mwanangu huwa mapigo yake Yana piga haraka haraka ila anacheza vizuri tu.na halalamiki.ila mara nyingine akitembea usema amechoka,yupo darasa la tatu Ana miaka tisa kasoro.wakati mwingine ukimgusa kifuani unasikia mapigo hupiga Kasi naomba maoni yako
Habari, pole sana
Zipo sababu nyingi sana zinazoweza kusabbisha tatizo kama hili kwa watoto, sababu nyingine ni za kawaida tu na nyingine ni kubwa zinazohitaji uangalifu mkubwa aktika matibabu. Ninashauri ukutane na daktari, amfanyie uchunguzi wa mwili na kama ataona kuna viashiria vya ugonjwa ataagiza afanyiwe vipimo ili kujua sababu. Mapigo ya moo kwenda mbio ni dalili ya matatizo mengi. Asante na karibu tena
Nlikua mjamzito nikapata missed abortion nimepata matibabu lakin moyo unaenda mbio Sana
Pole sana, yawezekana umepungukiwa damu, ulipaswa kutumia dawa za kuongeza damu kwa angalau mwezi mmoja mpaka 3. kama haukupata dawa hizi. nenda kituo cha afya ufanyiwe tathmini kama vp upewe dawa. au ongea na daktari wetu atakushauri zaidi na ikiwezekana atakuandikia dawa bora za kununua
Me nnatatizo la moyo kwenda mbio na linanitokea mara nyingi sanaa na linaweza likachukua hata kama lisaa lizima mpaka nahc mwili kukosa nguvu kabisa mara nyingine naskia mpaka kwenye uti wa mgongo inakaza na kupumua napumia kwashida nifanyeje?? Ili nirudi katika hali ya kawaida??
habari
sante kwa kutuandkia, pole sana pia
mapigo ya moyo kwenda mbio ni dalili inayosababishwa na matatizo mengi, kama unaonatatizo hili linaendelea, fika kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi wa mwili na ikibidi daktari ataagiza vipimo kuangallia nini tatizo
pole sana na ugua pole
Mwanangu ndo anaanza kusimama cku mbili nyuma alipatwa na mafua pia kuchemka nilifika kituo cha afya akapimwa MRDT ikawa negative akaaandikiwa cephalexin cetirizine na Panadol nikamnunulia lakin toka nimerud moyo unamuenda mbio na joto linapungua kwa mda mfupi tu sijui tatizo n nn hasa
Naona nimechelewa kukujibu. Kwa maswali yanayohusu dharura ni vizuri kutumia namba iliyopo hapo chini, ili kupata jibu harak. I hope anaendelea vizuri
Doctor mimi ninatatizo hilo la mapigo ya moyo kwenda kwa kasi sana hata nikiwa niko kawaida tu hiyo hali inatokea mara kwa mara nakosa nguvu,kizunguzungu na nashindwa kupumua vizuri sijuwi nifanyaje
Mimi huwa ninapata maumivu ya
Kichwa ( kipanda uso) nahisi joto na kuna muda mapigo ya moyo huenda mbio na kupoteza hamu ya kula,mwili kukosa nguvu hii hali ilinianza tangu mwaka jana mwezi wa nane mpaka sasa imenipelekea kupungua uzito wa mwili . Je linaweza kuwa tatizo gani
Ni vigumu kujua tatizo ni nini kwa maelezo haya. Ni vizuri kumwona daktari ili akupe msaada zaidi
Sorry doctor mm nlikuwa nna shda kuna siku Moyo unakuwa unadunda sana siku zingine unakuwa kawaida mara gafla unaanza kudunda haraka unaacha alaf kifuani huwa sijiskii vizur
Ni vizuri kuangalia visababishi ni nini kama hauwezi kuviondoa au hauvijui onana na daktari atakusaidia
Me hasa nikiwa peke yng sna inatokea mapigo ya moyo kwenda mbia km sekunde 1 hivi au mbili pili cku hizi cpati ucngizi vzr km nimelala bac masaa 5 tu
Jichunguze ili kuona kama kuna kisababishi, kama ukijaribu kuondoa visababishi vyote na bado ukaona yanakwenda mbi
Mwone daktari
Habari za mda huu mtaalam….. Mimi huwa na tatizo la maumivu ndani ya moyo kwa takriban mwaka sass…sikuwai kumwona dactari hadi sasa kwa hof nliyokuwa nayo…. Je kutakuwa na namna ya kuligundua tatizo
Kamwone daktar ufanyiwe uchunguzi, ni vzr zaidi ukijua
Moyo wangu huwa unaenda mbio na mara nyingine huuma ghafla Kwa mda wowote na baada ya muda hupo na kirudi katika Hali ya kawaida ni nn tatizo
Mapigo ya moyo kwenda mbia sio tatizo kama utakwenda mbio wakati wa mazoezi, baada ya kushtushwa, kunywa kahawa n.k. kama kuna sababu unayoifahamu jaribu kuidhibiti. ila kama mapigo ya moyo yanakwenda mbio yenyewe bila kuwepo sababu ya msingi unayoijua . nenda kamwne daktari akusaidie kuitafuta
Mwanangu huwa mapigo yake Yana piga haraka haraka ila anacheza vizuri tu.na halalamiki.Ana miaka miwili kasoro.wakati mwingine ukimgusa kifuani unasikia mapigo hupiga Kasi naomba maoni yako
N vizuri akanoana na daktari ili atambue sababu yake ni nini, Asante na poleni sna
Mapigo ya moyo kupiga shingoni
Mwone daktari, wakati mwingine mapigo ya moyo yanaweza ku-extend mpaka shingoni kama moyo unafanya kazi kuliko kawaida: sababu ni nyingi: upungufu wa damu mwilini, msongo wa mawazo, kushtushwa, mazoezi au kazi ngumu n.k.
