Maelezo ya jumla
Mapunye/ Vibarango/ Mashilingi ni ugonjwa unaosababisha madoadoa kama magamba kwenye ngozi. Madoa ni ya mviringo, yanayowasha, mekundu na yanaongezeka ukubwa ndani ya wiki moja au zaidi. Mwishowe yanatengeneza umbo kama pete nyekundu.
Mashilingi yanaweza kutokea mahala popote mwilini, lakini mara nyingi yanatokea zaidi kwenye ngozi ya kichwani. Mapunye yanaweza pia kusababisha nywele zikakatika kwa urahisi na kusababisha mtu kupoteza nywele
Ugonjwa huu unasababishwa na maambukizi ya fangasi, ambao huambukizwa kwa kugusana na mtu mwenye vibarango au kama mnachangia vitu kama taulo au vitana vya nywele.
Mwone daktari kama una mapunye/vibarango/mashilingi
Ni vizuri kupanga kumwona daktari
- Kama una mapunye mengi au kama una vibarango kwenye ngozi ya kichwa
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe ukiwa na mapunye
Unaweza kuondoa mapunye mwilini kwa kufanya mambo yafuatayo AU unaweza kufanya mambo yafuatayo sambamba na matibabu atakayokuwa amekuandikia daktari
- Kama una eneo dogo lenye kibarango, unaweza kujaribu kutumia “cream” yenye dawa ya kuondoa fangasi (antifungal cream).
- “Cream” kama hizi zinatumika kutibu sehemu ndogo yenye mapunye kama bado hujaenda kwa daktari akuandikie dawa. Paka kama maelekezo yanavyoelekeza kwenye pakiti.
- Ukiendelea kupaka tunategemea kuwa utaanza kuona mapunye yanaondoka baada ya wiki 1 au 2, japo inaweza kuchukua tena wiki nyingine kadhaa vibarango kupotea kabisa, kwa hiyo kuwa na subira
- Endelea kutumia hiyo cream kwa siku nyingine kadhaa hata baada ya kuona kuwa umepona kabisa
- Kila baada ya kupaka hii cream au kushika mashilingi, nawa mikono vizuri
- Weka ngozi kuwa safi na kavu na jitahidi usijikune
- Ili kuzuia usiwaambukize wengine au kujiambukiza mwenyewe tena, fua nguo, matandiko na taulo ulizotumia. Kama una mapunye kichwani, pia osha vitana, brashi na kofia mara tu baada ya kuzitumia
- Epuka kuwashika wanyama wenye dalili za maambukizi, kwa mfano wanyama ambao unaona nywele zinanyonyoka. Kama unahisi mfugo wa kufugwa ana mapunye hakikisha anapata matibabu kutoka kwa mtaalamu wa afya ya wanyama
- Kama una mapunye kwenye kichwa, tumia shampoo nyepesi, kwa mfano baby shampoo na kisha suuza na kukausha nywele vizuri, epuka kutumia hair dryer. Usitumie gels na bidhaa nyingine kwenye nywele.
- Sio lazima ujitenge na watu wengine, lakini vizuri ukaepuka kujihusisha na michezo au shughuli zinahitaji kugusana na watu wengine mpaka umetumia antifungal kwa angalau siku 4.
Omba msaada wa daktari kama
Panga kumwona daktari kama:
- Kama mapunye hajaanza kuitikia matibabu japo umekuwa ukipaka dawa vizuri kwa zaidi ya wiki moja
- Kama unaona ngozi imekuwa nyekundu au kama unaona mapunye yanatoa majimaji au kama kidonda kimetokea
- Kama una uvimbe mkubwa kwenye ngozi ya kichwa na unatoa usaha au unasababisha nywele kunyonyoka
Mimi nimetoka na hayo mapunye sijui ila sijawahi kuwa natabia ya kuchangia kitu chochote sasa nilitumia sonaderm lakini baada ya mda yamerudi tena sasa sielewi
Pole sana, tumia tena dawa
na yanatokea sehemu gani ya mwili?
na mimi yamenipata tuboni na mgongoni sijui hata yametokana na nini natumia griseofulvini kwa sasa yanakauka yaancha alama ila kuna kama mawili mabisho sana yanakauka ukijakucheki tena unakuta yapo hai nachukia sana kwa sasa yamebaki matatu tu
Kuwa na subira, endelea kutumia dawa yataisha. Magonjwa yanayosababishwa na fangasi huchukua muda mrefu zaidi kupona kuliko magonjwa mengine
Kuwa na subira, endelea kutumia dawa, utapona