Maelezo ya jumla
Wanawake wenye matatizo yanayotokea siku chache kabla ya hedhi ‘’premenstrual syndrome’’ husumbuliwa na dalili kadhaa ambazo huanza siku angalau siku 7 kabla ya hedhi na kuanza kupungua baada ya damu ya hedhi kuanza kutoka. Unaweza kuwa mwenye kisirani, mgomvi, mwenye hasira, mwenye huzuni mwingi au unaweza kuwa na wasiwasi mwingi bila sababu ya msingi. Unaweza kujisikia hauko sawa na ukapata ugumu kufikiria ‘’concentrate’’ vizuri. Dalili nyingine ni pamoja na maumivu ya kichwa, matatizo ya kupata usingizi, kutamani aina fulani ya vyakula, kufunga choo, kuvimbiwa, kupungua uzito na maumivu au uvimbe kwenye matiti. Msongo wa mawazo unaweza kuchangia kutokea kwa matatizo haya.
Kama una matatizo yanayotokea siku chache kabla ya hedhi mwone daktari kama
Panga kumwona daktari kama hauna uhakika kuwa dalili unazozipata zinatokana na haya matatizo yanayotokea siku chache kabla ya hedhi ‘’PMS’’
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kama una matatizo yanayotokea siku chache kabla ya hedhi
Kuna baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyafanya wewe mwenyewe ili kudhibiti matatizo haya. Anza kutumia mbinu hizi kabla ya dalili ya kwanza kujitokeza.
- Kula mara kwa mara ili kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu na kupunguza uwezekano wa kuwa mgomvi na mkali. Kula vyakula vyenye wanga kwa wingi, kama vile pasta na viazi, na ongeza kiwango cha matunda na mbogamboga unachotumia. Epuka kula vyakula vyenye sukari nyingi; kama una njaa kabla muda wa kula haujafika, kula matunda au kula mkate usiokobolewa.
- Punguza matumizi ya chumvi; tumia viungo vingine ili kuongeza ladha ya chakula
- Kunywa maji angalau gla 6-8 kwa siku na punguza unywaji wa vinywaji vyenye ‘’caffeine’’ kama vile kahawa. Epuka kunywa pombe siku chache kabla ya kipindi cha hedhi.
- Unaweza kuwa na daftari maalumu litakalo kukumbusha vitu unavyopaswa kufanya ili kupunguza karaha
- Jaribu kupunguza msongo wa mawazo. Kama inawezekana ahirisha kwanza kufanya maamuzi au mipango mikubwa na epuka maamuzi magumu. BONYEZA HPA KUJIFUNZA JINSI YA KUDHIBITI MSONGO
- Nenda nje ukapate hewa safi na ikiwezekana tembea ili ujinyooshe. Pata usingizi wa kutosha usiku
Kuzuia matatizo yanayotokea siku chache kabla ya hedhi
Ili kuzuia baadhi ya matatizo haya, unaweza kufanya mambo yafuatayo na yakasaidia kupunguza karaha na kukusaidia kudhibiti yal yanayobakia
- Tunaz daftari la kumbukumbu kwa muda wa miezi 3 ukiandika ni vitu gani vinafanya dalili kuwa mbaya zaidi, kwa mfano aina fulani za vyakula au msongo wa mawazo unaotokana na kazi, ili siku ingine uweze kuepuka.
- Unaweza kujaribu kutumia vitamin B6 ili kupunguza dalili. Kuna ushahidi kuwa vitamin B6 husaidia kuzuia dalili zinazotokea siku chache kabla ya hedhi.
- Unaweza kuhitajika kutumia virutubisho hivi kwa muda wa miezi 2-3 ili kuanza kuona matokeo.
- Au kama mbadala , unaweza kuboresha mlo kwa kula vyakula vyenye B6 kwa wingi, kama vile kuku, mayai, ndizi na karanga.
- Jitahidi kuembea kwa angalau dakika 20-30, siku 5 za wiki au unaweza kuanza kufanya mazoezi ya kuogelea au yoga mara kwa mara.
Mwone daktari kama
Panga kumwona daktari kama:
- Bado unaendelea kuona matatizo yanayotokea siku chache kabla ya hedhi, hata baada ya kufuata ushauri uliotolewa hapa au kama unaona dalili zinazidi kuwa mbaya zaidi
This is a topic that’s close to my heart… Cheers! Exactly where
are your contact details though?
Feel free to surf to my site: lam bang cao dang