Mwanangu anaumri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja alipata mafua na kifua nikamchukulia dawa lakini baada ya happy mtoto mapigo yake ya Moto yanapiga kuliko kawaida na sijui tatizo Nini
Habari Doc mimi mapigo ya moyo hunitokea gaflaa wakati mwingine hata usingizini yanapiga kwa Kasi mno na wakati mwingine inaweza kuchukua muda kuacha au Mara nyingine huambatana na Giza machoni na kuishiwa nguvu nayakiwa yanataka kupungua kurudi katika Hali yake huwa yanaachia napata kama ubaridi unapiga Hadi utosini kichwani hapo ndo unakuta yanakata yanarudi kuwa normal sasa.
pole sana, kama nilivyoelekeza, sababu ya mapigo ya moyo kwenda kasi ni nyingi, na ni muhimu kutambua sababu. kama haujatambua sababu au kuhisi sababu ya tatizo lako hata baada ya kusoma makala hii, ni vizuri ukamwona daktari ili akusaidie kuitambua
Doctor mimi ninatatizo hilo la mapigo ya moyo kwenda kwa kasi sana hata nikiwa niko kawaida tu hiyo hali inatokea mara kwa mara nakosa nguvu,kizunguzungu na nashindwa kupumua vizuri sijuwi nifanyaje
pole sana kwa kuugua, kwa maelezo yako haya ni ngumu kutambua tatizo lako hasa ni nini?, kama umeona moja ya jambo linalosababisha katika makala hii katika maisha yako, jaribu kulirekebisha kwanza, yawezekana ukapata nafuu.
kama nilivyosema hapo awali, sababu ni nyingi , kama umeshindwa kuitambua ni vyema kumwona daktari akusaidie kuitambua na hata kufanya vipimo
Mimi Nina maumivu ya moyo hasa ninapofanya mazoez ya kwa dak20 pia moyo huenda mbio,napungukiwa na nguvu za mwili,uchovu mwingi,na pia Nikola baadhi ya vyakula napata chida ya kukosea nguvu na mapigo kuongezeka,naomba msaada wa Hili dactari
pole sana. kuna mambo mengi sana yanayoweza kusababisha tatizo lako, hizi zinaweza kuwa dalili za upungufu wa damu, matatizo ya moyo hasa chembe ya moyo./ angina au yawezekana hakuna shida kubwa pia
ninashauri uangalie makala yetu kuhusu angina/chembe ya moyo kama una dalili kama hzo onana na daktari
ila kama sivyo, basi boresha mfumo wako wa maisha, punguza mafuta, chumvi na sukari kwenye mlo wako. kula mboga, matunda na mzizi kwa wingi
na fanya mazoezi
unaweza kuchoka haraka na moyo kwenda mbio kwa sababu haujafanya mazoezi muda mrefu
Ushauri tafadhali Dr, me sina shida yoyote ya mwili nafanya kazi zote vizuri, ata upumuaji sina tatizo, tatizo nikisha kula chakula chochote ata chai na adazi, mapigo ya moyo yanakimbizana, kigne wakati nakaribia siku zangu napo moyo unaenda kama nakimbia marathoni flani, shida n nini? Pia dawa sina ya ampicillin inaweza akawa na chanzo au shida, kwani Nina zitumia sana, Nina shida ya kupata kivua ata kwa vumbi LA ndani au perfermu nilio endana nayo, basi me nikumeza hizo dawa. Tafadhali ushauri
Pole sana
Najua kujisikia hvyo kunaweza kukupa shida , kama una wasiwasi ni vzr kufanyiwa uchunguzi na daktari
Inawezekana usiwe na tatizo lolote kabisa, kwa maelezo yako haya haitoshelezi kukushau3i vzr, ni vzr kumwona daktari
Polee sana
Mke wangu baada ya kunifungia baada ya wiki mbili tatzo la moyo kwenda Kasi lilimuanza wkt anakuwa vzr tu Hana shd yoyote ila c kwa muda Sana lnaacha