Maelezo ya jumla

Tatizo la kujipinda miguu au matege  (bowlegs) huchukuliwa kuwa jambo la kawaida kwa watoto chini ya miezi 18. Mtu mwenye tatizo hili akisimama mguu sawa magoti hayagusani, magoti huwa mbali mbali kama vifundo vya miguu vimekutanisha.

Je, nini dalili za kujipinda miguu/matege ?

  • Magoti hayagusani akisimama mguu sawa (vifundo vya miguu vikiwa vimegusana)
  • Kupinda kwa miguu huwa ni linganifu kwa pande zote mbili (kupinda kwa upande mmoja ni sawa na upande mwingine)
  • Matege huendelea kuwepo hata baada ya umri wa miaka 3

Kujipinda miguu/matege husababishwa na nini?

Watoto wanazaliwa na hali hii kwa sababu huwa wamejikunja wanapokuwa ndani ya mji wa mimba (uterasi). Miguu ya watoto wachanga wenye matege huanza kunyooka wanapoanza kutembea (katika umri wa miezi 12 hadi 18). Miguu ya mtoto mwenye tatizo hili hunyooka kabla ya umri wa miaka 3, isiponyooka huitwa matege.
Matege yanaweza kusababishwa na magonjwa kama vile:

  • Ukuaji usio wa kawaida wa mifupa (bone dysplasias)
  • Mvunjiko wa mifupa ambao haukupona kwa usahihi
  • ugonjwa unaosababishwa na sumu ya risasi (lead) au floraidi
  • Matege ”rickets” yanayosababishwa na upungufu wa vitamini D

Utambuzi wa matege/kujipinda miguumatege

Mara nyingi daktari atatambua kuwa mtoto ana shida hii kwa kumwangalia tu.  Daktari hupima umbali kati ya goti moja na jingine mtoto akiwa amelala chali. Vipimo vya damu vinaweza kuhitajika ili kuhakikisha mtoto hana upungufu wa vitamin D unaoweza kusababisha matege (rickets)
Eksirei zinahitajika kama:

  • Mtoto ana umri wa miaka 3 au zaidi
  • Tatizo linazidi kuongezeka
  • Kama kupinda kwa mguu mmoja si sawa na mwingini
  • Kama matokeo ya vipimo vingine yameashiria kuna ugonjwa

Ukiwa na matege ni wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone mtoa huduma ya afya kama mtoto mwenye umri zaidi ya miaka mitatu ana matege au yanaongezeka.

Uchaguzi wa matibabu kama una matege/tatizo la kujipinda miguu

Hakuna tiba inayopendekezwa kutibu matege ya kawaida. Ila mtoto anapaswa kumwona daktari kwa angalau mara moja kila baada ya miezi 6.
Kama hali ni mbaya sana au kama mtoto ana ugonjwa mwingie, viatu maalum, braces, au hogo (cast) vinaweza kutumiwa. Ila hakuna uhakika wa vitu hivi kuleta mabadiliko. Wakati mwingine, upasuaji hufanywa ili kurekebisha ulemavu huu, hasa kwa vijana walio kwenye balehe wenye miguu iliyojipinda saana.

Nini cha kutarajia ?

tatizo la kujipinda miguuKwa kesi nyingi matokeo ni mazuri, na huwa hakuna shida wakati wa kutembea.

Matatizo yanayoweza kutokea

Matege ambayo hayaondoki na hayatibiwi, yanaweza kusababisha kutokea kwa yabisi kavu magotini  au mapajani kadri muda unavyokwenda.

Kuzuia

Hakuna njia ya kuzuia hali hii, lakini unaweza kuepuka matege (rickets) yanayosababishwa na ukosefu wa vitamin D. Hakikisha mtoto anapata mwangaza wa jua na  kula mlo wenye vitamini D ya kutosha.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/rickets.html#:~:text=Rickets%20causes%20soft%2C%20weak%20bones,the%20minerals%20calcium%20and%20phosphorous.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *