Maelezo ya jumla

Wanawake wengi wanapatwa na shida hii ya maumivu na uvimbe kwenye matiti. Dalili mara nyingi zinaathiri matiti yote mawili na huwa zinahusiana na mabadiliko ya homoni wakati wa mzunguko wa hedhi. Siku chache kabla ya kupata damu ya hedhi unaweza kupata maumivu na uvimbe kwenye matiti na yanaweza kuuma yakiguswa. Dalili hizi mara nyingi huisha zenyewe baada ya damu ya hedhi kuisha. Tatizo hili huwa linawapata zaidi vijana walio kwenye balehe, wajawazito au wanawake wanaotumia madawa ya kupanga uzazi au tiba ya homoni. Matiti ya wanawake wanaonyonyesha yanaweza kuwa mekundu, ya moto ukiyagusa na yayouma kwa sababu ya kujaa sana kwa maziwa au kwa sababu ya maambukizi. Japo sehemu kubwa ya vivimbe vinavyotokea kwenye matiti sio kansa, uvimbe unaokuwepo kwa muda mrefu unapaswa kuchunguzwa.

Kama una maumivu na uvimbe kwenye matiti mwone daktari kama

Panga kumwona daktari haraka kama:

  • Utakuta kuna uvimbe kwenye titi
  • Una uvimbe ambao unadumu kwa muda mrefu kwa kipindi chote cha mzunguko wa hedhi
  • Una maumivu ya titi yanayodumu kwa muda wote na hayana uhusiano na mzunguko wa hedhi au kama maumivu yanapafika kwenye kwapa
  • Unadhani dalili zimetokana na dawa za kupanga uzazi unazotumia au homoni unazoongezewa
  • Matiti yamevimba, ni mekundu, yanauma na yana joto ukiyashika ‘’mastitis’’

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kama una maumivu na uvimbe kwenye matiti

Unaweza kutumia njia zifuatazo ili ili kutambua na kuondoa maumivu na uvimbe kwenye matiti unaojirudia kwa kila mzunguko wa hedhi (Kama matiti yamevimba, ya moto, mekundu na yanauma, utafuata maelekezo yatakayofuata kwa chini kidogo)

  • Tunza daftari lenye kumbukumbu za mzunguko wa hedhi kwa miezi 2 au 3, ukiandika ni wakati gani matiti yanapoanza kuvimba au kuwa na vivimbe, yanapoanza kuuma na ni wakati gani dalili hizi huondoka. Hii itakusaidia kuamua kama tatizo hili linahusiana na mabadiliko ya homoni wakati wa mzunguko wa hedhi.
  • Hakikisha kuwa manati ya kubebea matiti ‘’bras’’ hayabani na yanatoshea vizuri. Jaribu kuvaa manati yenye size kubwa kidogo, wiki 1 kabla ya kuanza kupata hedhi, vaa’’bra’’ inayoyategemeza vizuri matiti ili yasichezecheze sana. Unaweza kujaribu kuvaa ‘’bra’’ laini usiku, kwa baadhi ya wanawake inawapunguzia karaha.

maumivu na uvimbe kwenye matiti

  • Punguza kiwango cha ‘’caffeine’’ unachotumia kwa kupunguza unywaji wa kahawa, chai na cola
  • Kama miguu huwa inavimba na kujaa maji, ni vizuri kupunguza kiwango cha chumvi unachotumia wiki 1 kabla ya hedhi kuanza
  • Ongeza kiwango cha wanga kwenye mlo, kula kiasi kikubwa cha matunda na mbogamboga, na epuka vyakula vya mafuta.
  • Kama uzito ni mkubwa, jaribu kupunguza uzito. Kama kuna kiwango kikubwa cha mafuta mwilini kinaweza kuathiri kiwango cha homoni mwilini na kuchangia maumivu ya matiti
  • Msongo mkubwa wa mawazo ni moja ya hatari inayoweza kukuongezea uwezekano wa kupata maumivu ya matiti. Jaribu kufanya mazoezi ya upumuaji ‘’deep breathing exercise’’ au kufanya mazoezi ya kulegeza misuli ya mwili ‘’muscle relaxing exercise’’. UNAWEZA KUJIFUNZA KUHUSU NJIA HIZI HAPA
  • Tumia madawa ya kupunguza maumivu siku unazojisikia maumivu. Madawa kama vile ‘’acetaminophen’’ au ‘’ibupprofen’’ yatasaida kukupunguzia karaha kwa siku hizo chache unazopata maumivu wakati wa hedhi. Kama unanyonyesha ongea na daktari kwanza kabla ya kuanza kutumia dawa yoyote.
  • Kwa baadhi ya wanawake wakitumia virutubisho vyenye vitamini B6 husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwenye matiti unaotokea kipindi cha hedhi
    • Vitamin B6 supplements zinaweza kusaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwenye matiti unaotokea wakati wa hedhi. Kwa kawaida utahitaji kutumia virutubisho hivi kwa miezi 2-3 kuona faida zake.
    • Usizidishe kiwango cha dozi uliyoandikiwa, kwa sababu kiwango kikubwa saa kinaweza kuleta madhara
    • Ili kuongeza kiwango cha B6 kinachoingia mwilini, kula vyakula kama vile kuku, mayai, soya, mkate usiokobolewa, nafaka, ndizi na karanga
  • Fanya uchunguzi wa matiti yako mwenyewe mara kwa mara. BONYEZA HAPA KUJIFUNZA JINSI YA KUFANYA UCHUNGUZI WA MATITI YAKO MWENYEWE

Mwone daktari kwa maelekezo zaidi kama

Panga kumwona daktari kama:

  • Unaona uvimbe ambao unakuwepo wakati wa hedhi, umekuwepo katika mizunguko 2-3 na hauondoki hata baada ya kutumia njia za kujisadia zilizoelezwa hapo juu.
  • Maumivu na uvimbe kwenye matiti unakusababishia karaha kiasi kwamba unashindwa kutekeleza majukumu ya kila siku

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003155.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *