Matatizo ya lenzi za macho ‘’contact lens ‘’

Sababu kubwa ya matatizo ya lenzi za macho yanatokana na lenzi ambayo haikai sawa kwenye jicho, lenzi ambayo haifanyiwi usafi vizuri, lenzi ambayo inaharibiwa na dawa za kusafishia na vumbi au mazingira yenye upepo mwingi. Kama ukivaa lezi kwa muda mrefu au kukiwa na kipande cha uchafu au vumbi iliyotwama au kujificha nyuma ya lenzi, macho yanaweza kuanza kuhisi usumbufu, kuwa mekundu na yanaweza kuanza kutoa machozi. Wakati mwingine lenzi inaweza kuteleza ikaingia sehemu ya ndani ya kope na utahitaji kuifuatailia na kuirudisha mahala pake.

Mwone daktari haraka kama

Tafuta msaada wa haraka kama:

  • Kama macho yanauma, , unaona maluweluwe au kama uwezo wako wa kuona umepungua au kama mwanga unakuumiza sana ukiuangalia
  • Kama macho yamekuwa mekundu sana

Matatizo ya lenzi za macho – unachoweza kufanya mwenyewe

Ukifanya mambo yafuatayo unapunguza sana hatari ya kupata matatizo ya macho kama unatuamia lenzi ya macho

  • Kama unaona au unahisi macho yanapata usumbufu, ondoa au toa lenzi kwa muda wa saa moja au mbili kisha angalia kama dalili zitapungua. Kama zitajirudia utakapoweka tena lezi ndani, ni vizuri kumwona daktari au mtaalamu wa macho aangalie tatizo ni nini
  • Unaweza kujaribu kutumia maji maalumu ya kulowesha jicho (matone ya machozi bandia ‘’lubricating eyedrops”) ambayo yametengenezwa maalumu kwa ajili ya kutumika na lenzi za macho
    • Matone haya ya kulowanisha au kuongeza unyevu kwenye macho huwa yametengenezwa kwa ”sodium chloride” ambayo husababisha iwe rahisi kuweka na kutoa lezi jichoni.
    • Usitumie aina nyingine za matone ya kulowesha jicho ‘’eyedrops’’ bila ushauri wa daktari au mtaalamu wa macho, kwa sababu baadhi ya bidhaa hizi zinaweza kuharibu lenzi
  • Isipokuwa kama unatumia lenzi za macho za kuvaa muda wote ‘’continous-wear lens’’, usivae lenzi muda mrefu zaidi ya uliyoelekezwa na mtaalamu wa macho. Kama unaona haiwezekani, ziondoe mara moja moja ili kupumzisha macho. Hakikisha unavua lenzi kabla haujaenda kulala, kujilaza au wakati wa kuogelea au kuoga
  • Kabla haujashika lensi za macho, safisha mikono kwa kutumia kitakasa mikono au nawa kwa kutumia sabuni vizuri na kisha suuza mikono vizuri kabisa
  • Safisha na kusuuza lenzi vizuri kila unazitoa kwenye macho kwa kutumia dawa maalumu za kusafishia na kutunzia kama ilivyoelekezwa. Safisha pia kikopo cha kutunzia lenzi na kikaushe vizuri.
  • KAMWE, usilambe au kutumia maji kulowanisha lenzi kabla ya kuziweka jichoni
  • Unaweza kuongea na mtaalamu wa macho ‘’optometrist’’, kuna aina ya lenzi za macho unazotumia mara moja na kutupa ‘’disposable contact lens’’, kama mazingira yanaruhusu unaweza kutumia hizi, hautahitaji kuziosha kila mara maana zinatumika mara moja tu ndani ya siku moja. Zinapunguza uwezekano wa kupata usumbufu kwenye macho
  • Kuwa makini unapotumia vipodozi. Paka vipodozi baada ya kuweka ndani ya jicho lenzi ya macho, na usitumie ”eye shadow” iliyotengenezwa kwa poda au poda aina yoyote kwenye macho. Kama unatumia ”Spray” za nywele jitahidi zisiingiendani ya macho.
  • Lenzi za macho haziwezi ‘’kupotelea’’ ndani ya jicho. Ila kuna wakati lenzi inateleza na kuingia chini ya kope ya jicho. Jaribu njia hii ili kuirudiha ikae vizuri kwenye jicho
    • Kwanza, weka matone 2-3 ya kilainishi ‘’eyedrops’’ kwenye jicho husika. Wakati mwingine kama jicho ni kavu, kuweka tu majimaji haya yanayolainisha yanaweza kusababisha lenzi ikaelea na kurudi mahala pake bila wewe kufanya jambo jingine lolote

matatizo ya lenzi za macho

    • Pili, Kama kuweka ”eyedrops” hakujasaidia, funga jicho, kisha iongoze lenzi kwenda kwenye eneo husika kwa kubonyeza taratibu juu ya kope kwa kutumia kidole kimoja. Ukifanya hivi itasaidia kuisukuma lenzi irudi kwenye sehemu ya mbele ya jicho

Matatizo ya lenzi za macho – mwone daktari kama

Unapaswa kumwona daktari au mtaalamu wa macho kama:

  • Kama usumbufu kwenye jicho unaendelea au kama unaona kuna uchafu unatoka kwenye jicho
  • Kama unaona kuna tatizo jipya limejitokeza kwenye macho/jicho lako

Vyanzo

https://www.aao.org/eye-health/glasses-contacts/contact-lens-102

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *