Maelezo ya jumla

Magoti ni maungio yanayobeba sehemu kubwa ya uzito wa mwili, na kwa sababu hii ni rahisi sana kuteguka au kuumia. Unaweza kuwa na maumivu ya goti moja au yote, yanaweza kuwa yamevimba, yana joto ukigusa na inakuwa ngumu kujongesha. Ukigeuza kwa nguvu sehemu ya goti ni rahisi sana kuumia, na hii ni moja wapo ya sababu kubwa ya maumivu kwenye goti. Kukaza na maumivu ya muda mrefu ya goti mara nyingi yanasababishwa na kuvimba kwa maungio au vifuko vya majimaji vinavyozunguka goti “bursitis” (vifuko hivi vinasaidia kupunguza msuguano kwenye maungio ya goti) na yabisi kavu.

maumivu ya goti
Kushoto- Vifuko vyenye afya, Kulia -Vifuko  vilivyovimba “bursitis”

Mwone daktari haraka

Tafuta msaada wa kitabibu haraka:

  • Kama una maumivu ya goti ambayo ni makali sana na/au kama unaona goti limevimba, limekuwa jekundu na moto ukigusa na kama una homa
  • Kama unashindwa kutembea baada ya kuumia au kama unashindwa kuchezesha/kujongesha goti

Ni vizuri kupanga kumwona daktari:

  • Kama unawasiwasi wowote baada ya kuumia goti
  • Kama unaanza kupata maumivu kwenye maungio mengine na/au umekuwa ukipata maumivu ya goti kwa muda mrefu

Unachoweza kufanya mwenyewe ukiwa na maumivu ya goti

Kuna baadhi ya mambo unayoweza kufanya wewe mwenyewe nyumbani ili kupunguza maumivu ya goti na kuongeza mjongeo

  • Kama umeumia kwenye goti unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kukupa nafuu
    • Pumzisha mguu ulioumia. Epuka kufanya shughuli yoyote inayoleta maumivu au kufanya yawe makali zaidi. Kaa au lala ukiwa umeweka mguu wako mahala pazuri
    • Weka barafu ili kupunguza uvimbe na maumivu. Unaweza kuchukua barafu iliyopondwa kwenye mfuko ukaifunika na kitambaa chepesi kisha ukaweka eneo lililoumua, au chukua taulo chovya kwenye maji ya barafu, likamue kisha funga eneo lililoumia. Fanya hivi kwa dakika 10
    • Funga eneo lililoumia. Unaweza kufunga kwa kutumia ‘’elastic bandage’’ sehemu iliyoumia, hakikisha kuwa haukazi sana na kuzuia damu kupita. Bonyeza ukucha wa kidole kimoja mpaka rangi inapopotea kisha uachie, kama rangi ya damu itarudi haraka, ina maanisha damu inapita vizuri.

maumivu ya goti

    • Nyanyua mguu. Kunyanyua mguu kunapunguza mzunguko wa damu kwenda eneo liloumia na kupunguza damu kuvia mahali hapo. Unaweza kuunyanyua mguu kwa kuuweka juu ya kiti au mto. Jitahidi usiutumie mguu kwa masaa kadhaa ya mwanzo
  • Tumia dawa za maumivu. Madawa ya maumivu kama ‘’acetaminophen’’ na ‘’ibuprofen’’inayoweza kupunguza uvimbe pia.
  • Unaweza pia kutumia dawa za kuchua ‘’counterirritants’’. Dawa za kuchua zinapooza eneo linalouma na kupunguza maumivu.
  • Ili kupunguza mkazo kwenye goti, jitahidi kulijongesha mara kwa mara kadri maumivu yanavyopungua na kuruhusu. Unaweza kuendelea kuongeza mjongeo wa goti kadri maumivu yanavyopungua
  • Kama maumivu ya goti yanatokana na yabisi kavu ‘’arthritis’’, kutumia virutubisho kama ‘’glucosamine’’ au ‘’chondroitin’’ zinaweza kusaidia muda unavyokwenda. ‘’Glucosamine’’ na ‘’chondroitin’’ zinapatikana kwa asili kwenye gegedu za goti na kuzitumia inaweza kupunguza uvimbe na taratibu kupunguza mkazo na kasi ya yabisi kavu. Inaweza kuchukua angalau mwezi kuanza kuona mabadiliko.
  • Kama inahitajika punguza uzito, kwa sababu ukiwa na uzito mkubwa unaongeza shinikizo kwenye maungo ya goti
  • Vaa viatu vizuri, vinavyokutosha a visivyo na kisigino kirefu
  • Mazoezi ya mara kwa mara kama vile kupanda ngazi au kuendesha baiskeli, kutaimarisha misuli inayotegemeza maungio ya mwili.

Mwone daktari kama

Panga kumwona dakari:

  • Kama maumivu ya goti au uvimbe uliotokana na kuumia goti, hakupungui baada ya siku 2
  • Kama maumivu ya goti yanazidi kuwa makali zaidi
  • Kama unaaza kuona dalili nyingine ambazo hazikuwepo hao mwanzo

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003187.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *