Maelezo ya jumla

Matubwitubwi au machubwichubwi ”Mumps” ni ugonwa unaosababishwa na virusi na ulikuwa unawaathiri sana watoto kabla ya enzi za chanjo. Dalili za ugonjwa huu huanza kuonea siku 2 – 3 baada ya kuambukizwa. Dalili za mwanzo za ugonjwa huu ni homa, maumivu ya kichwa na maumivu ya misuli. Baadae hufuatiwa na uvimbe kwenye upande mmoja au pande zote za uso na shingo. Uvimbe huu hutokana na kuvimba kwa ezi za ‘’parotid’’ zilizo mbele kidogo ya masikio.  Mgonjwa anaweza kuhisi maumivu wakati wa kuogea, kula na kunywa. Matubwitubwi ni ugonjwa ambao sio mkali sana ukiwapata watoto wadogo, lakini unaweza kuleta madhara makubwa ukiwapata vijana wanaobalehe au watu wazima.

Kama una matubwitubwi mwone daktari kama;

Panga kumwona daktari ili agumbue ugonjwa huu wa matubwitubwi na kuangalia kama kuna matatizo mengine yaliyosababishwa na ugonjwa huu.
Mwone dakatari haraka sana kama unaanza kuona mambo yafuatayo:

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kama una matubwitubwi

Hakuna matibabu maalumu ya ugonjwa huu, lakini ukifanya mambo yafuatayo yatapunguza karaha kwa mgonjwa

  • Pumzika kadri unavyoweza mpaka utakapoona dalili zinaanza kupungua
  • Weka kitambaa cha moto kwenye eneo lililoathirika, chukua kitambaa kilichochovya kwenye maji ya moto, kikamue na kisha kiweke kwenye upande mmoja wa uso uliovimba itasaidia kupunguza maumivu kwenye tezi zilizovimba.
  • Kunywa maji ya kutosha, epuka vinywaji vyenye asidi nyingi kwa sababu vinachachawisha na kuzalisha mate mengi, na kwa sababu hii kusababisha tezi kuuma zaidi. Tumia mrija kunywa kama kupanua mdomo ni shida.
  • Kunywa supu, maziwa ‘’yogurt’’ au vinywaji vingine baridi, kula vyakula laini ambavyo ni rahisi kumeza.
  • Tumia dawa ya kupunguza maumivu ili kupunguza homa na kupunguza maumivu ya tezi zilizovimba
    • Kwa mtoto, mpatie ‘’acetaminophen’’, unaweza kuipata dawa ya kunywa au kidonge cha kutafuna AU unaweza kutumia ‘’ibuprofen’’, inayopatikana kama dawa ya kunywa
    • Hakikisha unamuuliza mfamasia, ili kupendekeza aina ya dawa inayomfaa zaidi mtoto
    • Watu wazima wanaweza kutumia ‘’acetaminophen’’ au ‘’ibuprofen’’
  • Kama ugonjwa wa matubwitubwi utaathiri korodani, baki kitandani na uvae nguo zinazotengemeza pumbu, kwa mfano unaweza kuvaa chupi 2 zinazobana mpaka utakapoona dalili zimepungua

Angalia pia: maumivu ya pumbu

  • Kama hakuna matatizo mengine yaliyojitokeza, mtoto anaweza kurudi shuleni, au kama ni mtu mzima kurudi kazini siku 5 baada ya ugonjwa kuanza. Kupona kabisa kunaweza kuchukua wiki 1 – 2.matubwitubwi

Kuzuia matubwitubwi

Chanjo ili kukinga dhidi ya ugonjwa wa matubwitubwi hutolewa kwa watoto wote kama ilivyoelekezwa na mpango wa taifa wa chanjo. Hakikisha kuwa mtoto wako anapata chanjo ya kuzuia ugojwa wa Matubwitubwi.

Ukiwa na matubwitubwi mwone daktari

Panga kuonana na daktari kama:

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001557.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *