Maelezo ya jumla
Wanawake wengi wanahisi maumivu wakati wa ngono kwa wakati fulani. Wakati mwingine, tatizo linaweza kuwa la kimwili: Kwa mfano, ngono huleta karaha kama umetoka kujifungua hivi karibuni, hasa kama ulishonwa au kama ulipata mchaniko wakati wa kujifungua au kama umefikia ukomo wa hedhi na uke umekuwa mkavu kwa sababu ya kupungua kwa kilainishi. Maambukizi au harara ukeni, au hata kufunga choo tu, kunaweza kuleta shida hii. Ukavu wa uke kwa sababu ya kukosa mshawasha au mzuka wa kushiriki ngono ni sababu pia ya maumivu wakati wa ngono. Katika hali isiyo ya kawaida, baadhi ya wanawake wanaweza kupatwa na mkazo wa misuli ya uke ‘’vaginismus’’ na kusababisha iwe ngumu au kushindwa kabisa kwa uume kuingia. Dalili za kimwili kama hizi mara nyingi zinatokana na matatizo ya kisaikolojia kama vile uwoga, aibu, hatia au uwepo wa uzoefu au kumbukumbu kuwa tendo la ngono linasababisha maumivu.
Mwone daktari kama
Panga kumwona daktari kama:
- Kama unapata maumivu ndani kabisa ya nyonga wakati wa kushiriki tendo la ngono
- Mkazo wa misuli ya uke na/ au matatizo ya kihisia yanachangia maumivu wakati wa ngono
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe
Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, jaribu kutambua sababu ni nini na chukua hatua kuzirekebisha
- Jaribu kutumia kilainishi wakati wa ngono kama uke unakuwa mkavu sana. ‘’Water-based lubricants’’ zikiwekwa ukeni kabla ya kuanza tendo la ngono husaidia kupunguza ukavu.
- Kama baadhi ya mikao wakati wa ngono inasababisha maumivu, jaribu mkao mwingine. Baadhi ya wanawake wanapenda kuwa juu, ili waweze kudhibiti ni kwa kiasi na kasi gani uume unaingia.
- Kama unadhani kuwa kukauka kwa uke kunatokana na kukosa mshawasha au mzuka wa kushiriki tendo la ngono, zungumza na mwenzi wako. Hakikisha mnatumia muda mwingi kuandaana kabla ya tendo. Kutomasana taratibu kwa muda mrefu kabla ya ngono kutasaidia pia kukupunguzia uwoga na shinikizo linaloweza kusababisha mkakosa kujiachia.
- Ukihisi maumivu wakati wa tendo la ndoa, inaweza kusababisha ukawa na uwoga siku nyingine ukitaka kushiriki tendo na ikasababisha ukajikaza sana. Itasaidia sana kama kabla ya ngono mtatumia muda mwingi pamoja, kuchezeana, kuzungumza na kutomasana kabla ya ngono.
- Kama unatumia ‘’tampons’’ , hakikisha unaajiangalia usijekuwa umeisahau hapo ndani siku ya mwisho wa hedhi
Tafuta ushauri wa daktari kama
Panga kumwona daktari kama:
- Maumivu yataendelea hata baada ya kutibu sababu na kutumia njia za kujisaidia mwenyewe
- Unaanza kuona dalili nyingine , kama vile kutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ngono