Shisha ni nini?

Shisha ni vifaa vinavyotumia umeme (vimewekewa betri) ambavyo hupasha majimaji na kutoa moshi uliojaa unyevunyevu. Unyevuunyevu huu kama moshi huwa na kemikali ya nikotini. Kemikali ya nikotini inapatikana kwenye sigara za kawaida na ndio hufanya sigara kusababisha uraibu na ushindwe kuiacha. Baadhi ya watu wanatumia shisha  badala ya sigara za kawaida kwa sababu hazina harufu ya moshi au wanadhani sigara hizi ni salama zaidi. Watu wengi wanauita mchakato huu wa kuvuta sigara ya kisasa “vaping”

Juuls ni nini?

shisha

Kuna aina nyingi na brands mbalimbali za shisha. Kwa sasa, juuls ndio maarufu zaidi. Juuls ni ndogo, zenye umbo la mstatili na zinaonekana kama flash/thumb drive. Ni rahisi kuzitunza na kuzichaji. Juuls ina kifaa cha kushikilia au kutunzia majimaji “cartridge” , ambacho unaweza kubadilisha au kukitupa baada ya matumizi na kisha kuweka kingine. Vifaa hivi vya kutunzia majimaji unaweza kuvinunua kwa mkupuo na vina ladha mbalimbali na kiwango tofauti tofauti cha kemikali ya nikotini. Vijana walio kwenye balehe wanapendelea sana kwa sababu ya ladha mbalimbali zinazotolewa.

Je, shisha ni salama?

Hapana. Japo Shisha zinaweza kuwa salama zaidi ukizilinganisha na sigara za kawaida, hii haimaanishi kuwa ni salama kwa afya ya mwanadamu. Bidhaa ya nikotini ni kali sana na inaweza kusababisha uraibu haraka sana. Kuna kemikali nyingi katika sigara hizi za kisasa, na baadhi yao husababisha kansa. Kimiminika kinachokuwa kwenye shishaa zinaweza kuwa sumu kama zitakumwagikia kwenye ngozi au kama utazimeza. Hii inawaweka hatari watoto wadogo, kama sigara hizi hazitumiwi na kutunzwa vizuri, zinaweza kulipuka na kukuunguza au kusababisha matatizo mengine hatari.

Je, ninapaswa kuzungumza na mtoto wangu kuhusu shisha?shisha

Ndio. shishaa zimekuwa maarufu na zinapendelewa zaidi na vijana kuliko sigara za kawaida. Itasaidia kumuuliza kijana kama amewahi kusikia kuhusu “vaping” au “juuls”.  Kutumia sigara hizi za kisasa kunaweza kupelekea kijana akaanza kuvuta sigara za kawaida kwa vijana ambao hawajawahi kuvuta. Inawezekana pia kuongeza uwezekano wa kuanza kutumia bangi kwa kijana.

Msaidie mtoto kutambua kuwa shisha zinaweza kusababisha akawa na tabia mbaya na ghali ya kuvuta sigara maisha yake yote. Tabia hii inaweza kumsababishia matatizo ya ubongo, kujitambua na kihisia.

Ni muhimu kutambua kuwa, kampuni nyingi zinazotengeneza shisha zinamilikiwa na kampuni zinazotengeneza sigara za kawaida. Kampuni hizi zitafaidika iwapo kijana atakuwa na uraibu wa kuvuta nikotini na baadae kuvuta sigara za kawaida.

Je, ni ipi njia salama ya kuacha kuvuta shisha?

Njia salama ya kuacha kuvuta ni kwa kufuata namna salama zilizokwisha kufanyiwa utafiti na kuonekana zina ufanisi, kama vile kutumia gum za nikotini, lozenges na vibandiko (patch) vya nikotini. Daktari anaweza kukusaidia kuchagua njia moja inayofaa.

Kama tayari unatumia sigara hizi za kisasa na hauko tayari kutumia njia nyingine kuacha kuvuta, jaribu kubadili kabisa uvute shisha pekee (usichanganye na za kawaida). Kisha, anza kupunguza kiwango cha sigara unachovuta mpaka utakapoweza kuacha kabisa kutumia bidhaa za nikotini.

Je shisha ni salama wakati wa ujauzito?

Hapana. Nikotini inaweza kusababisha madhara kwa mtoto (mtoto akiwa bado yuko tumboni). Kemikali nyingine zilizo ndani ya shisha  pia zinaweza kusababisha matatizo. Haupaswi kutumia shisha au sigara za kawaida wakati wa ujauzito. Kama wewe ni mjamzito na unatumia sigara za kawaida au shisha, ongea na daktari akusaidie njia nzuri ya kuacha kuvuta sigara.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/patientinstructions/000761.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *